barafuyamoto
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 32,405
- 29,811
Asilimia 70 ya wanaosema hawali kiti moto hula pembeni...Inasemwa kuwa eti mfalme mmoja aliekuwa na wake wawili wazuri alialika wageni nyumbani kwake. Akaagiza wachinjwe wanyama wa kila aina kutoka katika mifugo yake - mbuzi, ng'ombe, ngamia, kuku, bata, kondoo, nguruwe, nakadhalika.
Baada ya mapishi kuwa yamekamilika wake wa yule mfalme waligundua kuwa miongoni mwa mapishi yale, nyama ya nguruwe ndiyo ilikuwa tamu kuliko zote kule jikoni.
Basi mke mmoja miongoni mwa wake wa mfalme yule aliamua kwa makusudi kuificha ile nyama tamu ili baadae wageni watakapokuwa wamekwisha kuondoka akampakulie mumewe ale. Na kwa akili ya yule mama alidhani kwa kumfanyia hayo mfalme yeye (huyu mama) atapendwa zaidi kuliko wake wenza.
Baada ya wageni kuwa wamekula na kushiba hatimae muda wa kuaga kuondoka kurejea makwao ukafika. Wakaenda zao.
Basi yule mke wa mfalme aliyekuwa ameficha ile nyama tamu akaipakua na kumtengea mfalme. Huku na kule mfalme akahoji kulikoni nyama ile iletwe hali wageni washaondoka? Mke akasema aliona ni vyema aifiche kwa ajili ya mfalme ili ampende zaidi.
Mfalme akasusa kuila akasema yeye aliandaa karamu kwa ajili ya kula na wageni wake na si kula peke yake kiuchoyo. Basi mfalme akatangaza mbele ya mkewe yule kuwa nyama ile haili na kwamba chakula kile (kitimoto) ni haram.
Kumbe wote tunakula kitimoto ila tu wengine wanakula kwa kificho na wikiendi ndo hii. Hapa Euro pale sahani ya kitimoto 😋
Ndio. Ukipata mtayarishaji mzuri inazidi kabisa. Upate rosti hapo au iliyokaangwa na mtaalam. Aaaah, alafu unakula ktk pub fulani hivi na ndizi kaangwa pembeni barmaids wazuri wanapitapita! Dunia nzuri sanaYaan kitimoto izidi kuku na samaki kwa utamu??
Sijawah onja kitimoto ila haiwezi fikiaNdio. Ukipata mtayarishaji mzuri inazidi kabisa. Upate rosti hapo au iliyokaangwa na mtaalam. Aaaah, alafu unakula ktk pub fulani hivi na ndizi kaangwa pembeni barmaids wazuri wanapitapita! Dunia nzuri sana
😂😂😂Wakwetu halo ndo hamuitendei haki bia,yani unywe bia mbili alafu maji Lita tatu.
Kiukweli hivyo vyakula vyote vinasubiri kwa kitimoto, labda kama hujawahi kuila hiyo kitu.. weka mbali na watoto hiyo nyama aisee+ kimea ndio kbsaaSijawah onja kitimoto ila haiwezi fikia
Kuku ,samaki,mayai,maziwa
🤣🤣🤣🤣 Mambo ya food and nutritionNi kwa sababu ni mtamu shinda mnyama yoyote. Jaribu kula pilau la nguruwe uone utamu wake.
Utamu wake ni mara 10,000 ya hivyo ulivyovitaja[emoji848]Yaan kitimoto izidi kuku na samaki kwa utamu??
Ngoja nimalize kazi za watu nikajilipue na huyu mdudu hapo Micasa[emoji39][emoji39]Kiukweli hivyo vyakula vyote vinasubiri kwa kitimoto, labda kama hujawahi kuila hiyo kitu.. weka mbali na watoto hiyo nyama aisee+ kimea ndio kbsaa
Ngoja nimalize kazi za watu nikajilipue na huyu mdudu hapo Micasa[emoji39][emoji39]
Mkuu acha kunitamanisha basi ukizingatia haya makazi mpaka niyamalize ni saa kumi na moja[emoji19][emoji19]Mimi mda huu nimetoka kuchukua kilo 3 buchani nataka niiandae mwenyewe ndio hua nainjoi zaidi. Mchana naipiga na ugali mkubwa sana inayobaki jioni inapigwa na ndizi rosti..[emoji39][emoji39] Bila kusahau coke baridi na altar wine
Ni kweli kabisaAsilimia 70 ya wanaosema hawali kiti moto hula pembeni...
Mkuu acha kunitamanisha basi ukizingatia haya makazi mpaka niyamalize ni saa kumi na moja[emoji19][emoji19]
Na hii nimeihifadhi kimakusudi
Maliza kurost unirushie ebu[emoji39][emoji39]Hahaaa... usijali mkuu ntakutumia na picha ili nikufuruge kabisa akili lako [emoji23][emoji23]
Nimekula mara kadhaa sehemu tofauti tofauti nkaona niwaachie muendeleeYawezekana ulilishwa kibudu, au mkaangaji alikuwa hajui.
Asubuhi yako si ya wangeni kwa mfano hapa nilipo mimi ndio saa11 asubuhiAkili za kimaskini ni hatari Sana inakuaje asubuh yote hii unawaza mambo ya kulakula