Kwanini Historia ya Wachagga inafichwa Sana?

Hvyo ndivyo ilivyo mkuu mambo mengi hayafundishwi labda uwe msomaji somaji ndio utapata vitu vingi..... Ata uhuru utafundishwa kua Nyerere ndio alituletea lakini ukifatilia sana utakuta kulikua na watu wengi nyuma yake
Nyerere aliungana na wenzake walioanza harakati kabla yake.
Lakini mwenye akili ndiye huinuliwa zaidi.
 
Ila yeye kainuliwa zaidi na zaidi asee!!
Tunakoelekea historia lazima itawekwa vizuri ili kubalance mambo na ukweli, kumbuka tuliko toka, ilikuwa elimu duni, ukisimuliwa kijiweni ndio ilikuwa unageuzwa ukweli wa mambo, na waandishi wa historia kipindi kile hawakuwa na ubavu wa kwenda kinyume na Mwl Jk.
Historia za kweli zipo katika maktaba ya wazungu lkn pia nao wamejipendelea upande wao kuliko mashujaa wetu.
 
Tunakoelekea historia lazima utawekwa vizuri ili kubalance mambo na ukweli, kumbuka tuliko toka, ilikuwa elimu duni, ukisimuliwa kijiweni ndio ilikuwa unageuzwa ukweli wa mambo, na waandishi wa historia kipindi kile hawakuwa na ubavu wa kwenda kinyume na Mwl Jk.
Historia za kweli zipo katika maktaba ya wazungu lkn pia nao wamejipendelea upande wao kuliko mashujaa wetu.
Kweli mwl. nae alikua hataki mambo mengi yajulikane ila historia ikiwekwa sawa kama unavyosema itapendeza zaidi
 
Wakuu nimewahi kusoma vizuri Historia ya Wachagga kwenye kitabu kimoja kilichoandikwa na Msweden mmoja, akimzungumzia vyema Mangi Marriale Obe II, na Binti aliyekuwa anaitwa Sia,
Aliyesome udaktari huko Sweden,

Pia inaonekana Mangi Marriale Obe II alikuwa msomi, na Hadi mwaka 1954 alikuwa anakaribia kuhitimisha kuomba uhuru wa Wachagga waliokuwa wamefika mbali kimaendeleo bila msaada wa Wazungu, hicho kitabu kinaeleza vizuri kuwa Gavana wa Uingereza kipindi hicho alikuwa hachangii chochote kwenye maendeleo ya Wachagga, hawa walikuwa wanakatwa kodi kutoka kwenye zao la kahawa.

Mipango ya kibajeti ilikuwa inawekwa vizuri sana kupitia kodi hizo na nyingine mbalimbali,
Kulikuwa na mfumo mzuri wa Elimu, pamoja na Miundo mbinu.
Niliona bajeti kuu yao iliyochapishwa mwaka 1954.
Na kila mwaka walifanya mkutano mkuu wa Wachagga, uliokuwa unafanyikia Moshi...

Najiuliza ni kwanini Historia hii haisemwi popote katika utaratibu wa Mafundisho ya Historia!

Mkuu Malcom Lumumba nakupa copy hapa...na wanahistoria wengine
Hiyo historia haisemwi popote kwa sababu ni ya uongo. Wachagga waliendelea bila msaada wa wakoloni? Uongo.
Wachagga waliendelea kwa msaada wa wakoloni katika mpango wao wa divide and rule. Huu ulikuwa mkakati rasmi wa Governor Sir Donald Cameron katika sera yake ya indirect rule, na ukaendelezwa na magavana waliofuatia.
Jamii ziligawanywa:
  1. Kikabila: majimbo yaligawiwa kikabila, na ndani ya kila jimbo kulikuwa na machifu wa kila kabila, hata yale makabila madogo, waliopewa nguvu za ukibaraka kutawala kwa niaba ya wakoloni. Machifu wa enzi ya ukoloni (including huyo Marealle) walikuwa kama viranja tu waliotumwa kazi na wakoloni
  2. Kwa mgawanyo wa kazi: Wakoloni walihakikisha jamii za Tanganyika zinatengwa kwa mujibu wa kazi. Manamba wa mashamba ya mkonge na miwa walisombwa kutoka Kigoma, Rukwa, Mbeya na kupelekwa mashambani kwa treni. Askari KAR, magereza na polisi wengi wao walichukuliwa kutoka Mara, Tabora, Iringa. Makarani na walimu walitoka Kilimanjaro na Kagera nk. Hii yote ilikuwa kuhakikisha watanganyika hawawezi kuunganisha nguvu kama taifa.
  3. Kielimu: maeneo fulani fulani yalipewa elimu bora kuliko wengine na kuaminishwa kuwa wako tofauti sana na watanganyika wengine
  4. Kipato: Maeneo fulanifulani yaliwezeshwa kujipatia kipato kikubwa kwa mazao ya biashara. Kumbuka wakoloni wenyewe ndiyo walioleta mazao ya biashara ya kahawa, pareto, chai, mkonge nk, lakini kwenye maeneo mengine walinyang'anya ardhi wakawapa walowezi wa kizungu na kwenye maeneo mengine wakaruhusu wakulima wenyeji kulima mazao hayo kwenye ardhi yao na kuuza, mfano wake ni huo wa kahawa uchaggani. Hii ilivunja kabisa ule umoja wa kudai ardhi (aliyeruhusiwa kutumia ardhi yake hawezi kuungana na aliyenyang'anywa ardhi)
  5. Kiimani: serikali ya kikoloni ndiyo iliyoamua mgawanyo wa wamisionari wa kikristo kwenda kutafuta converts sehemu mbalimbali za Tanganyika. Katika kila jimbo, wamisionari walipangiwa maeneo tofauti bila kuingiliana, na walifundisha waumini wao kutengana na wa madhehebu mengine. Wakatoliki walifundishwa kuwatenga waprotestanti nk.
  6. Kimaendeleo: Wakoloni waliyapendelea maeneo fulani fulani ili yatofautiane na mengine na ili yasitamani kushirikiana na maeneo ya watu 'duni'. Mojawapo ya watu waliopendelewa na wakoloni kwa mtindo huo ni wachagga, hadi kufikia kujiona kuwa wao ni bora kuliko watanganyika wote, na hadi wakatamani wasiwe sehemu ya Tanganyika, na hiki ndicho kisa cha Marealle kutaka uhuru wa wachagga pekee! Mpango huu ungefanikiwa, ungewezesha wakoloni kuendelea kutawala kupitia uhuru bandia wa baadhi ya maeneo kama walivyokuwa wanafanya makaburu kule South Africa.
Kwa ujumla hakuna chochote cha kusifia kuhusu maendeleo bandia yaliyonasibishwa kwa machifu wa enzi za ukoloni, wote walikuwa waroho tu na njaa zao. Wazalendo wa kweli ni wale waliosimama dhidi ya wakoloni na vibaraka wao na kuwezesha nchi nzima ya Tanganyika kujitawala.
 
Mkuu nikikipata Kitabu nitakutumia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom