Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,372
Siku 3 au 4 zilizopita niliona kupitia Star tv mtoto mdogo akiwa na uvimbe mkubwa sana usoni uvimbe ambao matibabu yalishindika kufanyika hapa ndani ya nchi.
Kwa mujibu wa Star tv,mtoto huyo alitibiwa hospitali ya mkoa Mbeya,hospitali ya kanda na baadae hospitali ya Taifa Mhimbili ambako nako matibabu yake bado yalishindikana na anatakiwa kupatiwa matibabu nje ya nchi.Kwa waliomuona mtoto huyo bila shaka watakubaliana nami kuwa picha ile inasikitisha na kuumiza sana.
Mtoto huyo anaehangaika na mama yake kujitokeza katika vyombo vya habari kuomba msaada wa fedha ni mfano tu wa watanzania wengi ambao wamekuwa wakijitokeza katika vyombo vya habari kuomba msaada wa wasamaria wema katika kugharamia matibabu yao ndani na nje ya nchi.
Jambo hili huwa linaniumiza sana na nakumbuka niliwahi kuliongelea hapa JF siku za nyuma. Kinachonisikitisha na kuniumiza ni kuona watanzania hawa wanaoteseka na maradhi haya wakijitokeza mbele ya camera ili tu kuomba msaada wa fedha ili hali serikali yao ipo!Serikali ni kwanini inashindwa kuwa na sera ya kugharamia matibabu ya watu wake kwa magonjwa yaliyoshindikana kutibiwa hapa nchini?
Haingii akilini kuona Raisi,Raisi Msaafu,Makamu wa Raisi Mstaafu, Waziri Mkuu,Waziri Mkuu Mstaafu,Mawaziri,Wabunge na Vigogo wengine Serikali wakitibiwa nje ya nchi wakati mwananchi masikini akiteseka kwa maradhi huku akiomba msaada wa matibabu kutoka Taasisi na watu binafsi ili kuokoa maisha yake. Tukumbuke serikal ndio yenye wajibu wa kujenga hospitali na pia kutoa ruzuku kwa hospitali hizi ili mwananchi wake apate huduma bora za afya na kama imeshindwa basi serikali ndio ina wajibu wa kumgharamia mtanzania huyu apate matibabu popote pale ndani na nje ya nchi.
Pamoja na kuwepo utaratibu wa "cost sharing" katika hospitali za umma, watanzania wengi hawana bima za afya, hawamudu gharama kubwa za matibabu kwa baadhi ya magonjwa na hata matumizi ya Bima za kawaida nayo bado yako limited kwa baadhi ya magonjwa.
Nafikiri wakati umefika tuwe na sera ya kugharamia matibabu yaliyoshindikana ndani ya nchi na baadhi ya magonjwa yanayotibika hapa nchini lakini yanagharama kubwa sana kwa mtanzania wa kawaida.
Kiongozi mzuri,awe Raisi,Waziri au Mbunge,ni yule atakaetumia nafasi yake serikalini au ndani ya Bunge kuhakikisha tunakuwa na sera ya aina hii si kila wakati viongozi hawa kujitolea kugharamia matibabu ya watanzania hawa kila wanapojitokeza katika vyombo vya habari kuomba misaada.
Nakumbuka hivi karibuni ilitoka taarifa kuwa serikali inajiandaa kusitisha kupekeka watu nje kwa ajili ya matibabu kwa kuboresha hospitali ya Muhimbili ila binafsi naamini bado tu kuna magonjwa hayatatibika hapa nchini na hivyo serikali haiwezi kukwepa jukumu hili ambaolo mara nyingi ni kugharamia vigogo wa serikali na si mwananchi wa kawaida.
Kama kuna sera ya aina hii(jambo ambalo siliamini),basi sera hiyo na sheria zake zitakuwa mbovu na zenye mapungufu makubwa kwani zitakuwa hazina msaada sana kwa mtanzania wa kawaida na hivyo zinatakiwa(kama zipo) kupitiwa upya.
Wabunge wote bila kujali vyama vyenu mna wajibu wa kupeleka hoja binafsi Bungeni juu ya jambo hili na si kuisubiri serikali ambayo kila wakati inahitaji kusukumwa au chama chake ku-copy na ku-paste sera za wenzao kama vile ile sera ya elimu bure, n.k.