Kwanini bajeti ya serikali isipangwe kutokana na uhitaji wa mkoa husika?

Kwanini bajeti ya serikali isipangwe kutokana na uhitaji wa mkoa husika?

Nyarupala

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2024
Posts
641
Reaction score
1,055
Habarini?
Ni matumaini yangu mnaendelea vizuri ikiwa ni pamoja na kufuatilia mpambano baina ya Iran na Israel ambapo tunayo mengi ya kujifunza kutokana na teknolojia za hali ya juu zinazotumika na nchi zote mbili katika mzozo huo.

Ni leo ikiwa siku ya tatu tangu bajeti ya serikali ya mwaka 2025/2026 ilipowasilishwa kwa wananchi kupitia bunge letu na kuonekana bajeti hii ikiwafurashia zaidi madereva bodaboda na bajaji kutokana tu na kushusha bei ya kukata leseni kwa madereva hao.

Katika bajeti hii,ikumbukwe pia nchi za Africa ya mashariki zilisoma bajeti zao ikiwemo nchi ya Kenya.

Kenya wao nmeona bajeti zao wanaziwasilisha kwa mgawanyo wa mikoa ambapo kwao mikoa hujulikana kama county,yaani kama Mombasa bajeti yao itakuwa kiasi kadhaa ambazo zitatumika kununua dawa za mahospitali,kujenga barabara na huduma nyingine za kijamii. Vivyo hivyo na kwa kila county .

Hi kitu nmeona tunaweza kuiga kwasababu inaweza kupunguza mzigo mkubwa kiuendeshaji. Kwa mfano kama wizara ya ujenzi unakuta waziri ni mmoja nchi nzima na pesa zoote ili zitoke lazima zianzie kwake kwa maana ya wizarani kwahyo mpaka pesa inafika ilipotakiwa kufika ili ifanye kazi ya ujenzi inakuwa imepitia kwenye account nyingi na hivyo kufanya udanganyifu mwingi pamoja na kuchepusha fedha kwenda kwenye account binafsi za baadhi ya watumishi wasio waaminifu.

Kwahyo,Mimi naona serikali ingeweka mfumo wa kila mkoa kuwa na uwe unapangiwa bajeti yake na pesa itakayotumika kwa mwaka mzima halafu pesa zoote zikipatikana zinapelekwa mahali pa kazi moja kwa moja na kazi ya waziri au wizara husika iwe ni ufuatiliaji wa namna pesa zinvyotumika tu.
 
Dar itapata hela nyingi zaidi mara 2 ya inavyopata sasa.

Sababu wote lazima mje huku
 
Back
Top Bottom