Kwanini hamuangalii Bongo Movie?!

Naona waigizaji wa bongo movie mmeamua kujipigia promo, poleni
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] noma sana mkuu
 
Nikwambie kitu,Bongo movie watu bado kuwekeza pesa vizuri,kwa mfano muandishi wa script hawezi kuwa mtu mmoja lazima awe ni mtu mwenye firm na timu ya wataalam ambo wanweza kutengeneza multiple versions za scene moja.Subtitles lazima kuwa na wataalam wa lugha waliosomea lugha za watu sio makanjanja wa mtaani.Watu wa kutengeneza story lazima iwe ni timu ya watu sio mmoja ambao wanaangalia flow ya story mpaka ikamilike na kuwa na version kadhaa.Bongo movie wao ni kamera basas wanatoa movie kumbi movie kwanza lazima uistage kwenye jukwaa kwanza ikiweza kumvutia mtazamaji kwenye jukwa basi ndio mnaenda kutafuta locations zitazovaa ila image anayopata msikilizaji.

Bongo movie inahitaji uwekezaji mkubwa nagharama wanzatumia kutengeneza hivi vimuvi vya mwendo kasi wangewekeza kutengeneza Movie zenye stori nzito na kuweka hesabu zao sawa wangefika mbali sana.Sasa unatengeneza movie yenye bajeti ya milioni chache halafu unataka ikuingizie milioni nyingi.
 
Hahahaaa...to digi medicine" ilikuwa movie gani hiyo mkuu nami nikacheke niongeze siku
 
Bongo Movie's si ilikufa na Kanumba?.

Baadhi ya sababu;..

Ngono; Hii ni sababu mama ya kutokutizama Bongo Movies. Rushwa ya ngono imekuwa sababu kuu ya mtu kuingia kwenye Tasnia ya Filamu Nchini. Yaani bila umbo, makalio, nyonyo za kuamsha hisia, sura nzuri huigizi. Hakuna kutizama vigezo vingine. Sijui kipaji, uwezo mzuri kiakili (Up-stairs medula), Elimu nzuri na orodha inaendele... Ukiwa na hivi vigezo unaonekana mshamba kweli.

Bonde la Ufa vichwani; Pia ni sababu ya kutotizama Filamu za hapa nyumbani. Waigizaji wengi, waongozaji nk ni weupe mno vichwani. Ubunifu hakuna, yaani ni kama vile mtu kushindwa kuuza Ubuyu na kuona Bongo movie ndio mpango mzima. Huwezi kufanikiwa kama kichwani haupo vizuri. Ni kanuni ya Dunia.

Kutumika kisiasa/ Ki-soka; Ukishakubali kutumika, basi ni lazima ukubali kudharaulika. Bongo movies wengi wanatumika vibaya na wanasiasa. Kugawa mashabiki ni kosa kubwa mno kwa muigizaji. Hifadhi mhemko wako. Kwani kuna ulazima wa Kujionesha kuwa U-CCM, CHADEMA, ACT-Simba, Yanga, Azam na kadhalika?. Ukimgawa shabiki basi tegemea kula mabua.

Madawa ya kulevya/drug's; Madawa ya kulevya ni hatari mno kwa Maisha ya msanii. Kama una uwezo mdogo kimapato basi tegemea kuwa kile kidogo utakachokipata utakielekeza kwenye madawa na mwishowe kuishia kuporomoka ki-tasnia, kiafya na mengine mengi. Bongo Movies wengi ni wabwia Unga. Ukibwia unga, mashabiki lazima wakupike.

Hizi ni baadhi tu ya sababu. Unaweza kuongeza mpaka zifike Mia.
 
zina changamoto nyingi bongo movie kama sio story nzuri basi waigizaji sio wazuri. Tatizo watu hawagawani kazi huwezi wewe ukaandaa story harafu wewe mwenyewe ukawa final editor ....lets say wewe ni fundi nguo ukishona next person aseme umeshona vizuri na sio wewe useme nimeshona vizuri.....ideally kazi ya kutengeneza movie ni kazi ya watu wengi sana tena sana na na ndio maana wenzetu mbele wanaandaa movie kwa miaka kadhaa
 
Uhuni mtupu!
Mmomonyoko wa maadili!
Waigizaji unakuta wanavaa vichupi, wanaume milegezezo, kuvaa heleni, kujichubua , n.k
 
=story nyingi visa ni vile vile pia mikasa (like mapenzi sijui fumanizi ).

=creativity zero.

tunajua movie ni act, lakini hawawezi kufanya hiyo act iendane na uhalisia.. mfano
-mtu ameamka asbh usoni make up, kavaa hereni
-jambazi lazima avae koti refu jeus na ni lazima awe kauzu
-mlinzi wa getini lazima dishi liwe linacheza(lofa fulani hivi)
-jambazi wanaenda kuvamia sehem wanavua viatu ndio waingie ndani ? .

=haka kamchezo ka part one na two kanakera, alafu ni uzamani

=matangazo almost dakk karibia 20 mwanzoni mwa movie(japo sio zote).

kwa kifupi zina mapungufu mengi sana, licha ya kuiga unaijeria lakini bado. hizi picha niliacha kuangalia kitambo sana, kabla hata ya king wao kanumba hajafariki. huwa sijui chochote khs bongo movie kwa sasa.
 
Hatuna muda na mambo ya kihuni!
Waigizaji wa zamani walikuwa wakivaa mavazi yenye staha na lugha ya staha! Nakumbuka enzi Za "mambo hayo"
Sasa siku hizi mmweeee?!
Yani nina miaka chungu nzima sina mda yangu nilipogundua Kumbe ndivyo walivyo!
 
Aya shemeji
 
Kwa hiyo unaposti ukiwa umefichwa Zenji na Mume? kweli anatuangusha saana Wanaume wa Kisukuma. Ningekuwa mimi usinge hata comment achilia mbali kuanzisha uzi hapa
Tulia wewe acha umbea
Kila jambo na wakati wake
 
Nyie mnasema bongo movie mbaya mbona namwona hadija kopa hapa anaigiza
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…