Barubaru
JF-Expert Member
- Apr 6, 2009
- 7,161
- 2,329
Wa Ukumbi.
Kwanza kabisa napenda kutoa Pole zangu kwa Familia ya Mwangsi kwa kumpoteza mpendwa wao wakti akitekeleza majukumu ya kazi yake.
Pili natoa pole kwa wanahabari wote wa Tanzania hususan Upande wa Bara kwa kumpoteza mwanachama wenu mahiri katika mazingira ya kusikitisha akiwa akitekeleza wajibu wake kisharia wa kupasha habari.
lakin pia WaTanzania wote kwa kumpoteza mwananchi mwenzenu makini sana .
Baada ya salam hizo za Pole napenda pia kutoa mshangao wangu kwa baadhi ya vyama vya Siasa huko Tanzania kwa kulivalia njuga suala ma kifo hichi na kuvisahau vifo vingine. Hapa nimeshangazwa sana na Chama Cha Chadema ambachi kimekuwa mstari wa mbele sana kulishadidia hili.
Ikumbukwe kuwa wenye haki kamili ya kulishadidia hili ni waandishi wa Habari ambao ndio sio tu kwa kupewa pole lakin wanajitetea na kudai haki zao za msingi pindi wanapokuwa katika utendaji wa shughuli zao. Ikimbukwe kuwa Wanahabari kwa nchi zinazofuata Rules of Law wao wanakuwa ni muhimili mkuu wa nne lakin usio rasmi katika uongozi wa nchi. Mihimili iliyo rasmi kwa mujibu wa Rules of Law ni mahakama, Bunge na Serikali.
Mimi nilitaraji chama cha Chadema walitakiwa kujua kuwa Mwangosi aliuawa katika tukio hilo akiwa kazini kama Mwandishi wa habari na si kama mshabiki au mwanachama wa Chadema. Chadema walitakiwa wayashadidie mauaji ya wanachama wao ambao wamekuja kushiriki katika tukio la kichama kama yale ya Arusha au hata yaliyotokea hivi karibuni huko Morogoro. Lakin hili si muswiba wao ni muswiba wa wanahabari japo tukio lilitokea katika hadhwara yao.
Kwa lugha ya Pwani tunasema Chadema wanasafiria Nyota ya Mwangoso katika kujitafutia umaarufu wa kisiasa. Kwani hata katika baraza kuu lao Jana walishikiria kifo hicho na kuonyesha mpaka video yake lakin hawakuonyesha video ya mauaji ya Mwanachama wao Morogoro. Hivyo kuzidisha thamani kwa Mwangosi ambaye ni mwanahabari na kumsahau mwanachama wao wa Pale morogoro. Sote tunaamini watu wote ni sawa lakin familia ni sawa zaidi. Na kila muswiba una wenyewe wengine wote mnakuwa wasindikizaji. Ni vizuri Chadema wajue kuwa katika Muswiba wa Mwangosi wao ni wasindikizaji tu lakin muswiba ni wa wanahabari.
Kijumla ninalaani mauaji ya watu hususan haya ya mwandishi akiwa anatekeleza majukumu yake lakin napinga sana watu kutumia muswiba huu kwa kujitafutia umaarufu na kusahau mauaji ya wanafamilia wake. Tukumbuke kila muswiba una wenyewe. Muswiba wa Mwangoso ni wa wanahari wote sio tu Tanzania bali Dunia nzima na wengine wote tunakuwa wasindikizaji tu.
Tussafirie nyota za wengine katika kutafuta umaarufu wa kisiasa.