Kwanini hawa wanaweza wengine washindwe

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Katika kutafuta maisha nilipanga nyumba moja na vijana watatu kutoka nchi za Kiarabu. Vijana hawa walitoka Syria, Lebanon na Iraq. Umri wao wote walikuwa kati ya 23-26, wote walikuwa wanafunzi.

Vijana hawa walikuwa na maumbo na sura za kuvutia na wasichana wa kizungu waliwapenda sana. Vijana hawa wote hawakuwa na girlfriends.

Kwanza waliishi kama ndugu, yule aliyetoka Iraq ya miaka hiyo alikuwa na full government sponsorship, hawa wengine walikuwa wanasomeshwa na wazazi wao. Walipika pamoja na kula pamoja. Wasipokuwepo ndani watakuwa msikitini au shuleni.

Waliheshimu kila mtu na walikuwa wacheshi sana. Niliwauliza mbona mnawatesa hawa wadada wa kizungu wanakuja mpaka hapa kuwatembelea lakini hamchangamkii tenda. Walinijibu wao hawajawahi kufanya mapenzi na watabaki hivyo mpaka waoe.

Sasa ninajiuliza hii discipline ilipotelea wapi katika jamii yetu? Ni wazi kuwa hakuna dini inayokubaliana na zinaa.
 
Aisee sisi tumejaliwa kujaribujaribu tukiona haina maradha na ni tamu ndio unskuwa mchezo wetu sisi ni watofauti !!
 
Bila shaka hawakukuacha salama
 
Hawa hawana watoto wa nje kila kona, mapenzi anayaanza na mke wake. Lakini fikiria kijana ajitunze hivyo alafu aoe ambae si bikra.
 
Ilikuwa mwaka gani?
 
Jibu rahis ...malezi. hawa waarab wana misimamo sana na wanafundishwa ethic fulani za jamii yao mpaka wanapokuwa wakubwa wanakuwa wako vizur sana. Which ni kitu kizuri
 
bongo ukifanya ivyo, hawakawii kukusambazia ruma mtaani kua wewe ni hanithi, shoga, haisimami, mchele mchele!
Jamii ya kibongo achana nayo bwana. Ndio walivyo. Jamii ya wa waarab kwenye misimamo nawakubali sana
Wako strict
 
Wanaogopa kupigwa mawe mpaka kuuwawa. We unafikili adhabu kama hizo zingekwepo bongo kuna mtu angeunganisha vikojoleo?
 
Fikiria kama ndo wewe umekuja room kwangu halafu umeondoka sijakuvua, wewe kama mwanamk wa kitanzania kabisa utachukuliaje
 
Ni jambo jema sana, sema tunamsingizia sana shetani. Naamini walioolewa/waliooa na umande wao wapo so proud.
 
Ngoja waje wakuulize hapa kwanini walipewa vikojoleo kabla ya ndoa kama lengo lilikuwa wavitumie ndani ya ndoa,hapo ndo utawaelewa wabongo.

[emoji117][emoji117][emoji117][emoji117] sababu ni malezi,wenzetu wanasheria kali sana.
 
Sasa kikojoleo kimoja kikihisi uwepo wa kiingine chenyewe kinasimama na kuelekea uelekeo huo unahisi nn apo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…