Kwanini General Chiwenga Anacheka Na Mfungwa Wake?

Jeshi la Zimababwe linatambua Comrade Robert Gabriel Mugabe ana wafuasi wa kutosha ndani ya ZANU PF,Jeshini na Uraiani ndio sababu kwa maslahi mapana ya Zimbabwe CDF kakataa kuonesha Siasa za Chuki na kuligawa Taifa.

Uwezo wa kumuondoa Mugabe kinguvu wanao na upo lakin hawajaona busara hiyo kwa kuwa itakuwa ndio chanzo cha chuki na Mgawanyiko ndani ya Taifa lao kama inavyoshuhudiwa Egypt baada ya kuondolewa Hosni Mubarak na Mohamed Mursi.
 
Hii move nakubaliana kabisa ni ya kumzuia Grace na wala si kumuondoa Mugabe
Ndio sababu kubwa hiyo ili Grace asitawale
Halafu alikuwa na mbwembwe sana maana alijua kwa vyovyote yeye ndie Rais
Maneno yake yalikuwa ya kuudhi sana wazee wakaona hapa ni kushika kwa mabavu tu
She bites off more than she can chew.
0cb009124827c8e64dfe19b801af2d84.jpg
c39c0163f4c57a821f61e387c60f2610.jpg
 
Shida ni kuwa jeshi halitaki nchi kuongozwa na mwanamke...hiyo ni mwiko kwa africa...hata wamarekani hilo hawawezi kulikubali....jeshi linajaribu kumweka sawa mzee..asidhubutu kumwachia huyo manzi na badala yake atafte mtu mwingine
Liberia iko bara gani ?
 
Ndo hata mm nashangaa hicho kibabu kilichoharibu uchumi ilitakiwa kiwe jela kikakutana na kiliowaweka jela, kinaishi maisha mazuri wakati wananchi wako hoi.
 
Zimbabwe Nyuma Ya Pazia:

Kwanini General Chiwenga Anacheka Na Mfungwa Wake?

Ndugu zangu,

Picha hiyo imeishangaza dunia. Kwamba Rais aliyepinduliwa na kuwekwa kwenye kizuizi cha nyumbani ' House Arrest', anatembelewa na kiongozi wa mapinduzi. Wanakaa kuongea, kunywa chai pamoja na kucheka.

Lakini, waliojitahidi kuifuatilia Zimbabwe kabla na baada ya uhuru watakubaliana nami, kuwa hilo si la ajabu kabisa.

Army General Constatine Chiwenga na Robert Mugabe ni marafiki. Ni makomredi waliofahamiana tangu zama za Chimurenga- Mapambano ya msituni kupigania uhuru wa Zimbabwe.

Kwanini Mugabe hakosi usingizi mbele ya akina Chiwenga?

General Chiwenga na makomredi wenzake hawawezi kamwe kumdhuru Robert Mugabe na kisha kuandamwa na laana ya kihistoria.

Si wengi wenye kufahamu, na wengine wanahitaji kukumbushwa, kuwa ukweli ni kuwa Robert Mugabe zamani kidogo alishawaambia makomredi wenzake ndani ya ZANU PF na kwenye Jeshi la Zimbabwe akiwemo Army General Chiwenga, kuwa angependa kuondoka.

Nyuma ya pazia, iko kwenye rekodi, kuwa ni jeshi la Zimbabwe ndilo limemng'ang'aniza Mugabe asiondoke madarakani. Ilikuwa ni mwisho wa mwezi Machi mwaka 2008. Ni baada ya kujulikana matokeo ya uchaguzi kuwa Morgan Tsvangirai kura zake zilitosha kuingia Ikulu.

Kwenye mkutano wake wa siri na majenerali inasemwa Robert Mugabe aliwaambia makomredi wenzake kuwa yuko tayari kuachia ngazi. Ndipo pale Mkuu wa Majeshi, General Chiwenga akamwamuru Mugabe asiyakubali matokeo. Akaambiwa atulie Ikulu na mengine awaachie jeshi.

Jambo hili linaandikwa na mwandishi mahiri kutoka Sweden, Bw. Stig Holmqvist kwenye kitabu chake. (Pa Vag Till Presidenten, ukurasa wa 300). Kimeandikwa kwa lugha ya Kiswidi ikiwa na maana ya ' Njiani Kwenda Kwa Rais'. Nina bahati ya kukutana na mwandishi huyo ambaye pia amepata kukutana na Robert Mugabe.

Hakuna shaka kuwa Jeshi ndilo limekuwa likimcontrol Mugabe kwa muda mrefu sasa. Yawezekana kabisa, hesabu za makomredi akina Chiwenga na wenzake, watu wa aina ya Emerson Munangagwa zimevurugwa na alichokionyesha Grace kuwa amedhamiria kweli kuchukua madaraka na hata kuwa na nguvu za kumshawishi Robert Mugabe kumwondoa kwenye Umakamu wa Rais Munangagwa.

Katika mazingira hayo, haishangazi kuwa Robert Mugabe hana wasiwasi wowote na anaweza kusinzia, kulala na hata kukoroma mbele ya waliomwambia kuwa abaki tu madarakani wakati alitaka kuondoka.

Haishangazi kuwa Robert Mugabe jana alipowaambia kuwa kuna graduation alialikwa kwenda kama mgeni rasmi, akina Chiwenga wakahakikisha anakwenda.

Tusishangae, wakati taratibu za makomredi kukamilisha hesabu za Mugabe kukabidhi madaraka hazijakamilika, Mugabe anaweza pia kutokea hata kwenye sherehe ya harusi.

Kwa sasa si Mugabe anayeongoza Zimbabwe. Ni Jeshi.

Maggid Mjengwa.

0688 37 36 52
Zimbabwe watu wake wameenda shule na wanajua vizuri historia ya nchi yao. Wanajua kabisa kuwa adui mkubwa ni mzungu na siyo wao kwa wao. siyo kama hapa akina TL wanapewa vipesa vya madafu alafu wanawasaliti watanzania, huku fans wao wakishangilia kama mazuzu
 
Hawa nadhani hawakujenga bifu za ajabu kama kwenu huku. Wanajua a 93-year-old man hakuwa akitenda yale kwa akiri yake. Hii move ni kumzuia Grace na criminals wenzake
Kweli kabisa mkuu. Kati ya waarifu waliomzunguka mualifu namba moja ni huyo demu. na kwa umri wa mzee ina maana demu ana jamaa zake wanaomgonga kimtingo.....
 
Zimbabwe Nyuma Ya Pazia:

Kwanini General Chiwenga Anacheka Na Mfungwa Wake?

Ndugu zangu,

Picha hiyo imeishangaza dunia. Kwamba Rais aliyepinduliwa na kuwekwa kwenye kizuizi cha nyumbani ' House Arrest', anatembelewa na kiongozi wa mapinduzi. Wanakaa kuongea, kunywa chai pamoja na kucheka.

Lakini, waliojitahidi kuifuatilia Zimbabwe kabla na baada ya uhuru watakubaliana nami, kuwa hilo si la ajabu kabisa.

Army General Constatine Chiwenga na Robert Mugabe ni marafiki. Ni makomredi waliofahamiana tangu zama za Chimurenga- Mapambano ya msituni kupigania uhuru wa Zimbabwe.

Kwanini Mugabe hakosi usingizi mbele ya akina Chiwenga?

General Chiwenga na makomredi wenzake hawawezi kamwe kumdhuru Robert Mugabe na kisha kuandamwa na laana ya kihistoria.

Si wengi wenye kufahamu, na wengine wanahitaji kukumbushwa, kuwa ukweli ni kuwa Robert Mugabe zamani kidogo alishawaambia makomredi wenzake ndani ya ZANU PF na kwenye Jeshi la Zimbabwe akiwemo Army General Chiwenga, kuwa angependa kuondoka.

Nyuma ya pazia, iko kwenye rekodi, kuwa ni jeshi la Zimbabwe ndilo limemng'ang'aniza Mugabe asiondoke madarakani. Ilikuwa ni mwisho wa mwezi Machi mwaka 2008. Ni baada ya kujulikana matokeo ya uchaguzi kuwa Morgan Tsvangirai kura zake zilitosha kuingia Ikulu.

Kwenye mkutano wake wa siri na majenerali inasemwa Robert Mugabe aliwaambia makomredi wenzake kuwa yuko tayari kuachia ngazi. Ndipo pale Mkuu wa Majeshi, General Chiwenga akamwamuru Mugabe asiyakubali matokeo. Akaambiwa atulie Ikulu na mengine awaachie jeshi.

Jambo hili linaandikwa na mwandishi mahiri kutoka Sweden, Bw. Stig Holmqvist kwenye kitabu chake. (Pa Vag Till Presidenten, ukurasa wa 300). Kimeandikwa kwa lugha ya Kiswidi ikiwa na maana ya ' Njiani Kwenda Kwa Rais'. Nina bahati ya kukutana na mwandishi huyo ambaye pia amepata kukutana na Robert Mugabe.

Hakuna shaka kuwa Jeshi ndilo limekuwa likimcontrol Mugabe kwa muda mrefu sasa. Yawezekana kabisa, hesabu za makomredi akina Chiwenga na wenzake, watu wa aina ya Emerson Munangagwa zimevurugwa na alichokionyesha Grace kuwa amedhamiria kweli kuchukua madaraka na hata kuwa na nguvu za kumshawishi Robert Mugabe kumwondoa kwenye Umakamu wa Rais Munangagwa.

Katika mazingira hayo, haishangazi kuwa Robert Mugabe hana wasiwasi wowote na anaweza kusinzia, kulala na hata kukoroma mbele ya waliomwambia kuwa abaki tu madarakani wakati alitaka kuondoka.

Haishangazi kuwa Robert Mugabe jana alipowaambia kuwa kuna graduation alialikwa kwenda kama mgeni rasmi, akina Chiwenga wakahakikisha anakwenda.

Tusishangae, wakati taratibu za makomredi kukamilisha hesabu za Mugabe kukabidhi madaraka hazijakamilika, Mugabe anaweza pia kutokea hata kwenye sherehe ya harusi.

Kwa sasa si Mugabe anayeongoza Zimbabwe. Ni Jeshi.

Maggid Mjengwa.

0688 37 36 52
Je Influence za ukabila haziwezi pia kuwa sababu maana hawa wote sio Washona ambao tangu Uhuru wamekuwa wakiendesha nchi kwa siasa za hiana dhidi ya jamii ya Wamatebele?
 
Ndebele tribe waliuwawa sana wakati huo na ukabila umekithiri sana
Huyu alipokuwa National security minister alishiriki mauwaji ya kabila la ndebele
 
IMG_20171118_190426.jpg

Lazima hapo ujue kuna jambo muhimu la kimaamuzi lifanyike haraka sana kama kiongozi wa nchi ili amani iendelee kutawala.

Hatua kama hizi wanaume wa kazi wakishaamua hazinaga lelemama kabisa.
 
Back
Top Bottom