Kwa mda mrefu sasa wabunge wa chadema wamekuwa wakiendesha harakati za kupinga mwenge wa uhuru,
Najiuliza chadema wanachukia mwenge wa uhuru au wanachukia shughuri zinazofanywa na mbio za mwenge,
Pengine wanadhani mwenge usipopita wao watazidi kuungwa mkono kwenye maeneo mengi,
Lakini imani yangu ni kuwa chadema wanapingana na maendeleo yanayozinduliwa na kufunguliwa wakati wa mbio za mwenge kwani wao ni wapinga maendeleo ili serikali ionekane haijafanya kitu,hizi siyo siasa bali ni kupotoka kwani siyo busara kupinga kila kitu.
Kwanini CCM wanaupenda Mwenge wa Uhuru? Fikiri kwanza kuhusu faida na hasara yake
Wewe ulishaona wapi watu wanapinga kila kitu hata cha manufaa kama siyo kupoteza utashi wa kimaendeleo ni nini?,
tafuta hotuba yoyote ya kiongozi wa chadema hutasikia akihamasiaha au kupongeza maendeleo fulani.
Maneno mengi lakini ya maana ni mawili tu,Naheshimu mawazo ya kila mtu.
Ila ndugu yangu nashindwa kuamini kama mtu mwenye akili timamu na mpenda maendeleo anaweza akaunga mkono 'mbio za mwenge'. Yaani unashindwa kufikiri kwamba hiyo miradi inayozinduliwa na mwenge ingekuwepo hata bila mwenge!?
Mwenge haukuleta hiyo miradi, bali ukifika mahali flani wanatafuta kitu cha kuzindua. Ndio maana wamefikia hatua ya kuzindua hata 'Guest houses' za watu binafsi. Nimeshuhudia 'guest house' iliyozinduliwa na kiongozi wa mbio za mwenge.
Nadhani tatizo lako ni CHADEMA na wala sio mwenge
weka wewe data za garama za mwenge na faida zakeMkuu we hewa kweli ambacho sijui nini hapo nilijua utatoa data unazojua lakini umetokwa povu tu.
Kwa mda mrefu sasa wabunge wa chadema wamekuwa wakiendesha harakati za kupinga mwenge wa uhuru,
Najiuliza chadema wanachukia mwenge wa uhuru au wanachukia shughuri zinazofanywa na mbio za mwenge,
Pengine wanadhani mwenge usipopita wao watazidi kuungwa mkono kwenye maeneo mengi,
Lakini imani yangu ni kuwa chadema wanapingana na maendeleo yanayozinduliwa na kufunguliwa wakati wa mbio za mwenge kwani wao ni wapinga maendeleo ili serikali ionekane haijafanya kitu,hizi siyo siasa bali ni kupotoka kwani siyo busara kupinga kila kitu.
sure Mkuu, viongozi wa CHADEMA ni hodari sana wa kuropokaManeno mengi lakini ya maana ni mawili tu,
kunahaja ya chadema kuacha kuropoka kwa kupinga kila kitu badala yake ijikite kuendeleza jamii zaidi kuliko kupinga.
hili liko wazi chadema ni wapinga maendeleo hatushangai kupinga maendeleo yanayofanywa na serikali.
Wewe naona umekurupuka. Kwani umeambiwa mwenge unapeleka fedha za miradi? Mbio za mwenge hutumika kuzindua miradi iliyotekelezwa kupitia vyanzo mbalimbali vya mapatoTukiacha U-CHADEMA labda tupe mfano wa mradi ulowahi kutekelezwa kwa pesa za MWENGE. Usipende kutoa majibu ya jumla na matusi toa hoja kuthibitisha mchango wa mwenge katika maendeleo na jibu hoja kuhusu matumizi ya hovyo ili kuukimbiza mwenge