Safari_ni_Safari
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 23,263
- 17,140
Mitaala inayosema kuwa "samaki amepaiwa" kweli imenipiga chenga
Unatakiwa kusema "kupara samaki" na passive tense yake ni "samaki ameparwa"
Mnajua vitu vingapi vinaitwa PAA?
- Kupaa kwa kuruka
- Kupaa samaki
- PAA la nyumba
- PAA kama mnyama
Kupaa samaki ndio kufanya nini?
Kama ni kile kitendo cha kumtoa magamba, basi samaki hapaiwi bali huparwa
basi kama ni hivyo kuna kuparamiwa na kupara
samaki
Kumtoa magamba samaki ni kumparapata.Kuna kuparamiwa, kupara miwa na kupara samaki
Kunanyimbo moja ya msondo inasema:
Ulitaka kuolewa, utampara samaki
Samaki huyo wa tasi, utampara samaki
Ana mwiba katikati, utampara samaki
BwanJuma huyo BwanJuma, ana mliowe akwereza
Akwereza vipi? Kwarara Kwarara
Ana mliowe akwereza Akwereza
Mitaala inayosema kuwa "samaki amepaiwa" kweli imenipiga chenga
Unatakiwa kusema "kupara samaki" na passive tense yake ni "samaki ameparwa"
Hivi inaitwa mbuzi au kibao cha mbuzi?
Hao Msondo nao wana mambo... hivi tasi unampara vipi wakati hana magamba?Kuna kuparamiwa, kupara miwa na kupara samaki
Kunanyimbo moja ya msondo inasema:
Ulitaka kuolewa, utampara samaki
Samaki huyo wa tasi, utampara samaki
Ana mwiba katikati, utampara samaki
BwanJuma huyo BwanJuma, ana mliowe akwereza
Akwereza vipi? Kwarara Kwarara
Ana mliowe akwereza Akwereza
Hao Msondo nao wana mambo... hivi tasi unampara vipi wakati hana magamba?
Umenifanya nikafungue kamusi na linasema:
Para, v., also paa, v. ?........scrape, graze
Licha ya kuwa yote yana maana sawa, sijui passive tense yake
Samaki amepaiwa?
Labda kuparura
Hii ndiyo mbuzi ya awali. Swali la kuuliza ni kwa nini yule mnyama anaitwa mbuzi, ndiye kaiba jina.
Tangu ninazaliwa hadi umri huu, nimesikia tangu bibi zangu, shangazi na mama zangu wakisema "kupara samaki" na passive tense yake ikiwa "samaki wameshaparwa" kama kamusi lilivyo ainisha
Anaetumia "kupaa samaki" atalazimika kutumia "samaki amepaiwa" na si "samaki ameparurwa" maana mizizi yake hailingani
Besides, kupara (kupaa) na kuparura yana maana tofauti
Mie nina jibu la ukweli ila kwa sharti la kwanza kwako Mbuzi mzee...ebu badilisha avatar yako iwe mbuzi ya kukuna nazi (yaani uwe mbuzi mzee cha kukuna nazi) ....Jibu lake hutakubaliana nalo
Mie nina jibu la ukweli ila kwa sharti la kwanza kwako Mbuzi mzee...ebu badilisha avatar yako iwe mbuzi ya kukuna nazi (yaani uwe mbuzi mzee cha kukuna nazi) ....Jibu lake hutakubaliana nalo