Kwanini Bongo movie imedorora??

255Gene

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
888
1,090
Wasalaam wanacelebrities na wanajf kwa ujumula... Kwanini Bongo movie imedorora na wengine wamefikia kusema imekufa ni sababu zipi zinazofanya hadi movie za kibongo kukosa soko
Je tatizo ni waingizaji?? ni directors amna ?ukosefu wa vifaa vyakisasa??? ni wandishi wa story na wa script wamekosekana?? wasambazaji amna??
Au labda zimekosa soko la
ndani???
Wadau na wapenzi wa Movie za kibongo mnakarubishwa kutoa hoja zenu
 
Zinakosa uhalisia.Mtu anaigiza yeye ni masikini lakini unamuona amevaa nguo za thamani na amejipamba vito vya thamani!Tukio ni la huzuni lakini muhusika unamuona hajaguswa na jambo hilo.Kila mdada mrembo anapewa nafasi ya kuigiza tena nafasi ya muhusika mkuu hata kama hana kipaji cha uigizaji!Kuna baadhi ya wasanii wako vizuri kama kina Muhogo mchungu,Jengua,Jangala,Onyango,bi Hindu nk.
Nawashauri wakubali kujifunza na kubadilika.Wawatumie watu wanaoweza kuandika hadithi nzuri kama akina Sultan Tamba.Nitarudi.
 
Siasa, tamaa, sembe , vipaji zero na mapenzi ndiyo vitu vinaua hiyo tasinia ya filamu.
Hizo, sababu nilizoweka hapo juu ukiyatathimini utaelewa Sana.

Mfano, nakumbuka nikiwa mdogo, home hawataki kabisa tuangalie huo ujuha Kwa sababu, kila muigizaji analialia na mwigizaji mwenzake katika issues za mpenzi kwenye kila filamu.

Nimeelewa baada ya kukua na kutambua matatizo yao.
 
Kweli mkuu

nasikia mkuu wa mkoa wa dar ameahidi kurudisha soko lao kwa kufungia uuzwaji wa movie za nje!!!
zimebaki siku ngapi sijui, wenyewe walikuwa wanahesabu huko insta!
 
Uhalisia ndio kitu kinachowagharimu..pia kurudiarudia Story pia inachangia..

Ndo maana mimi hawanipati siku hizi, nacheki zangu series/seasons za kikorea, kichina, india, US, thailand n.k
 
Wasalaam wanacelebrities na wanajf kwa ujumula... Kwanini Bongo movie imedorora na wengine wamefikia kusema imekufa ni sababu zipi zinazofanya hadi movie za kibongo kukosa soko
Je tatizo ni waingizaji?? ni directors amna ?ukosefu wa vifaa vyakisasa??? ni wandishi wa story na wa script wamekosekana?? wasambazaji amna??
Au labda zimekosa soko la
ndani???
Wadau na wapenzi wa Movie za kibongo mnakarubishwa kutoa hoja zenu

Tokea Waganga wao wengi wafariki hasa wa kule Bagamoyo ambako ndipo walikuwa wakijazana kila Weekend na wao wamekwisha sasa Kisanii.
 
Back
Top Bottom