Kwanini CCM Zanzibar haipati wahamiaji kutoka upinzani? Je, haipendwi au wanasiasa wa visiwani wamekomaa kuliko wa bara?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,932
141,897
Naomba anayejua sababu ya kutowasikia wanasiasa wa upinzani kule Zanzibar wakihamia chama tawala anijuze tafadhali.

Au sisi Watanganyika tunajua kucheza na kete za kisiasa kuliko Wazanzibari?

Majibu tafadhali.

Maendeleo hayana vyama!
 
ZANZIBAR Siasa ni ITIKADI siyo TUMBO MBELE.

Ndio maana MAALIM SEIF aliipigania CUF 2015 wakati LIPUMBA amepewa mapesa na CCM anazurula RWANDA bila kushiriki uchaguzi.

Lakini leo kamwachia mabilioni hayo ya RUZUKU ya CUF, LIPUMBA ANATAFUNA tu na kwenda kuanza upya kwenye chama kichanga kabisa chenye ruzuku MILIONI 4.

SEIF Ni Gwiji La Mwanasiasa Ndio Maana Hata Wazanzibar WANAMWAMINI.
 
Zanzibar wanachukulia Siasa serious na zaid ya Uadui

Kuna yule Jamaa alikataa kumfuata Seif Sharif ACT akabaki CUF jamaa wamemtenga hadi akifika Maskan Muuza kahawa anagoma kumuuzia Kahawa, so kuwa watu hawataki kuunga Mkono Juhudi za Dr Shein bali wanaogopa watatebgwa, wakifiwa hawatopata WaombolezJi, Sokoni hawauziwi, kwny Daladala wanazuiwa, yaan kuna Siasa za Kishamba sana Visiwan

Siasa chukulia kama Mpira tu ili usipate stress

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo ili Zanzibar kusiwe na siasa za Kishamba walipaswa kuunga Mkono juhudi ama?
 
Naomba anayejua sababu ya kutowasikia wanasiasa wa upinzani kule Zanzibar wakihamia chama tawala anijuze tafadhali.

Au sisi Watanganyika tunajua kucheza na kete za kisiasa kuliko Wazanzibari?

Majibu tafadhali.

Maendeleo hayana vyama!
Swali zuri lakini huwezi kuvumilia majibu sahihi.
Baki na ushabiki wako mkidanganyana eti wananuliwa
 
Kule upinzani ni upinzani kweli wana msimamo sio kama huku bara bahasha ya kaki na shati la kijani fasta mtu anaita waandishi wa habari
Naomba anayejua sababu ya kutowasikia wanasiasa wa upinzani kule Zanzibar wakihamia chama tawala anijuze tafadhali.

Au sisi Watanganyika tunajua kucheza na kete za kisiasa kuliko Wazanzibari?

Majibu tafadhali.

Maendeleo hayana vyama!
 
Naomba anayejua sababu ya kutowasikia wanasiasa wa upinzani kule Zanzibar wakihamia chama tawala anijuze tafadhali.

Au sisi Watanganyika tunajua kucheza na kete za kisiasa kuliko Wazanzibari?

Majibu tafadhali.

Maendeleo hayana vyama!

Ccm bara Magufuli anaweza kuchota hela hazina na kuhonga wapinzani, huko Zanzibar Shein hawezi hizo siasa za kishamba.
 
Back
Top Bottom