Kwanini Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu (HESLB) inaendesha mambo kisiasa?

Jul 25, 2020
65
125
Haya ni Maoni Yangu, kwa mtazamo wangu naona Hili swala linaumiza sana watoto wa walala hoi kwanini Bodi ya mikopo Elimu Ya Juu inaendesha mambo yake kwa ahadi za kisiasa sana.

Kwenye briefing zao na taarifa ambazo huwa wanazisoma mbele ya media huwa zinajaa mbwembwe sana kuwa tuna hela Tayari mKononi kiasi kadhaa za kuwapangia wanafunzi mikopo.

Kwa maelezo Yao waliyoyatoa walidai wana hela tayari imetolewa ya kuwapa wanafunzi vyuo vikuu laki moja na elfu sitini (160000/) nachojiuliza ni kuwa mpaka vyuo vinaelekea kufungua hata nusu ya hao wanafunzi laki na sitini walioahidi kutoa haifiki kati ya waliowatangazia kuwapa mkopo hii imekaaje.

Katika walioahidi laki na sitini wametoa majina hata nusu yake hawafiki. Kwa maoni Yangu Naona imekaa kisiasa Sana.

Nini Maoni Yako Katika Hili?

Screenshot_20211022-162115_Chrome.jpg
 
Imeundwa na wanasiasa.
Inaumiza sana Vijana wengi mno wamekosa mkopo ila wanavoitisha media yaani wanajitapa wamepokea hela ziko tayari billion 500 zinasubiria wanafunzi au hela wanataka wagawane au ndio utasikia tumerejesha serikalini billion 200 zilizokosa wanafunzi SIASA Inaumiza sana watoto wa walalahoi
 
wale wanaoendelea waangaliwe.

Maana hakuna alopata hata mmoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
kabisa Yaani na kwanini waseme watawapangia watu laki na elfu sitini wakati wanajua hawana huo uwezo inakuwa ni siasa mpaka kwenye masomo ya watu maana mwaka wa masomo unaanza tarehe 25 ilitakiwa mpaka sasa hata kuvuka nusu ya laki na elfu 60 wawe washapangiwa mkopo badala yake ni hata nusu ya nusu ya laki na elfu 60 haijafika
 
Inaumiza sana Vijana wengi mno wamekosa mkopo ila wanavoitisha media yaani wanajitapa wamepokea hela ziko tayari billion 500 zinasubiria wanafunzi au hela wanataka wagawane au ndio utasikia tumerejesha serikalini billion 200 zilizokosa wanafunzi SIASA Inaumiza sana watoto wa walalahoi
SIASA zinaumiza watoto wa MATAJIRI kwakuwa wazazi wao wanalipa kodi lakini MASKINI ndio wananufaika.
 
Mbona unalia lia..wakati hizo hela niza freshers na continuous..ulizani niza first year tu..pia huo ni mkopo sio lazima kupewa wote.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom