aise
JF-Expert Member
- May 16, 2018
- 7,459
- 20,963
Nyumbani kule kijijini kuna vikundi vinaitwa "vikundi vya maafa na kusaidiana"
Hivi ni vikundi unaweza kukuta kijiji kizima kuna kikundi kimoja au viwili.
Familia karibia zote wamejiunga, awe mwalimu au mkulima.
Ada ya kujiunga kwa mwanachama mgeni ni Tsh 2,000 tu.
Wanachama wake pindi mwanakijiji apatapo tatizo, hukusanyika na kuchanga kila mtu sh 500,
Hii mia tano ukizidisha kwa wanakijiji wote inapatika hela nyingi sana ambayo kwa kawaida inatosha matibabu na ghalama zingine.
Changamoto yake ni pale mwaka unaisha na kwenye familia yenu hakuna anayeugua, kwahiyo nyie itakuwa ni mwendo wa kuzitoa 500 kila ngoma ikilia.
Ila siku ukipatwa na matatizo lazima uyasahau machungu yote,
Maana kijiji chote watakuchangieni.
Kwanini hili jambo halipo mjini?