Kwanini Hayati Rais Magufuli alishindwa Kudhibiti 'SIRI' za Serikalini 'Kuvuja' ila kwa Rais Samia ameweza kwa muda mfupi tu huu?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,571
108,926
Hapa wala tusidanganyane kuna 'Mtu' hivi sasa kila akija na Taarifa na Kujiamini nayo kabisa ama inakuwa ya Uwongo au hata isitokee kabisa na kabaki tu 'Kupuyanga' na Umaarufu wake taratibu kuanza Kushuka.

Hata hivyo GENTAMYCINE hapa nina Maswali mengi sana ya kwanini kwa Uongozi wake Hayati Rais Magufuli kulikuwa na uvujaji mkubwa wa SIRI za Serikali (ambazo 85% ) zilikuwa za Kweli lakini ndani ya muda mfupi tu wa Uongozi wa Rais Samia SIRI nyingi za Serikali zimedhibitiwa na wala hazivuji tena kitu ambacho nakipongeza sana.

Taratibu sasa naanza kuielewa ile Kauli ya Rais Samia kuwa Watu wa Mitandaoni hasa Wazushi au Wapotoshaji ( siyo GENTAMYCINE ) siku zao zinahesabika na muda wowote ule watakamatwa (mtakamatwa)

Pia GENTAMYCINE nimeanza Kuamini kuwa kuna Uwezekano mkubwa sana Hayati alikuwa 'amewakumbatia' Maadui zake huku Yeye akidhani ni Wana ( Marafiki ) zake ambao huenda ndiyo hao hao ndiyo walikuwa 'Wakivujisha' Taarifa zake nyingi ambazo zingine ni za Maisha yake binafsi kabisa.

Vile vile GENTAMYCINE nimeenda mbali zaidi kuwa huenda hata 'System' ya nchi hii iliyokuwa na dhamana Kubwa Kwake nayo ilikuwa imeshagawanyika na kuwepo kwa 'Mpasuko' mkubwa hali iliyopelekea Taarifa 'Nyeti' za kuanzia Ikulu hadi Serikalini kwa Watendaji na Wateule wake 'Kuvuja' kwa wingi mpaka Kwetu Sisi Watu wa kawaida (Mangumbaru)

Kwa Kitendo hiki cha muda wake huu mfupi tu Uongozini kwa Rais Samia SIRI nyingi za Serikalini 'Kutokuvuja' kama ilivyokuwa kwa Hayati Rais Magufuli GENTAMYCINE nimeanza Kuamini kuwa waliotulia sasa 'Kutozivujisha' wamemkubali, wanamheshimu na wanampenda vilivyo Rais Samia na huenda hata Yeye Rais Samia anawakubali.

Mwisho kabisa GENTAMYCINE naanza kuielewa vyema ila Kauli ( Msemo ) wa Kihenga usemao KIKULACHO KI NGUONI MWAKO na kwamba ANAYEKUMALIZA ANAKUJUA VYEMA kabisa.

Baada ya Kutathmini kwa mbali sana Kuna Kitu 'Kimenishtua' na GENTAMYCINE najua kuwa Kazi ya Kuzitwaa Roho za Sisi waja wake ni yake kwa Uratibu mzuri wa Israeli, ila kwa Mtazamo wangu binafsi ( na mtanisamehe kwa wale nitakaowakwaza ) naona Kuondoka ghafla vile ( Kufariki ) kwa Hayati Rais Magufuli 'Kuliratibiwa' na Kundi fulani na kwa 'Makubaliano' fulani pia.

Sina tu uwezo ila kama ningekuwa nao ( kwa nia njema tu ) ningeomba Kuundwe Kamati 'Maalum' ya Kuchunguza Kifo chake na tusiishie tu katika 'Kuaminishwa' kuwa ni tatizo lake la Moyo alilokuwa nalo muda mrefu ndiyo limeuondoa Uhai wake.

Kuna Watu ( Wazee ) nawajua wana Matatizo ya Moyo tena Makubwa tu kuliko la Hayati lakini hadi hivi leo 'tunadunda' nao Mitaani na hata katika Nyumba za Kulala Wageni tunapishana nao 24/7 kama Dalalada za Mbagala - Stesheni wakiwa na 'Totooz' za maana.
 
Ukiona siri zako zinatoka ujue una maadui wengi au watu wanatafuta what next ? hutabiriki.Mama wanajua hakurupuki ,anakuandaa,anakutafuta,unamkosoa nk.So watu hawaogopi kuwa kuna surprises.JIWE alijenga mfumo ambao sio rafiki wa utoaji habari na utekelezaji wa kazi zake
 
Uko sahihi....

Trace matukio mengi ya kisiasa ndani ya CCM.

Wale wazee kuandika waraka wakimsema musiba kwa namba moja.

Pia kulikua na kauli ya wastaafu wanawashwa washwa....etc.

Plus hayati kutaka kuongeza muda na bunge kuanza kutaka kuijadili mada ya namba moja yule kukaa zaidi ya 10 yrs na navyolijua bunge kweli lingepitisha azimio la kutengu katiba muda wa URAIS wa hayat uongezwe .

Ukitaka kujua na kama mtaalamu angalia picha za wale walinzi wa hayati,anzia na ADC wake ,wale PSU ukiangalia facial expressions zao unajua kabisa wana mengi walikua wanaambiwa na hayati au wanayajua hayati alikua anawambia.

Sura zao zina mengi ya kusema ila kikatiba hawawezi.

Mambo yalikua mengi sana na ilibidi hayati atangulie tu.....
 
Nimejiuliza iki kitu lakini nikajiuliza pia au Namba 1 wasasa naye alikuwa mnyetishaji?
Kwa hiki ulichokihoji hapa Mkuu kama tuko Makumbusho ndani ya Dalalada tunaelekea Posta basi hivi sasa tupo Kituo cha Palm Beach.

Nina yangu ya Moyoni ila ngoja tu ninyamaze na nimuombee tu Hayati Makazi mema huko 'alikolazimishwa' kwenda.
 
Huyo unayempongeza ndiye alikuwa mnyetishaji wa hizo ulizoita siri-kali, au pengine shemasi hana haja na nyeti za mama!
 
Nina hamu uanzishe mada ya tetesi ya Kifo cha Hayati na kundi lililoratibu kwa makubiano maalumu. Pia wamekubaliana na nani bila kutaja majina ya wahusika, taja wajihi tu. Naisubiri Sana mada hii, hata bungeni Mama kagusia hili Jambo.
 
Back
Top Bottom