Kwanini General Chiwenga Anacheka Na Mfungwa Wake?

M

maggid

Verified Member
Joined
Dec 3, 2006
Messages
1,084
Likes
398
Points
180
M

maggid

Verified Member
Joined Dec 3, 2006
1,084 398 180
Zimbabwe Nyuma Ya Pazia:

Kwanini General Chiwenga Anacheka Na Mfungwa Wake?

Ndugu zangu,

Picha hiyo imeishangaza dunia. Kwamba Rais aliyepinduliwa na kuwekwa kwenye kizuizi cha nyumbani ' House Arrest', anatembelewa na kiongozi wa mapinduzi. Wanakaa kuongea, kunywa chai pamoja na kucheka.

Lakini, waliojitahidi kuifuatilia Zimbabwe kabla na baada ya uhuru watakubaliana nami, kuwa hilo si la ajabu kabisa.

Army General Constatine Chiwenga na Robert Mugabe ni marafiki. Ni makomredi waliofahamiana tangu zama za Chimurenga- Mapambano ya msituni kupigania uhuru wa Zimbabwe.

Kwanini Mugabe hakosi usingizi mbele ya akina Chiwenga?

General Chiwenga na makomredi wenzake hawawezi kamwe kumdhuru Robert Mugabe na kisha kuandamwa na laana ya kihistoria.

Si wengi wenye kufahamu, na wengine wanahitaji kukumbushwa, kuwa ukweli ni kuwa Robert Mugabe zamani kidogo alishawaambia makomredi wenzake ndani ya ZANU PF na kwenye Jeshi la Zimbabwe akiwemo Army General Chiwenga, kuwa angependa kuondoka.

Nyuma ya pazia, iko kwenye rekodi, kuwa ni jeshi la Zimbabwe ndilo limemng'ang'aniza Mugabe asiondoke madarakani. Ilikuwa ni mwisho wa mwezi Machi mwaka 2008. Ni baada ya kujulikana matokeo ya uchaguzi kuwa Morgan Tsvangirai kura zake zilitosha kuingia Ikulu.

Kwenye mkutano wake wa siri na majenerali inasemwa Robert Mugabe aliwaambia makomredi wenzake kuwa yuko tayari kuachia ngazi. Ndipo pale Mkuu wa Majeshi, General Chiwenga akamwamuru Mugabe asiyakubali matokeo. Akaambiwa atulie Ikulu na mengine awaachie jeshi.

Jambo hili linaandikwa na mwandishi mahiri kutoka Sweden, Bw. Stig Holmqvist kwenye kitabu chake. (Pa Vag Till Presidenten, ukurasa wa 300). Kimeandikwa kwa lugha ya Kiswidi ikiwa na maana ya ' Njiani Kwenda Kwa Rais'. Nina bahati ya kukutana na mwandishi huyo ambaye pia amepata kukutana na Robert Mugabe.

Hakuna shaka kuwa Jeshi ndilo limekuwa likimcontrol Mugabe kwa muda mrefu sasa. Yawezekana kabisa, hesabu za makomredi akina Chiwenga na wenzake, watu wa aina ya Emerson Munangagwa zimevurugwa na alichokionyesha Grace kuwa amedhamiria kweli kuchukua madaraka na hata kuwa na nguvu za kumshawishi Robert Mugabe kumwondoa kwenye Umakamu wa Rais Munangagwa.

Katika mazingira hayo, haishangazi kuwa Robert Mugabe hana wasiwasi wowote na anaweza kusinzia, kulala na hata kukoroma mbele ya waliomwambia kuwa abaki tu madarakani wakati alitaka kuondoka.

Haishangazi kuwa Robert Mugabe jana alipowaambia kuwa kuna graduation alialikwa kwenda kama mgeni rasmi, akina Chiwenga wakahakikisha anakwenda.

Tusishangae, wakati taratibu za makomredi kukamilisha hesabu za Mugabe kukabidhi madaraka hazijakamilika, Mugabe anaweza pia kutokea hata kwenye sherehe ya harusi.

Kwa sasa si Mugabe anayeongoza Zimbabwe. Ni Jeshi.

Maggid Mjengwa.

0688 37 36 52
 
Attachments:

  • File size
    49.2 KB
    Views
    57
L

lolo123

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2017
Messages
455
Likes
445
Points
80
Age
25
L

lolo123

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2017
455 445 80
Ukimpa mnofu mbwa, kamwe hawezi kukubwekea
 
Pancras Suday

Pancras Suday

Verified Member
Joined
Jun 24, 2011
Messages
7,609
Likes
1,650
Points
280
Pancras Suday

Pancras Suday

Verified Member
Joined Jun 24, 2011
7,609 1,650 280
Inaonesha kumbe tangu zamani jeshi limeshika nchi chini ya kivuli cha Mugabe ndo maana hata yeye Mugabe huwa hana wasiwasi na mtu yeyote
 
Slowly

Slowly

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Messages
1,266
Likes
1,695
Points
280
Slowly

Slowly

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2016
1,266 1,695 280
Shida ni kuwa jeshi halitaki nchi kuongozwa na mwanamke...hiyo ni mwiko kwa africa...hata wamarekani hilo hawawezi kulikubali....jeshi linajaribu kumweka sawa mzee..asidhubutu kumwachia huyo manzi na badala yake atafte mtu mwingine
 
Abunwasi

Abunwasi

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2009
Messages
3,764
Likes
1,522
Points
280
Abunwasi

Abunwasi

JF-Expert Member
Joined Jun 25, 2009
3,764 1,522 280
Zimbabwe Nyuma Ya Pazia:

Kwanini General Chiwenga Anacheka Na Mfungwa Wake?

Ndugu zangu,

Picha hiyo imeishangaza dunia. Kwamba Rais aliyepinduliwa na kuwekwa kwenye kizuizi cha nyumbani ' House Arrest', anatembelewa na kiongozi wa mapinduzi. Wanakaa kuongea, kunywa chai pamoja na kucheka.

Lakini, waliojitahidi kuifuatilia Zimbabwe kabla na baada ya uhuru watakubaliana nami, kuwa hilo si la ajabu kabisa.

Army General Constatine Chiwenga na Robert Mugabe ni marafiki. Ni makomredi waliofahamiana tangu zama za Chimurenga- Mapambano ya msituni kupigania uhuru wa Zimbabwe.

Kwanini Mugabe hakosi usingizi mbele ya akina Chiwenga?

General Chiwenga na makomredi wenzake hawawezi kamwe kumdhuru Robert Mugabe na kisha kuandamwa na laana ya kihistoria.

Si wengi wenye kufahamu, na wengine wanahitaji kukumbushwa, kuwa ukweli ni kuwa Robert Mugabe zamani kidogo alishawaambia makomredi wenzake ndani ya ZANU PF na kwenye Jeshi la Zimbabwe akiwemo Army General Chiwenga, kuwa angependa kuondoka.

Nyuma ya pazia, iko kwenye rekodi, kuwa ni jeshi la Zimbabwe ndilo limemng'ang'aniza Mugabe asiondoke madarakani. Ilikuwa ni mwisho wa mwezi Machi mwaka 2008. Ni baada ya kujulikana matokeo ya uchaguzi kuwa Morgan Tsvangirai kura zake zilitosha kuingia Ikulu.

Kwenye mkutano wake wa siri na majenerali inasemwa Robert Mugabe aliwaambia makomredi wenzake kuwa yuko tayari kuachia ngazi. Ndipo pale Mkuu wa Majeshi, General Chiwenga akamwamuru Mugabe asiyakubali matokeo. Akaambiwa atulie Ikulu na mengine awaachie jeshi.

Jambo hili linaandikwa na mwandishi mahiri kutoka Sweden, Bw. Stig Holmqvist kwenye kitabu chake. (Pa Vag Till Presidenten, ukurasa wa 300). Kimeandikwa kwa lugha ya Kiswidi ikiwa na maana ya ' Njiani Kwenda Kwa Rais'. Nina bahati ya kukutana na mwandishi huyo ambaye pia amepata kukutana na Robert Mugabe.

Hakuna shaka kuwa Jeshi ndilo limekuwa likimcontrol Mugabe kwa muda mrefu sasa. Yawezekana kabisa, hesabu za makomredi akina Chiwenga na wenzake, watu wa aina ya Emerson Munangagwa zimevurugwa na alichokionyesha Grace kuwa amedhamiria kweli kuchukua madaraka na hata kuwa na nguvu za kumshawishi Robert Mugabe kumwondoa kwenye Umakamu wa Rais Munangagwa.

Katika mazingira hayo, haishangazi kuwa Robert Mugabe hana wasiwasi wowote na anaweza kusinzia, kulala na hata kukoroma mbele ya waliomwambia kuwa abaki tu madarakani wakati alitaka kuondoka.

Haishangazi kuwa Robert Mugabe jana alipowaambia kuwa kuna graduation alialikwa kwenda kama mgeni rasmi, akina Chiwenga wakahakikisha anakwenda.

Tusishangae, wakati taratibu za makomredi kukamilisha hesabu za Mugabe kukabidhi madaraka hazijakamilika, Mugabe anaweza pia kutokea hata kwenye sherehe ya harusi.

Kwa sasa si Mugabe anayeongoza Zimbabwe. Ni Jeshi.

Maggid Mjengwa.

0688 37 36 52
Mtafute Gentamycin humu mjengoni atakupatia analysis ambayo itakidhi kiu yako kuhusu hili
 
Z

Zola7

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2015
Messages
476
Likes
238
Points
60
Z

Zola7

JF-Expert Member
Joined Jun 23, 2015
476 238 60
Lengo la jeshi la Zimbabwe ni kuifanya jumuiya za kimataifa sizipige kelele kwa mapinduzi walofanya na kinachoendelea sasa ni kumlazimisha mugabe atangaze kujiuzulu kwa hiari ili kulinda heshima yake na akiendelea kukataa nguvu zitatumika. Viongizi wengi wa ZANU-PF wamemkataa Mugabe kitambo sana ila hawakuwa wazi ili kulinda maslahi yao , pia wameitisha mkutano ili kutoa kauli ya pamoja juu ya Mugabe
 
black sniper

black sniper

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2013
Messages
9,511
Likes
6,566
Points
280
black sniper

black sniper

JF-Expert Member
Joined Dec 10, 2013
9,511 6,566 280
Kwenye graduation hiyo na Mke wa aliepundua nchi Gen Chiwenga alikuwa anachukua degree yake pia
 
DhulRah

DhulRah

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2016
Messages
253
Likes
211
Points
60
Age
30
DhulRah

DhulRah

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2016
253 211 60
Hawa nadhani hawakujenga bifu za ajabu kama kwenu huku. Wanajua a 93-year-old man hakuwa akitenda yale kwa akiri yake. Hii move ni kumzuia Grace na criminals wenzake
Hii move nakubaliana kabisa ni ya kumzuia Grace na wala si kumuondoa Mugabe
 
S

saimile

Member
Joined
Aug 11, 2017
Messages
25
Likes
14
Points
5
S

saimile

Member
Joined Aug 11, 2017
25 14 5
Shida ni kuwa jeshi halitaki nchi kuongozwa na mwanamke...hiyo ni mwiko kwa africa...hata wamarekani hilo hawawezi kulikubali....jeshi linajaribu kumweka sawa mzee..asidhubutu kumwachia huyo manzi na badala yake atafte mtu mwingine
Hivi kule Liberia G.Weah alishinda?
 
ArD67

ArD67

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2016
Messages
2,805
Likes
1,949
Points
280
Age
36
ArD67

ArD67

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2016
2,805 1,949 280
Haya mambo bwana, bado hayako wazi.
 
Njilembera

Njilembera

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2008
Messages
1,447
Likes
181
Points
160
Njilembera

Njilembera

JF-Expert Member
Joined May 10, 2008
1,447 181 160
Shida ni kuwa jeshi halitaki nchi kuongozwa na mwanamke...hiyo ni mwiko kwa africa...hata wamarekani hilo hawawezi kulikubali....jeshi linajaribu kumweka sawa mzee..asidhubutu kumwachia huyo manzi na badala yake atafte mtu mwingine
Kweli? Kule Liberia- au yule ni mwanaume? Makamu wa Rais Tanzania je? Vipi Joyce Banda Malawi au yule Rose wa Gabon(hata alitawala muda mfupi tu) au kule Central Afric Republic (jina limenitoka)? Africa haina ubaguzi wa kijinsia kama unavyofikiri. Hata kabla ya wakoloni tulikuwa na kina mama viongozi. Ulaya ndio wabaguzi- Mwanamume na Mwanamke waliosoma kuanzia chekechekea mpaka shahada watalipwa tofauti- kisa jinsia yao. Waajiri wengi tu bado wako hivyo. Tafiti bwana!
 
K

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Messages
4,334
Likes
2,394
Points
280
K

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2012
4,334 2,394 280
Shida ni kuwa jeshi halitaki nchi kuongozwa na mwanamke...hiyo ni mwiko kwa africa...hata wamarekani hilo hawawezi kulikubali....jeshi linajaribu kumweka sawa mzee..asidhubutu kumwachia huyo manzi na badala yake atafte mtu mwingine
Ni kosa kubwa sana kuongozwa na mwanamke katika nafasi kama ya urais!Ni hatari mno kwa usalama wa Taifa.Mwanamke aliumbwa kwa ajili ya mwanaume tu na si vinginevyo
 
Ndahani

Ndahani

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2008
Messages
14,741
Likes
2,025
Points
280
Ndahani

Ndahani

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2008
14,741 2,025 280
Shida ni kuwa jeshi halitaki nchi kuongozwa na mwanamke...hiyo ni mwiko kwa africa...hata wamarekani hilo hawawezi kulikubali....jeshi linajaribu kumweka sawa mzee..asidhubutu kumwachia huyo manzi na badala yake atafte mtu mwingine
Yule mama haifai Zimbabwe. Bora akae pembeni
 
tamuuuuu

tamuuuuu

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2014
Messages
11,097
Likes
8,082
Points
280
tamuuuuu

tamuuuuu

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2014
11,097 8,082 280
Watanzania daini katiba mpya ccm itoke vinginevyo mtapata tabu sana
 
Forum statistics

Threads 1,237,989
Members 475,809
Posts 29,308,999