Ni hivi...Kama Fuvu la Mkwawa lilirudishwa Tanzania baada kuchukuliwa na wakoloni wa Kijerumani, mwili wa baba Mwalimu Nyerere alipofariki London Uingereza ulirudishwa na kuzikwa nchini.
Alifariki Mh Mgimwa (Mungu amrehemu) akitibiwa S.Africa, Mwili ulirudishwa kuzikwa nchini, Alifariki Mh Celina Kombani(Mungu amrehemu) nchini India, mwili ulirudishwa nchini kuzikwa. Mahujaji waliofariki kule Makka wakati hija walirudishwa kuzikwa nchini, Mh Abdallah Kigoda amefariki nchini India na taratibu za kuurudisha mwili nyumbani kwa ajili ya mazishi zinaendelea...
SWALI
Kwanini BALALI alizikwa Marekani badala ya kuzikwa nchini ilivyo kwa wengine?