Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 65
Dr.
Unaongea siasa nyiiiiiiiiingi, lakini sikushangai kwa sababu hiyo ndio kazi uliyopewa na CHADEMA na umeilia kiapo.
Nyinyi CHADEMA kila kukicha mnakandia kila jambo linalofanywa na CCM badala ya kuangalia nini cha kujifunza kama unavyosema mwenyewe hapa.
CCM wameanza utaratibu wa kufungua matawi nje ya nchi, msaidizi wako Zitto Kabwe ameita hatua hiyo kuwa ni upuuzi.Hivi nyinyi mnaoingia bungeni kushiriki katika maamuzi ya taifa zima mnashindwa kutathmini kiasi gani CHADEMA inaweza kuchangiwa na wanachama wa nje ya nchi iwapo mtafungua matawi??? Ukifungua tawi Kigoma la wanachama 50 na lingine Houston la wanachama 50 unadhani kiuchumi mchango wa wanachama hawa ni sawa???
Ukweli ambao hutaki kuukubali ni kwamba Mbowe hapotezi chochote kwa kutoa pesa kwa CHADEMA na hiyo ndio inampa kiburi cha kuchagua nani wa kufanya naye kazi.Ndio maana anakodisha helkopta kumbe pesa ya kadi za wanachama hamna!
Nakupa siri moja, kwa watanzani walio nje ya nchi upinzani in general ni more popular than the ruling CCM.Iwapo mtaendelea na ushamba wa kukandia kila kinachofanywea na CCM mtaendelea kuitwa upinzani mpaka wewe utastaafu.
Gembe,
unazungumzia CHADEMA kukosa wafadhili, hivi "mfadhili" ni nani? Kwa maelezo ya Dr Slaa, viongozi wa juu wa CHADEMA wameamua kufadhili chama, sasa mfadhili gani mwingine wamekosa? au kwako wewe mfadhili mpaka awe yule mwenye asili ya "uarabu" au mwenye mkopo wa EPA?
Suala la kukosa wabunifu, Dr Slaa amezungumzia kuwa CHADEMA wamefanikiwa kuanzisha miradi sio ya kinadharia bali miradi kweli.
Swali langu kuhusu ubunifu: je kuna mradi gani ulioanzishwa na CCM (baada ya mfumo wa vyama vingi) ili tuwaone wao ni wabunifu na watu makini? Na ili tuutolee mfano kwa vyama vingine. Na nikauliza vipi SUKITA?
Kwa ufupi nakubaliana na wewe kuwa CCM na serikali yake kwa ujumla sio wabunifu, na niwepesi kutafuta pesa kwa njia za mkatisho (shortcut)!
Wakati ccm inakwiba pesa za nchi na kuunda kamati zisizoisha na kukataa kutolea maelezo chochote wanachofanya kwa visingizio vya usalama wa taifa
Dr.
Unaongea siasa nyiiiiiiiiingi, lakini sikushangai kwa sababu hiyo ndio kazi uliyopewa na CHADEMA na umeilia kiapo.
Nyinyi CHADEMA kila kukicha mnakandia kila jambo linalofanywa na CCM badala ya kuangalia nini cha kujifunza kama unavyosema mwenyewe hapa.
Ushaanza kashfa kama kawaida yako..... grrrrrr
Kujifunza toka kwa ccm walioiba na kufilisi nchi?
Kufungua matawi ya vyama nje ya nchi sio suluhisho la matatizo ya vyama Tanzania. Watanzania walioko nje wanaweza kuchangia bila hata kuwa na wanachama kwenye matawi hayo. Kwa taarifa yako watanzania wengi hapa US ambako hakuna udaku na upuuzi wa matawi ya ccm wanachangia vyama vya siasa Tanzania kuliko huko india na UK kwenye usanii wa matawi ya vyama na ulaji.
Wewe umeyajua vipi haya, nani asiyepoteza pesa akizitumia... what a damn excuse! nilidhani mjadala hapa ni wa nia ya kuendeleza kumbe wewe ni unazi tu unaleta.
Dr Slaa, lugha chafu kama hizi ni kawaida kwa huyu zemarcopolo kwa hiyo zichukulie jinsi zilivyo.
i) Acha uvivu wa kusoma, yaani hizo sentensi chache za Dr ndio umeona ni "nyingiiiiiii"? Hili ni tatizo mojawapo kubwa sana kwa wana CCM: uvivu wa kusoma maandishi, mbaya na aibu sana!
ii) Unataka chadema wawasifie CCM, hao walioajiriwa kwa ajili ya kusifia CCM wafanye kazi gani? Hicho cha kujifunza kutoka CCM ni kipi-rushwa, wizi na uporaji wa mali za umma??!
Pesa zinazochangwa Marekani zingekuwa zinatosha basi Mbowe and the gang wasingelazimika kujitolea.
Naona leo umekuja na mpya, nimeshakuwa mnazi duh!!!
Jamani tunaomba Dr.Slaa abadili hiyo line ya VODA maana huo ni mtandao wa kifisadi ili twende pamoja kupigana vita dhidi ya mafisadi.
Nani anayetaka CHADEMA wawasifie CCM?
Kukataa kujifunza kutoka kwa CCM ni mojawapo ya sababu inayovifanya vyama vya upinzani viendelee kuwa upinzani kwa miongo kadhaa.
Bado unaendelea kusema kuwa watu wajifunze toka ccm? wajifunze buzwagi, iptl, kiwira, kagoda, meremeta, dowans, wizi BoT au wajifunze nini zaidi?
Sasa imeshajulikana hapa kuwa ccm walitumia pesa za wizi BoT kufanyia kampeni 2005. Mafanikio ya ccm yako tainted na kwa jinsi mambo ya Mkapa na wenzake yanavyowekwa wazi, hakuna chochote chema cha kutoka CCM
zitto alisema kuwa CHADEMA ilienda Ghana kujifunza toka kwa chama cha Kufuor na Kenya kujifunza toka kwa ODM. Iwapo CHADEMA wanaona kuna cha kujifunza kutoka kwa Odinga na hakuna cha kujifunza kutoka kwa Kikwete, basi waendelee na attitude hiyo na watavuna walichopanda.
ODM haijawahi kushinda uchaguzi Tanzania, chama kinachoshinda uchaguzi Tanzania ni CCM.Siasa za Ghana na Kenya ni za Ghana na Kenya, siasa za Tanzania ni za Tanzania.
Mhe Slaa,
Nimependezwa na majibu ya hoja zilizotolewa na wachangiaji hapa JF. Nashukuru kwa kuja kutuweka sawa; nina swali la nyongeza ambalo naomba kwa faida yangu na wanabodi wengine ulipatie ufafanuzi.
Ref Jibu la 4. Huu utaratibu mliojiwekea Chadema wa kubadilisha muda wa Mwanachedema kuwa mchango wake kifedha.
Je utaratibu huo unaangalia Cheo/Majukumu ya wanachama wanaojitolea au muda unabadilishwa kuwa fedha kwa kiwango sawa? Mfano: Mhe Mbowe (Mwenyekiti) ametumia masaa 10 kwa shunguli za chama, masaa haya 10 kila saa ni Shs 10; mtayahesabu Shs 100 (10 x 10 = 100) kutoka kwa Mbowe kwenda Chadema kama mchango wake. Wakakti huo huo, J.J Mnyika amejitolea masaa 10 naye pia kwa shughuli za chama...yeye naye itahesabika kuwa amechangia Shs 100 kwa Chadema au kiwango cha kuzidisha kinatofautiana kwa nafasi aliyonayo mtu kwenye chama???
Natumai nimeeleweka, ni hayo tu.
Nashukuru.

lakini pia Zitto hakusema kuwa Chadema haitaki kujifunza toka kwa ccm. Haya ni maneno yako mwenyewe. Kama una hiyo quote unaweza kuiweka hapa.
Kwa jinsi ccm "inavyoshinda" Tanzania kwa kutumia wizi BoT, sidhani kama ni ushauri mzuri kwa Chadema kujifunza namna ccm inavyoshinda Tanzania. CCM inashinda kwa kutumia pesa za wizi so hii kwa maoni yangu ni out of picture.
Swali zuri sana,
kwa kuongezea tu, labda Dr. Slaa atuambie hizo "equipments" zinazokosekana kuhakikisha kuwa wanaojitolea mikoani, wilayani na vijijini nao wanapata haki zao ni equipments gani?