Kwanini Bastola hazioneshi kuwasaidia wamiliki?

Kwanini Bastola hazioneshi kuwasaidia wamiliki?

Hizo million 7.5 unakuwa unatembea nazo au zipo kwenye akaunti? Kama ziko kwenye benki unalinda ATM card?


Unawapelekea bank statement. Lengo lao ni kuhakikisha una pesa ambazo unahitaji silaha kujilinda wewe na pesa zako, elewa statement yako itaonyesha kuingia na kutoka hivyo wataangalia utokaji wake kama unahitaji kuwa na silaha ya kujilinda; sio unatoa ki elf tano kwa mwezi unategemea kupata kibali cha kumiliki silaha.
 
Unawapelekea bank statement. Lengo lao ni kuhakikisha una pesa ambazo unahitaji silaha kujilinda wewe na pesa zako, elewa statement yako itaonyesha kuingia na kutoka hivyo wataangalia utokaji wake kama unahitaji kuwa na silaha ya kujilinda; sio unatoa ki elf tano kwa mwezi unategemea kupata kibali cha kumiliki silaha.

Hao unaowaonyesha benki statement ni Polisi au mkuu wa mkoa na kamati yake ya usalama? Maana kama ni polisi, nahisi tunahatarisha maisha zaidi
 
Taarifa kutoka jeshi la polisi hii leo juu ya hili suala

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA

Anuani ya Simu “MKUUPOLISI” Ofisi ya

Inspekta Jenerali wa Polisi,Simu : !""# "$$!%&' Makao Makuu ya Polisi,(a) *a+ !""# "$&- S+L+P+ .$'$,Unapo/i0u tafa12ali ta/a: 3A4 5S SALAAM
+
20 Novemba, 2013.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika siku za hivi karibuni, imebainika kuwa, baadhi ya watu waliomilikishwa silaha kihalali wamekuwa wakitumia silaha hizo kinyume na malengo mazuri ya umilikishwaji.



Baadhi yao wamekuwa wakitoa vitisho kwa wanan[FONT=MingLiU_HKSCS][/FONT]hi kwa kutumia silaha hizo bila sababu za msingi wawa!o katika maeneo mbalimbali, kama vile kwenye mabaa, kumbi za starehe na hata kuli!izana visasi, jambo ambalo ni kinyume [FONT=MingLiU_HKSCS][/FONT]ha sheria na malengo ya umilikishwaji.

Ku"uatia hali hiyo, #eshi la $olisi n[FONT=MingLiU_HKSCS][/FONT]hini linatoa onyo kali kwa wote wenye tabia hiyo kua[FONT=MingLiU_HKSCS][/FONT]ha mara moja na badala yake wanatakiwa kuzingatia sheria na masharti waliyo!ewa wakati wa umilikishwaji.



%idha, #eshi la $olisi linaanza o!eresheni kali ya kuwabaini wote wanao"anya vitendo hivyo, ikiwa ni !amoja na kuwanyang&anya silaha hizo wale watakaobainika kwenda kinyume [FONT=MingLiU_HKSCS][/FONT]ha sheria na matumizi ya silaha zao.



#eshi la $olisi linatoa wito kwa wanan[FONT=MingLiU_HKSCS][/FONT]hi wote wazalendo na wenye ma!enzi mema na n[FONT=MingLiU_HKSCS][/FONT]hi yetu, kutoa taari"a zitakazosaidia kuwabaini watu hao wanaojihusisha na vitendo hivyo ili waweze kukamatwa na ku"ikishwa kwenye vyombo vya sheria ku!itia namba ya simu 0754785557 au namba za simu za makamanda wa mikoa au kwenye kituo [FONT=MingLiU_HKSCS][/FONT]ho[FONT=MingLiU_HKSCS][/FONT]hote [FONT=MingLiU_HKSCS][/FONT]ha $olisi.

+metolewa na[FONT=MingLiU_HKSCS][/FONT]-%dvera [FONT=MingLiU_HKSCS][/FONT]enso - [FONT=MingLiU_HKSCS][/FONT]$/semaji wa #eshi la $olisi.
 
Nakumbuka jirani yangu hv majuzi kanyang'anywa pistol na majambazi geti la kuingilia kwake usiku. Tatizo hawa mabitoz ambao hawakupitia hata sungusungu hawana defensive skills hata chembe, wao wanacho fahamu ni kuwa na pistol tu basi. Mf.unakuta mtu anasilaha, inapotokea ambush ya ghafla au hata kusikia mlio wa risasi tayari yeye suruali chapachapa imesha lowa. Mathalan mtu unapokuwa outing na silaha hasa nyakati za usiku lazíma utafute angle ya kukaa kwa ajili ya usalama wa silaha yako na matumizi sahíhi in case of anything. Unalikuta jitu lina silaha alafu linachukua sehemu/meza ambayo siò strategic halafu linabugia pombe bila kipimo mpaka lina angusha gari. Japo kimsingi unapokuwa na silaha unatakíwa akili iwe kamilifu bila ulevi sawa na kuendesha gari. Pamoja na kukulinda, mmiliki pia unatakiwa kuipatia ulinzi wa hali ya juu tofauti na hapo unamiliki kifo/kifungo bila kujua. R.I.P uncle Dito.
 
Wengine hawana maadili na mafunzo ya kutumia
 
Mimi ilishanisaidia sana sema kwasababu sikuua mtu ndo maana hukuipata hii story, kuna siku walikuja Majambazi nyumani kwangu, nilishtuka wakati grill la chuma linakatwa nilipochungulia dirishani nikaona watu kama wanne wameshika mapanga na wengine nisiojua idadi walikuwa wapo mlangoni, nilichokifanya nikarusha risasi kama tatu dirishani wakasepa je haikunisaidia?

Baada yawananchi na polisi kuja ndo tukafungua mlango kumbe wale washenzi walishafungua kabisa hata Geti kubwa la fence ili iwawie rahisi wakati wa kuondoka usije ukadhani nilikuwa sina mlinzi, ishu ni kwamba Mlinzi kumbe alikuwa anasepa tunapoenda kulala na kwasababu alikuwa anaruhusiwa kuondoka saa11 alfajiri hatukuwahi kumstukia kwamba halali kazini
.

Ninaamini ile siku wangefanikiwa kuingia leo hii nisingekuwa nn-comment kwenye hii thread
seriously mkuu niwekee hadharani au nipm kajibastola kakutishia wezi kama yako au aina tofauti yaweza cost how much kwa bei ya kawaida. Am serious!
 
Sawa na hongera .
Lakini hoja hapa ni wanaosaidiwa na bastola kama wewe (kama ni kweli) ni wachache sana ukilinganisha na wale wanaokufa nazo! Na je unamiliki bastola kwa kujilinda tu na hao vibaka?

Utafiti umefanyika wapi na lini mpaka kufikia hili hitimisho? Silaha binafsi zinawasaidia wamiliki wake sana huo ndio ukweli usiotangazwa.
 
kwa kweli hata mimi nasikitika saaana haziwalengi walengwa
 
sisi tuendelee kutumia mishale tu hizi bastola hazitufai
 
Nadhani sababu ni kwamba tunatumia muda mwingi kuilinda silaha kuliko inavyotulinda.
Adui anakuvamia muda na wakati wowote,ila silaha haiwekwi mahali popote,na ukienda nayo kila mahali
unakuwa mtumwa wa silaha badala ya silaha kuwa mtumwa wako.
Kwa wenye roho nyepesi kuua au kujiua kwa bunduki ni rahisi maana muda wa kufikiri ni mdogo
ukilinganisha na anayejinyonga kwa kamba au kumeza dawa za sumu kwani muda wa maandalizi kidogo ni mwingi ukilinganisha na aliye na bastola mfukoni.
 
Hayo si mahitaji ya silaha! ujiko eti? utakufa nayo
Ni kweli mkuu Byabato,majambazi wakijua una silaha
hata kama huna fedha,wanakuja kuichukua wafanyie kazi
mi nadhani kwenye vigezo vya mtu kumiliki silaha yaongezwe na mafunzo
kama vile tunavyojaribiwa kabla ya kupata leseni ya gari.
Majambazi wanajua wamiliki wengi wa silaha wanamiliki ki-fashion na siyo kitaaluma
hivyo unakuta silaha hizo zinakuwa makaburi ya wamiliki badala ya kuwalinda.
 
bastola ni silaha kama panga, ngumi nk. tofauti ni efficiency. tatizo watu wanafikiri bastola hufanya kazi yenyewe, training, discpline na ujasiri nda mpango mzima.
 
seriously mkuu niwekee hadharani au nipm kajibastola kakutishia wezi kama yako au aina tofauti yaweza cost how much kwa bei ya kawaida. Am serious!

Mimi ka kwangu ni simpo sana nilichukua kwa Tshs840,000 mwaka 2007, ila nasikia sasa hivi vimepanda kuwa na uhakika nenda pale JKT ngome nasikia nao pia wanauza ila vinaanzia M1.8
 
Sawa na hongera .
Lakini hoja hapa ni wanaosaidiwa na bastola kama wewe (kama ni kweli) ni wachache sana ukilinganisha na wale wanaokufa nazo! Na je unamiliki bastola kwa kujilinda tu na hao vibaka?

Kaka kama una record nisaidie, what I know ni kwamba Bastola/Bunduki zinasaidia watu wengi sana kuliko hata zinavyofanikiwa kufanya uharifu, ishu ni kwamba ni mara chache sana habari kuvuma mtu akijiokoa kwa bastola, lakini mara nyingi habari zinazovuma ni pale majambazi yanapoua au kufanikiwa kupora kwa kutumia Bastola/Bunduki chukulia mifano ya kawaida mitaani, ni mara nyingi majambazi hukurupushwa kwasababu ya mlemgwa mwenye siraha anakuwa kayatimua kwa njia ya kupiga risasi juu lakini kesho yake huwezi ukasikia vyombo vya habari vimetangaza, ila ikitokea majambazi yakafanikiwa lazima utaisikia hii habari.
 
Tukio la matumizi mabaya ya bastola Bukoba.More updates to come!

blogger-image-1686157629.jpg


Ndg Hassan Munjari maarufu kwa jina la Hans(picahni) ameuawa kwa kupigwa risasi na mtu asiyejulikana,tukio hilo limetokea majira ya saa 4 usiku wa Jumamosi Dec 7,2013 maeneo ya BUKOBA CUP HOTEL (Zamani yaasila hotel) mjini bukoba.
​
Jeshi la Polisi bado linaendeleana uchunguzi wa kifo hicho. ​
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi amen!
credit.Bukoba wadau
​
 
Unahitajika mkakati madhubuti kutoka kwa mamlaka katika kudhibiti hii hali!

Byabato
 
Taarifa za jana na leo ni juu ya kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa mawanza clement mabina kuua na wananchi wenye hasira baada ya kutumia bastola.kwa mara nyingine bastola haikumsaidia!Nasisitiza hapa kwamba bastola bado hazonieshi kuwasaidia wamiliki! ama ataua au kuuawa!

1471895_713097872041940_440424421_n.jpg

Hapo juu ni mwili wa mabina baada ya kuawa jana na wananchi.
 
Back
Top Bottom