Kwanini CHADEMA inasimama na Lwakatare, maamuzi ya Kamati Kuu

Makamanda msijali kwani hata Martin Luther King Jr aliteswa sana lakini alichokianzisha ndo sasa waafrika wamarekani wanafurahia matunda ya damu yake.
 
Mtoi tuliza kichwa ndugu yangu: point ya kwanza ilishaelezwa muda mrefu kwamba mmeweka mawakili tena wasomi! Ilitosha kuwaamini hao. Mnavyofanya ni kama ile theory ya uchumi ya diminishing returns! Unaweka matrekta 10 kwenye heka moja unategemea kutakuwa na ufanisi kwenye uzalishaji? Nimeconnect dots!

Hujajibu hata kipengele kimoja alichokuuliza Mohamed
 
Mnapenda siasa za mtaroni wanaCCM! Hivi ni wakati gani mnatumia muda wenu tunaoulipia kodi zetu kufikiri mambo ya kuondoa majanga mengi yanayoikabili nchi, naona 80% ya muda mnautumia kuifikiria chadema tu!

Logically ni sawa wakiifikiria CDM 24/7. Hebu imagine CDM wachukue nchi hayo madudu yote watayaficha wapi, kwa sasa ni kuhakikisha chama chochote chenye support ya watu ambacho kinaelekea kuwang'oa watapambana nacho usiku na mchana.

Hawa jamaa ni mabingwa na kubambikiza kesi ila hizi za sasa watawafukuza majaji wote cos hawawezi kudhalilisha taaluma yao kwa kuwabeba criminals.
 
Naona hata historia ya CHADEMA huijui.

Kwa kifupi ni kwamba CHADEMA ilipata umaarufu kwenye uchaguzi wa 2010 tu. Kabla ya hapo CHADEMA haijawahi kuwa na nguvu.

Prove me wrong!
You are very wrong!
ukimuuliza maalim seif au mzee wa ADC Hamad Rashid watakuambia chadema imejijenga kuanzia Bungeni na kuimaria sana kwa kumtumia dr slaa na ishu ya Epa, list of shame, kutimuliwa bungeni kwa Zitto,.akina halima mdee. Said Arfi, nk .,
na ndiyo maana hata mpambano wa chaguzi za tangu 2007 zilikiondoa Cuf na kubaki kuwa za vyama viwili Ccm vs Chadema, ref Tarime, Busanda na Biharamulo kwa hiyo hata uchaguzi wa 2010 ilikuwa rahisi kutabiri mwelekeo..
acha kutumia akili za akina nanii kuleta hoja ndugu yangu..
 
Kamanda mkakati wa kuidhoofisha CDM ni mkubwa sana, bora makamanda mmeligundua mapema. Sikiliza kisa hiki cha kweli kimetokea hivi karibuni hapa Mtwara. Viongozi wa SHURA YA MAIMAM MKOA wa Mtwara wameitwa mmoja mmoja na kuhojiwa juu ya sakata la gesia asilia kusafirishwa kwa njia ya bomba kwenda Dar. Mmoja wa viongozi wa shura alielezwa kuwa anatuhuma 2, moja anatuhumiwa kupita katika makundi ya vijana kuchochea vijana wapinge kusafirishwa kwa gesi asilia kwa njia ya bomba kwenda Dar na tuhuma ya pili kuwa anapitaka katika misikiti mbalimbali kuchochea waumini wapinge kusafirishwa gesi asilia kwa bomba kwenda Dar. Aliulizwa kama yupo tayari kutoa maelezo kuhusu tuhuma zinazomkabili. Ustadhi kabla ya kujibu alimlani shaitwani na kusoma dua ( kuruhwalahu) baada ya dua alisema yupo tayari kutoa maelezo. Mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo. Askari- Je unakijua chombo kinachoitwa baraza la vijana la wilaya? Ustadhi; Sikijui. Askari - Je unamjua mwenyekiti wa wilaya wa CHADEMA? Ustadhi: Simjui. Askari - Je tukimleta mtu hapa akathibitisha kuwa unamjua utasemaje? Ustadhi: Simjui. Askari - Wewe ndiyo mwenyekiti wa CHADEMA wa wilaya. Ustadhi - mimi? Askari - ndiyo, wewe ulikwenda Pride redio ambako umehojiwa na tunayo CD ya mahojiano yako. Ustadhi: Sauti unayoisikia hapa sasa inafanana na sauti uliyoisikia kwenye CD? Askali - ndiyo tena kwa asilimia mia moja. Ustadhi: Kama intelijensia yenyewe ya polisi ni hii, basi ni failia. Askali - unasemaje? Ustadhi: Kama intelijensia yenyewe ya polisi ni hii basi ni felia. Askari - Kwa nini unasema hivyo? Ustadhi: Mimi sijawahi kwenda redio, kwa mara ya mwisho nilikwenda redio mwaka 2010 wakati wa kampeni ya uchaguzi kura za maoni ndani ya CCM nikiwa mgombea. Askali: Nilikuwa na uhakika kwa asiliamia mia moja kuwa wewe ndiyo mwenyekiti wa CDM wa wilaya na tuhuma zilizopo kwenye faili hili nilikuwa nikufungulie charge na kesho nikupeleke mahakamani.

Makamanda hebu angalia mahojiano haya. CDM inatafutwa hapa. Huyu jamaa angekuwa tu hata mwanachama wa CDM nadhani ingekula kwake.
 
Mwanzo nilisema humu kuwa Chadema haijajipanga!. Sasa nasema, Chadema as Chama, kinakabiliwa na ukosefu mkubwa kabisa wa busara za kawaida, hivyo kiukweli safari ya Chadema kuongoza nchi as of now!, ni bado sana. Japo baadae nikakubali kuwa Chadema imeanza kujipanga! lakini kwenye hili la Rwakatare, "Chadema bado haijajipanga kabisa!", kwa sababu nasisitiza the Video is "bonafide genuine!", hivyo kitendo cha Cha Chadema kumkumbatia Rwakatare, kina very serious consequences and Chadema will pay for this very dearly!.
Wish you all the best!, hope for the best!, but get prepared for the worst!.
Pasco.
Nimemuona P kwenye mada za CHADEMA. Utabiri wa mabaya. P ulituasa tuepuke prophecy of doom. Tusiwaase wengine huku sisi tunatenda.

Hakuna kosa kubwa tutalifanya kama kuombea CHADEMA ife. Hiyo laana haitakaa ituache, itakula nasi sahani moja. Kama tulikubali NCCR na CUF vinyongwe, tusikubali haya kwa CHADEMA.

Makala nyingi za kuiponda CHADEMA na kukiombea mabaya hata kama sio sehemu ya zile project zina ukakasi na kuacha maswali mengi kuliko majibu.

Je, kuna personal issues nje ya politik?

Jr
Mkuu Mshana Jr, kwanza heshima mbele, hakuna mtu yoyote anayeiombea Chadema ife, kosa langu ni kuwa mkweli too much.

Humu jf tuna members wa aina 3, tuna
  1. Simple minds, discuss people, wao badala ya kujadili hoja iliyo mezani, hawa watamjadili mtoa hoja.
  2. Ordinary minds, discuss events, hawa watadili matukio, nini kimetokea etc
  3. Great minds discuss ideas, hawa watajadili hoja iliyo mezani.
Hivyo naomba keep on being free, kujadili watu, matukio na hoja, katika mabandiko yangu, ukiweza kujibu hoja, nitashukuru, ila hata ukinijadili, sikulaumu na likes nakutwangia.
Ukipata muda karibu ujibu hoja za bandiko hili.

Asante
P
 
Hapa ndio utajua hile barua yao ilikuwa fake! Asante sana makene kwa ufafanuzi hao walinzi wafukuzwe ikithibitika! Hakika ccmweli kazi wanayo! Nasasa hivi wanampango wa kujiteka na kujipindua waseme chadema! Tuko pamoja lissu.
Huyu alipewa nini mpaka leo anaichukuia na kuisema vibaya CHADEMA. Aisee aliyetukumbusha huu uzi ubarikiwe sana.
 
Mkuu Mshana Jr, kwanza heshima mbele, hakuna mtu yoyote anayeiombea Chadema ife, kosa langu ni kuwa mkweli too much.

Humu jf tuna members wa aina 3, tuna
  1. Simple minds, discuss people, wao badala ya kujadili hoja iliyo mezani, hawa watamjadili mtoa hoja.
  2. Ordinary minds, discuss events, hawa watadili matukio, nini kimetokea etc
  3. Great minds discuss ideas, hawa watajadili hoja iliyo mezani.
Hivyo naomba keep on being free, kujadili watu, matukio na hoja, katika mabandiko yangu, ukiweza kujibu hoja, nitashukuru, ila hata ukinijadili, sikulaumu na likes nakutwangia.
Ukipata muda karibu ujibu hoja za bandiko hili.

Asante
P
Rwakatare usimkuze na kumuabudu, wa kumuabudu ni MUNGU PEKEE.
 
asante sana mkuu. matatizo yakizidi jua neema inakaribia. mia
"Matatizo yakizidi jua neema inakaribia" Nukuu bora kabisa kuwahi kukutana nayo JF.

Nai-dedicate kwa wale makamanda wote wazalendo wa kweli(Sio wachumia tumbo), hakika neema i karibu, msikate tamaa pamoja na mateso yote yanayofanywa na wadhalimu wanaotumia nguvu na mabavu, siku yaja itakuwa ni kilio na kusaga meno kwao!
 
Back
Top Bottom