Kwanini hakuna salam wala msaada kutoka nchi zinazotuzunguka kuhusu janga lililotokea huko Katesh Manyara?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Tumekuwa wepesi kupeleka watu,mali na kutoa salam za pole pale janga au maafa yanapowakumba majirani zetu.

Leo ni siku ya tatu hakuna jirani aliyetukimbilia aidha kwa misaada au hata pole ya maandishi. Hawa majirani hawana taarifa ya matatizo haya wanayopitia ndugu zetu?

Lakini pia hakuna Ubalozi Nchini uliotoka adharani kutoa pole ya maandishi kupitia vyombo vya habari na website zao. Je wangekuwa viongozi hata wawili tu ndio wamepata gharika hii nakupotea au kupoteza wapendwa wao hizi taasisi zingekaa kimya?

Ubinadamu kwanini umeelekea zaidi kwa wale wenye nacho? Kwa nini Tanzania tunaanza kutengwa hata na majirani?
 
Sisi ni matajiri mno yaani sisi ni dona kantire hatuwezi kupokea misaada kutoka kwa masikini
 
Tumekuwa wepesi kupeleka watu,mali na kutoa salam za pole pale janga au maafa yanapowakumba majirani zetu.

Leo ni siku ya tatu hakuna jirani aliyetukimbilia aidha kwa misaada au hata pole ya maandishi. Hawa majirani hawana taarifa ya matatizo haya wanayopitia ndugu zetu?

Lakini pia hakuna Ubalozi Nchini uliotoka adharani kutoa pole ya maandishi kupitia vyombo vya habari na website zao. Je wangekuwa viongozi hata wawili tu ndio wamepata gharika hii nakupotea au kupoteza wapendwa wao hizi taasisi zingekaa kimya?

Ubinadamu kwanini umeelekea zaidi kwa wale wenye nacho? Kwa nini Tanzania tunaanza kutengwa hata na majirani?
Kwa upande wa misaada, 'we are a donor country.'
 
Bila shaka watawala wetu watapunguza sasa kujipendekeza na kujitutumua. Nakumbuka sana namna walivyo jipendekeza kwa Msumbiji, Kenya, Malawi na Uturuki.

Halafu leo hii wamekufa zaidi ya wananchi 60 kwa mafuriko, serikali hiyo hiyo ya kujipendekeza kwa wengine; inapamabana yenyewe! Yaani hata pole tu ya mdomo hakuna!! Malawi walipeleka mpaka ndege, waokoaji, vyakula, nk!!!
 
Ni aibu tupu
 
Katika kila matatizo kuna la kujifunza, lakini kama tumeweza kutenda vyema kwa majirani nyakati zao za shida na kwetu wakakaa kimya tumechukua somo na tunasonga mbele.

Tenda wema nenda zako ila sasa kuna la kujifunza zaidi kuhusu wema huo.
 
Kwa kawaida, ushiriki wa mataifa mengine kushiriki katika uokoaji au kupunguza athari kwa nchi iliyoathirika, unategemea sana weledi wa Wizara yenu ya mambo ya nchi za nje.

Watu hawawezi kutoka huko eti waje kukusaidia bila ya kuwa na details zozote. Waje wafanye nini? Kama humu humu ndani, watanzania wengi hawaelewi hata janga lenyewe, wanasema kuwa eti ni mafuriko, huko nje ya nchi, itakuwaje?

Kule Mozambique ilivyoyokea tu lile janga la kimbunga, ndani ya masaa 24 helicopter za uokoaji zilikuwa tayari zimefika toka South Africa, zikaanza kuwabeba watu na kuwapeleka maeneo salama. Ina maana balozi wa Mozambique nchini Afrika Kusini, alikuwa na taarifa sahihi, na haraka aliifikisha kwa Serikali ya South Africa, akitoa taarifa sahihi ya aina ya msaada wanaouhitaji waathirika, ambao wao Serikali ya Mozambique hawana uwezo wa kuutoa haraka.
 
Media zenyewe asubuhi mpaka jioni bado wako na umbea mipira miziki

Ova
Tanzania hakuna kitu kinachoenda kwa kutumia akili. Huko kwenye vyombo vya habari, ndiyo hakuna kitu kabisa. Akili zote zimeliwa na CCM. Wanachoelewa kuwa ni habari ni safari na hotuba za viongozi tu.

Tungekuwa kwenye nchi ambazo wanahabari wanaishi kwa akili zao na weledi, janga hili lingekuwa lipo kwenye live coverage masaa 24.
 
Back
Top Bottom