Kwanini CCM Iko Matatani?

Ni kwasababu baadhi ya watanzania wamekuwa na uroho wa madaraka na wanatumia njama za hata kuihujumu serikali arimradi watinge ikulu.watu hawa hawako vyama vya kupinga tu hata ccm na ndani ya serikali wapo.wanatumia kila hila hata kuhatarisha maisha ya kila siku ya watanzania lakini watz tunaofikiri kwa mmbongo zetu tumekataa kuwachagua kwa zaidi ya 60% of votes.
 
Ile kauli ya Dr. Mwakyembe kwamba WATANZANIA SIO ....................................... On the face of that statement, its just one simple statement. Ila ni kauli ya mtu kuandikia paper na ikawa published na akawa promoted (if it involves that).........

Tutake tusitake information is power. Igunga na sehemu zingine kote Tanzania mwamko na vugu vugu la kisiasa etc sio lelemama..... That power lipo Tanzania nzima, haya mengine sasa ya ufahamu, uelewa, hiki kikoje yanafuatia............
 
ccm haipo matatani kwani ilikuwa hivyo zamani ila sasa CCM IPO MATEKENI..................kila mwenye uwezo wa kubatua anabatua atakavyo
 
CCM as an organization has grown too big and therefore hard to manage. The stakes and interests are to many and quite diverse. Unlike Nyerere's time, ccm for the last decades has been promoting the wrong values (corruption, majungu, fornication and outright stealing from the state ). As such, these are not values which would promote a sustainable organization, instead, ccm is wrotening from within which is soon going to lead to an ultimate death.
 
Well said mkuu! hakika u made my day kwa huu uchambuzi wako....yaani kama mi-ccm itapita kwenye post hii basi BP itawashika.
Na hapo kwenye bold na blue, si Mwanakijiji tu hata wewe kwa huu uchambuzi uliyotumwagia hapa'wewe pia ni mzigo mzito kwa ccm. Big up!
 
Umesomeka kakaa..na hayo tu hoja ya kuwa wananchi wa sasa sio wa zamani haina mashiko..hata CCM ya sasa haipo ka zzaamani hivyo hilo sio tatizo...!naongezea wanaojiuma kuonesha maendeleo ambayo ndio vitu vya kuongelea kwa wananchi wanafanyiwa zengwe.
 
Ni kutokana na kuingiza kundi la wafanyabiashara kama wadhamini wakuu wa chama, mfanya biashara anaweza kuwa mwansiasa, lakini ni lazima kuwepo na misingi na kanuni zinazozuia kutumia utajiari wake kuinfluence power katika chama. Kwa sasa hivi makundi ndiyo jibu sahihi, lipo kundi la wanyonge ambalo linajiona limesahaulika kwa viongozi, lakini haliko radhi kuwaachia matajiri wachache wabaki na chama, hivyo wanakomaa nao humo humo, lipo kundi la matajiri ambalo linatumia ukwasi wao kuweka viongozi wa juu katika chama, na pia wanatarajia fadhira kutoka kwa hao viongozi. Hii inazaa upendeleo, kitu ambacho kinaleta minyukano ndani ya chama.
 
CCM ife tu hata leo na haina cha maana zaidi inatufanya watanzania kuwa maskini na kupoteza umoja wetu
 

CCM: Kutoka TAA mpaka kibatari.
 
Kwa wale tulioiona TANU, then ikaja CCM, watakubaliana nami kwamba huko nyuma mfumo wa utawala uliweza kuwadanya vizuri tu Watanzania kwamba ndio wamiliki wa nchi yao na hatima yao na watoto wao. Nadhani hii haikutokana na sera chama tu, bali haiba ya viongozi. Naamini hivyo kwa sababu mtu pekee alieyeweza kubuni mfumo na kuwapa wenzake wameze na kusimamia utekelezaji wa sera na maamuzi mbalil mbali (tena wakati mwingine watendaji hawakuelewa waliyotumwa) ni Nyerere. Ndiyo maana baada ya mzee huyo kustaafu kila kitu kikasambaratika.

Nadhani CMM hawawezi kulikwepa gharika. Hawakujenga mifumo ya utawala (governance institutions) na kwa sasa hawana tena muda wa kufanya hivyo.

Suala la kutafakari ni maandalizi ya maisha ya Watanzania bila CCM....Hata wakibebwa vipi...mbeleko zitachanika!
 
Wananch wanapoteza iman na ccm c kwa 7b inatenda mabaya la hasha ukichunguza kwa kna utagundua chadema kuna uozo zaid hata ya ccm..kwa kuwa watu hawakchunguz vzur na wanatekwa na propaganda na ahad zao zczo za kikwel pia cdm viongoz wake n opportunist..hvyo wamewapata watu weng sana wacopenda kujiulza haya n ya kwel au? Mf.dr slaa kudai wapunguziwe mishahara(wabunge)..masuala ya posho..wananch wanashdwa kuelewa kuwa cdm co wakomboz..na mwshowe wamewapata MAZUZU!..
 
ccm has sold its soul for buying its favourates! how now can liberate its people? watu walikipenda chama sabbu hapo mwanzo
chama kilikuwa ktk harakat za kupigania uhuru
2:hapo mwanzo chama kilikuwa ni cha wakulima na wafanyakazi leo ni pango la wafanya biashara wakubwa
3:ccm haikubaliki ni kutokana na wakati that is time bar watu wamechoka kuwa na hichi chama kutokana na kushndwa kutatua kero za wakati
3:upumbavu ujinga vinakata kamba mtazamo2
 
Kwani CCM hii ndiyo iliyotokana na TANU au Mwl. Nyerere?
Kama ndivyo basi iko kazi...
 
 
CCM ilianza kupoteza mvuto kwa wananchi na wanachama wake kwenye miaka ya 80 wakati ilipoanza kukumbatia wafanyabiashara na kuwaacha wakulima na wafanyakazi ambao ndio walikuwa nguzo na msingi mkuu wa chama. Wafanyabiashara wakaanza kujiingiza polepole hadi kwenye uongozi mkuu kwa kisingizio cha ufadhili na kufanikiwa kuwageuza hata viongozi safi tuliokuwanao kuanza kupenda mali na anasa kitu ambacho kilikwa mwiko enzi za awamu ya kwanza hadi kupelea kuvunjwa kwa Azimio la Arusha.

Nguvu ya wafanyabiashara kwenye chama ndiyo inayokiyumbisha chama, leo CCM hakitegemei tena wananchi kupiga kura ili kishinde kinategemea nguvu ya pesa hakina imani hata kama ni wanachama wake lazima kiwanunue. Zamani asset kubwa ya chama ilikuwa wananchi hasa wa vijijini lakini leo asset kubwa ya chama ni wafanyabiashara, mwananchi/mwanakijiji amekuwa akitumiwa kama tool (jembe) kufanikisha mavuno (kura) baada ya mavuno anasahauliwa hadi msimu mwingine.

CCM ijue dunia inabadilika hata siasa zinabadilika kwa kung'ang'ania mifumo ileile ya enzi na viongozi walewale ni kukinyima chama nafasi ya kujitanua. Viongozi kama kina Msekwa,Sitta wapo kwenye chama tangu tukiwa chipukizi miaka ya 70 wakituahidi sisi ni viongozi wa kesho, kesho imefika lakini bado wao ni viongozi, vijana wakileta mawazo mapya wanakumbushwa ahadi ile ya zidumu fikira za m/kiti/viongozi. Mwisho wa siku unakuta vijana ambao wanataka kutoa mawazo yao wanajiona kama hawatakiwi (Nape) wana deflect wanaamua kutafuta sehemu nyingine (chama mbadala) kutolea mawazo yao.
 
 
Kwa sababu wanahongwa suti na waarabu,hivyo tunahofia kizazi kijacho kisijekuwa si riziki.
 
Ni kwa sababu haijui majibu ya maswali makuu waliyo nayo Watanzania wa leo. Kwa mfano, Tanzania ina rasilimali nyingi kuliko nchi zote katika Afrika mashariki, laikini kimaendeleo iko nyuma kwa mbali ya Kenya. Ndiyo maana Rais Kikwete alikuwa Paris Ufaransa akaulizwa kwanini nchi yako ni maskini pamoja na kuwa na rasilimali nyingi akajibu kuwa hata yeye hakujua sababu ya umasikini wa Tanzania.


Sio hilo tu hata akija mtaalamu mshauri ambaye amefanya vema katika nchi nyingine zikafanikiwa ikifika kwenye utekelezaji kila kitu kinaharibikia hapo kwa sababu ya mtazamo finyu wa kutanguliza ubinafsi badala ya kusaidia nchi ifanikiwa ili mafanikio hayo yasambae kwa wengi. Ndiyo maana kwenye MKURABITA pamoja na ushauri mzuri wa gwiji wa uchumi duniani Prof. De Sotto mpaka leo hakuna mafanikio yoyote ya maana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…