Kwanini CCM bado ipo madarakani?!

Zillion

JF-Expert Member
May 15, 2017
1,357
1,804
Watanzania lazima tujiulize hili swali

Ni kwanini C.C.M bado ipo madarakani mpaka leo?

C.CM kwa miaka 60 wameshindwa kusambaza maji ya kunywa na umeme wa uhakika kwa wananchi kwanini tunawalea?

Najiuliza zile pesa walizonunia ndege cash ndege ambazo zinaingiza hasara kila mwaka zisingetosha kutoa maji ziwa Victoria na kusambaza nchi nzima?

C.C.M na serikali yao licha ya tuhuma za upigaji na ufisadi uliokithiri lakini pia wameshindwa kutumia rasilimali kama madini na mbuga zetu kupata fedha za kutosha na wanawaza tozo kila kukicha.

C.C.M inadharau sana wananchi leo waziri wanasimama na kusema asiyekubaliana na ujinga wake ahamie Burundi, leo viongozi wanaturingishia V8 wakati wakulima hawana mbolea?

Bunge la C.C.M lipo kutafuna pesa za wananchi na hakuna kazi wanayofanya hivi tunakubalije mtu mmoja anayeenda kupiga makofi bungeni alipwe Milioni 27 kwa mwezi na mwalimu alipwe laki 4?
Halafu baada ya miaka mitano anapewa zaidi ya 200Milioni mafao ambayo hakuchangia popote
Halafu mwalimu baada ya kutumika miaka 30 hapati hata nusu ya mafao yambunge aliyopewa kwa miaka 5 tu halafu anarudi tena kugombea ubunge kwanini?

C.C.M wanachagua viongozi kwa kuangalia ukada sio uwezo ukitazama wakuu wa mikoa, wilaya, kurugenzi na kibaya zaidi mpaka balozi wanapeana kwa ukada sio uwezo hii inadumaza sana maendeleo ya nchi
Viongozi wengi wa kuteuliwa hawana uwezo wala nia ya kuwatumikia wananchi wako kwa maslahi ya chama.

C.C.M wamevuruga uchaguzi mchana kweupe na kuwafungia watu mitandao huu ujinga na dharau za ccm kwa wananchi vinaota mizizi ni lazima tuchukue hatua

Ndege imeanguka ufukweni viongozi wamefika wanaanza kijifunika na miavuli wasiloe kwa ma nyunyu wakati watanzania wenzao wanakufa
na hakuna hatua iliyochukuliwa
Hivi tuna Serikali kweli?
Serikali ambayo inawekeza kununua magari ya maji ya kuwasha na mabomu ya machozi lakini inashindwa kununua vifaa vya uokoaji hito ni serikali?

Ni wakati wa kuiwajibisha C .C.M

Ni wakati wa kuvuna walichopanda.
 
1668735033849.png
 
Vyama vya upinzani dhaifu ndio sababu ya CCM kuendelea kutawala.. Tukiamua kuhamasishana kwa umoja wetu tukapige kura tunaiita CCM.. Lakini leo hii hata wapinzani hawajui wanataka nini..
 
Watanzania lazima tujiulize hili swali
Ni kwanini C.C.M bado ipo madarakani mpaka leo?
Mkuu Zillion , hili ni swali la msingi sana, na kwa bahati nzuri, baadhi yetu tuliisha jiuliza hili swali, na majibu tunayo!, kabla sijakupa majibu yangu na matokeo ya utafiti wangu, nina kaswali kadogo tuu kwako, swali lenyewe ni tukiipumzisha CCM, kuna nani wa kumpa?.
P
 
Mkuu Zillion , hili ni swali la msingi sana, na kwa bahati nzuri, baadhi yetu tuliisha jiuliza hili swali, na majibu tunayo!, kabla sijakupa majibu yangu na matokeo ya utafiti wangu, nina kaswali kadogo tuu kwako, swali lenyewe ni tukiipumzisha CCM, kuna nani wa kumpa?.
P
CHADEMA
wana uwezo na tukiwapa nafasi watafanya mambo makubwa tutaikwamua nchi hii kiuchumi, kisayansi, kiutamaduni na kifikra.
 
Back
Top Bottom