Mpaka Kieleweke
JF-Expert Member
- Feb 27, 2007
- 4,132
- 1,582
wewe subiri uje sikia sehemu walipoandika sijui kabila gani ndio utajua ,harafu huoni anaweza kutoka bagamoyo,lindi lakini ni mchaga
wewe waja kweli ndugu yangu
Huoni wabunge wakuteuliwa wanatoka mikoa mingine lakini wachaga .Taratibu mkulu
Kati ya watendaji wote wa ngazi za juu niliowataja wa makao makuu hakuna hata mmoja zaidi ya hao 3 ambaye anauhusiano ama wa kuolewa ama wa kuoa huko uchaggani.
Mwenye hilo na aseme,tuache unafiki na uongo tutaigawa nchi hii bila sababu za maana .
Ndio maana nimemuuliza mkamap alete ushahidi tofauti au ataje hao ambao yeye anadhani ni wachaga zaidi ya hao watatu waliotajwa hapo. Unajua ccm imekosa cha kusema kuhusu upinzania na sasa watakuja na vitu vya ajabu ambavyo havipo.
Wakipewa data wanakimbia kama zemarcopolo sijui kaishia wapi.
Tatizo lenu wengi ndio hilo wanao watakia mema kwa kukifanya chama kua na sura ya kitaifa zaidi ya sura ya KILI mwaja juuuuuuu
Vitu vya wazi mwabishaaaa .
Mpelekeni mahakamai CHACHA WANGWE kwa kudhalilisha CHADEMA na mkoa wa Kilimanjoro akiwa na nia ya uchochezi kwa kudaganya ya kwamba
1.MAJORITY makoa makuu ni wachaga
2.Wabunge 5 kati ya sita wanatoka KILI
3.Ruzuku ya laki moja imeanza kupelekwa mikoani baada ya yeye kuingia madarakani.
Kwanini tuandikie mate na wino upo !!! Kama mnaona ananjama ya kukiangusha chama mpelekeni MaHAKAMANI kwa maneno yake Harafu mkishinda kesi mmwadhibu ama msimuadhibu naye ikionekana alichosema ni kweli naye afanye atakavyo.
Mambo haya ya kubishana na Radio yanatoka wapi??
Mtu anampango wa kuhujumu chama mnamwachisha uongozi tu na endelee na chama hii ni sawa na uhaini ktk chama.
Ama kweli ubishi ni ubishi tu, kila mara ukibanwa kutetea ulichoandika unakosa cha kusema. Ndio maana kwenye ile thread nyingine umejifanya kuwa unamwongelea ndugu yako anayeitwa Mbowe Mkama wakati ambapo unajua kabisa uliyekuwa unamwongelea.
Mkama, hii issue ya ukabila imekosa ushahidi na baada ya dozi ya mpaka kieleweke hapo juu, inaoneka ccm hamna msingi kwenye hili. Wewe tafuta kingine maana hili limekosa msingi.
Ushaidi gani unataka wewe ndg yangu
Nimekwambia hivi mpeleke CHACHA mahakamani ama mwiteni mbele ya vyombo vya habari akane aliyoyasema ya kwamba.
1.majority makao makuu hawatoki KILI
2.wabunge 5 kati ya 6 hawatoki KILI
3.Hizo laki moja mikoani zimeanza baada ya yeye kuingia madarakani.
Mda wote mimi hoja zangu zipo hapo sijahama WANGWE mnaye hapo Mbowe mnaye hapo nenda basi hata kwenye vyombo vya habari WANGWE akakane hayo na muwaonyeshe waadishi wa habari makaratasi yote mbona ni rahisi sana. KUSPIN hakusaidii.
Nendeni na list nzima kutokea mfagizi hadi juu mkanushe hilo na wangwe akili.
mje la wabunge nalo mseme hawatoki kili mkanushe wangwe akili,harafu mje la ruzuku muonyeshe mmeanza lini mkanushe wangwe akili .Na mwisho mwambieni wangwe ayakane maneno yake.
Kuhujumu CHAMA ni swala zito msingeliachia hapohapo kumushusha jamaa tu cheo.
naona bado unaendeleza ubishi bila kurudi kwenye majina na makabila uliyopewa na mpaka kieleweke na wewe ukaanza kubisha kuwa huu kuna wachaga zaidi ya watatu waliotajwa pale.
Wewe acha kupotosha watu mimi nimeomba DOC za kiofisi zaidi na nikasema kuandika mtu unaweza andika utakayo.
Ya watu 5 kutoka KILI ni ya wabunge wa kuteuliwa ,wewe waja kweli na SPIN zako na ubishi wa kupika
na nikaongeza kuna uwezekano wa mtu kutoka Lindi lakini ni MSUKUMA kama ilivyo kwa wabunge wa kuteuliwa CHADEMA wanatoka mikoa tofauti lakini ni WACHAGA.
Nimekuambia hicho kibano unajosema ni UBISHI tu unaoondekeza kama MBOWE aende na CHACHA akakanushe na si hapa wewe na mpaka kieleweke kukanusha hapa na kutulazimisha tuamini mnavyosema.
Pia sio kunipa kibano mimi bali muwafahamishe wapiga kura wenu kwa uwazi na ukweli Mchukue CHACHA na MBOWE akakanushe kwenye vyombo vya habari kwa kuwataja majina kazi zao mahali na makabila yao kama alivyofanya hapa .Mbona mnakwepa hilo???
Hapo tutaamini na kua ule uzushi wa CHACHA na ukome.
pia wabunge wale watano kati ya 6 pia wakanushe tuone uzushi wa CHACHA anayetaka kuhujumu chama.
Pia akane kuhusu hizo ruzuku kua hazikuanza wakati wa uongozi wake
Hizo ndizo hatua mhimu za kufutilia mbali majungu na matope kinyume cha hapo ni SPIN tu.
Moderator!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! NAomba muongozo wa JF
Je nihalali kuniita mimi kutaja ID yangu kwamba ni CCM Na marufuku kutaja ID ya jina????
kama unajua kuwa kuna uwezekano wa kuwa haya unayosema hapo ya kuchanganya mikoa na ukabila, inakuwaje unasisitiza kuwa unajua wabunge 5 kati ya sita wa chadema walikotoka?
Umejuaje?
unauliza swali ambalo linakufunga mwenyewe, wewe umesema kuwa kuna wanachadema hapa, je kuna kosa gani la wewe kuwa miongoni mwa wana ccm?
Haya ndiyo mnajifunza huko ccm?
Mgaya na wewe nitakutaja jina lako !!!!!!! mimi nachukua Paketi za maseji yako nasoma IP adress ya comp unayotumia harafu natuma wajamaa wangu wanakuja kukopi mafili yote yako nakutaja jina ohhhhhhh.Nakutania tu mkulu wangu hicho nikikorobwezo tu.
Mzee tuhitimishe huu mjadala.
Kuelekea ukombozi ni lazima wachache ama wengi wawe tayari kuumizwa kwa faida ya wengi.
Hii ni vita ya kuelekea ukombozi ,na ijulikane kuwa wafanayabiashara na wenye pesa hawakichangii CHADEMA kwani wanaogopa CCM.
vitu vingine tuwe tayari kusema ukweli mbona hata hapa JF inaendeshwa kwa kuchangiwa na wanachama wake wenye uwezo wa kuchangia?
Mbona hapa hamlalamiki kuwa waache kuchangia?
Nani anamlipa Invisible na JF Crew yote hapa ?mbona wao wanajitolea na kufanya bure?
Ama kujitolea CHADEMA ndio dhambi na kosa?
Kwa maelezo ya Dr. Slaa CHADEMA ni sawa na kusema haina mfadhili hivyo inabidi miongoni mwa majukumu ya uongozi yawe ni kugharimia uendeshaji wa chama.
Kufananisha CHADEMA na TANU ni spin aliyoitumia DR. Slaa kama katibu wa chama ili kukitetea.Ukweli ni kwamba pesa za kuendesha TANU zilikuwa zinatolewa na watu ambao hawakuwa na mamlaka ya kikatiba ya kufanya maamuzi ya chama.Nyerere alikuwa na kamshahara ka ualimu ambako hakawezi kununua hata typewritter ya chama, lakini yeye ndio alikuwa mwamuzi mkuu wa chama unlike CHADEMA ambayo wale wanaotoa fungu ndio wanaotoa maamuzi.Hii sio sahihi.
CHADEMA bado ni NGO.
Yale yale, ya chama kina wenyewe na wenyewe ni sisi tuliojitolea tu-vijisenti; kazi kweli kweli
Nadhani hapa kuna hoja nzuri. Tusitake vyama vingine vifuate utaratibu wa CCM wa kujiendesha kwa kulipana mishahara. Siasa lazima iwe utumishi, na utumishi uwe wa watu kujiolea, siyo kuchuma. Kabla ya Mbowe na Dk. Slaa kuwa viongozi kwa nyadhifa walizonazo leo, utendaji wa wakati ule, chini ya Dk. Aman Kabourou, ulikuwa unalipana mishahara, na chama hakikukua mikoani.
Mbowe alipopiga vita hii tabia ya viongozi kula ruzuku kwa kujilipa mishahara, ilikuwa sababu ya kwanza ya Dk. Kabourou kutafuta mlango wa kutokea hasa baada ya Mbowe kuwa mwenyekiti. Sababu hizi hiiz za ulaji ndizo zilimuondoa Paul Kyara aliyekuwa mweka hazina na aliyeshirikiana kwa karibu na Dk. kabourou kutumbua ruzuku.
Sasa, kwa vyama visivyo na ruzuku kubwa, visivyoungwa na wafanyabiashara wengi (maana waliopo wanachangia CCM), kuna kosa gani kwa kina Mbowe na Ndesamburo kukichangia chama chao? Kuwataka wasichange pesa nyingi wakati wanazo ni mbinu nyingine ya kutaka kukidhoofisha chama hicho. Tuwatendee haki katika hili....Chadema hakina wahindi wa kukichangia, lakini hata CCM yenye Wahindi bado inategemea pesa za EPA! Shame!