Kwanini dada zetu mpo hivi

MAJANI YA KUNDE

JF-Expert Member
Aug 25, 2008
213
37
Najiuliza sipati jibu hebu jamani nisaidieni Kwanini Mwanaume anampenda Mwanamke anamchagua wafunge pingu za maisha bila ya kulazimishwa na mtu wanaishi kwa upendo na amani mwisho wa siku wife anakwenda kwa Waganga wa kienyeji kutafuta dawa ili amtawale mmewe why?inauma na kukela sana.kwanini?
 
Si amtawale, ila anamsaidi kumuepusha na mabalaa. maana hawa ni kama watoto hawakui wala hawaelewi wana dare kufanya vitu hatarishi so ni kumprotect huyu baba zaidi ,maana hawa wa baba mbili haikai tatu haikai na ucpoangalia anakuletea balaa la gonjwa au unabwagwa pwaa na mitoto yako huku akienda lea watoto wa hawala!
 
Hahahhahaha.....anataka kukaba mpaka penalty???
Nadhani hilo ni tatizo la kisaikolojia zaidi!!Kwanza inaweza kusababishwa na
....kutokujiamini!!Anaona kama vile unaweza kumtoka wakati wowote.Yani mtu anakua hajithamini kiasi cha kujiona anastahili kua na wewe mpaka aongeze kukutuliza.Ni sawa na kukufumba macho...ndivyo wanavyoamini.
....Possessiveness!Hapa unakuta mtu ana ile hali ya kutaka kukumiliki jumla...bila kuacha mwanya wowote wa wewe kupumua bila idhini yake!!
Yani anakua anataka kua incontroll of your emotions kuhakikisha kwamba utabaki kua wake tu hata kama ni kwa kukupumbaza!!!
 
Unakuta mwanamke hajiamini ndio maana anaweza kufanya hivyo na jingine ni vile kupata ushauri kwa shoga/marafiki nawe bila kufikiri unaamua kutenda
 
Hahaha! InatokeA kwa sababu ambazo wengine wameshaeleza hapo. Inanikumbusha kisa nilichowahi kusikia. mwanamke kaenda kwa mganga kumdhibiti mume wake "asitoke nje". Kwa utata wa kauli hii mume akawa anajifungia ndani hatoki nje, kama zezeta, kazi akawacha. Yale maisha ya raha waliyozowea yakaishia kuwa historia tu. Kwa mwanamke huyu kilchofuata ni majuto tu.
 
jana nilikuwa nasikiliza wapo redio usiku, mchungaji Dedora akihuburi alisema "mwanamke anaweza kuwa chombo cha hatari hata kuondoa maisha yako" nikakumbuka wale wanaitwa wapelestina!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom