Kwanini Herod Antipas aliitwa Mbweha na kwanini watu wa Mataifa wanaitwa Mbwa?

Kwanini Herod Antipas aliitwa Mbweha na kwanini watu wa Mataifa wanaitwa Mbwa?

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
5,527
Reaction score
7,121
Majina ya wanyama katika Biblia ni lugha ya picha iliyotumiwa kama kielelezo cha tabia, nafasi, au hali ya kiroho. Ni muhimu kuyasoma kwa muktadha sahihi wa kitamaduni na wa kimaandiko. Hii inasaidia kuelewa vizuri mafundisho ya Biblia na jinsi Mungu anavyowasiliana na watu kwa lugha inayoeleweka kwa wakati huo.

Mara nyingi katika tamaduni za Mashariki ya Kati, watu walipoitwa kwa majina ya wanyama, lengo halikuwa kutukana, bali kuelezea tabia, uwezo, nafasi au hali fulani ya kiroho ya mtu. Hii ni tofauti na nchi nyingine ambapo majina ya wanyama hutumiwa na watu kama matusi.

Hii hapa baadhi ya mifano katika Biblia inayoonyesha jinsi majina ya wanyama yalivyotumika kwa namna ya heshima au ya kiakili, kulingana na muktadha:

1. Yesu anaitwa "Simba wa kabila la Yuda" (Ufunuo 5:5). Hili ni jina linaloonesha mamlaka, ujasiri, nguvu na uongozi. Simba alijulikana kuwa mnyama mwenye nguvu na anayeheshimiwa sana katika jamii. Kwa hiyo, jina hili linamtambulisha Yesu kuwa ni Mfalme mwenye nguvu.

2. Herod Antipas aliitwa Mbweha
Yesu aliposema, “Mwambieni mbweha huyo…” (Luka 13:32), hakumtukana Herode bali alimtaja kwa sifa yake ya hila na ujanja ujanja. Katika jamii za Mashariki ya Kati, mbweha alionekana ni mnyama mjanja, asiye na nguvu na ujasiri wa kweli kama simba. Kwahiyo, watu waliokuwa wakifikiri kwamba Yesu alimtukana Herod Antipas, nadhani wamepata jibu hapa.

3. Shetani anaitwa nyoka kwa sababu alijivika umbo la nyoka ili kumjaribu Eva katika bustani ya Edeni. Katika Biblia, nyoka anawakilisha hila, udanganyifu na uovu — sifa alizo nazo shetani.

4. Yesu alipomwambia mama Mkananayo, “Si vema kuwapa mbwa chakula cha watoto,” (Mathayo 15:26), hakumtukana. Katika muktadha huo, ‘mbwa’ ni jina lililowakilisha watu wa Mataifa (wasio Wayahudi), waliokuwa nje ya agano la Israeli kwa wakati huo.

5. Katika Mathayo 25:31–46 Watakatifu wanaitwa Kondoo na wenye dhambi wanaitwa Mbuzi. Nadhani hakuna asiyejua sifa au tabia za kondoo na mbuzi.
 
Unaposoma Biblia kumbuka kuisoma kwa muktadha na kwa kutafakari mila na desturi za watu wa mashariki ya kati. Utamaduni unaokubalika Israeli, sio lazima ukubalike Afrika au katika nchi za magharibi. Ndio sababu, katika nchi nyingine ukimuita mtu fulani "mbwa" ni kosa kubwa sana.
 
Nguruwe wanaotajwa katika andiko hili ni wanyama au ni watu? Kama ni watu kwanini wanaitwa nguruwe? Nguruwe wanawakilisha sifa au tabia gani?
Mathayo 7:6 BHN
“...msiwatupie nguruwe lulu zenu wasije wakazikanyaga."
 
Katika 1 Kor 9:9 imeandikwa: “Usimfunge kinywa ng'ombe anapopura nafaka.”

Je, ng'ombe anayetajwa katika andiko hilo ni ng'ombe kweli, au ni lugha ya picha inayomwakilisha mtu fulani?
 
IMG_20250610_204958.jpg
 
Lucas, narudia tena lala upate muda wa kunyanduliwa
Lucas ni nani? Halafu wewe usifikiri utaishi milele duniani. Mungu hadhihakiwi. Upandacho ndicho utakachovuna(Gal 6:7-9)
 
Lucas ni nani? Halafu wewe usifikiri utaishi milele duniani. Mungu hadhihakiwi. Upandacho ndicho utakachovuna(Gal 6:7-9)
Lucas ni msifiaji Kama Wewe. Sifa na utukufu anapaswa kupewa Mungu tu sio watawala. Narudia tena lala
 
Lucas ni msifiaji Kama Wewe. Sifa na utukufu anapaswa kupewa Mungu tu sio watawala. Narudia tena lala
Wewe Biblia huisomi. Vinginevyo ungeishasoma andiko hili:
1 Wakorintho 11:2, ambapo Mtume Paulo anasema:
“Basi nawasifu, ndugu zangu, kwa kuwa mnayakumbuka mambo yangu yote, na kuyashika maagizo kama nilivyowapa.”

Inaonekana pia nyuzi zangu huzisomi? Hawa nimewasifia wapi?
 
Basi nawasifu, ndugu zangu,
Kama ndugu tu wanasifiwa, sembuse watawala?
Tatizo wewe Shadow7 unawaza tu NRNE badala ya kuyawaza yaliyo juu Kristo aliko. Btw nimesikia shughuli zenu zimepigwa ban, ni kweli?
 
Kama ndugu tu wanasifiwa, sembuse watawala?
Tatizo wewe Shadow7 unawaza tu NRNE badala ya kuyawaza yaliyo juu Kristo aliko. Btw nimesikia shughuli zenu zimepigwa ban, ni kweli?
Ni Kweli mkuu, wamepiga ban kwa siku 14
 
lugha katika masuala ya dini imejaa kauli za kiubaguzi. hili linanikera sana. utasikia wakristo wanawaita wengine wapagani mara waislamu wanawaita wnzao makafiri.
 
Ni Kweli mkuu, wamepiga ban kwa siku 14
Duh, poleni sana. Inaonekana Mungu hayuko upande wenu. Vinginevyo kwanini mambo yenu hayafanikiwi? Angalieni ni wapi mlipoanguka, mkatubu(Ufunuo 2:5)
 
herode antipass mocked jesus christ
Yes, Okoth p'Bitek
Herod Antipas did mock Jesus Christ during His trial, according to the Gospel of Luke.
That episode shows that Herod Antipas was complicit in the humiliation of Jesus, treating Him as an object of entertainment rather than with seriousness or respect.

Jesus’ silence before Herod Antipas fulfilled Isaiah 53:7, a messianic prophecy:
"He was oppressed and afflicted, yet he did not open his mouth;
he was led like a lamb to the slaughter, and as a sheep before its shearers is silent,
so he did not open his mouth."


By staying silent, Jesus aligned with the image of the suffering servant who submits to unjust treatment without protest.
 
Back
Top Bottom