Kwanini baadhi ya madereva na makondakta wa daladala ni wachafu?

goukun wadey

JF-Expert Member
Apr 22, 2020
241
284
1610012498510.png

1610012743690.png
Tanzania na hasa Dar es Salaam, kuna uchafu wa kutisha ambao hautajiki kabisa sijajua kwa nini, ni mazoea au hauonekani, sio rahisi kusikia utajwe na watu serikalini, binafsi, mashirika, wala viongozi wa umma.

Nakumbuka usafi wa Jumamosi ulivyozingatiwa lakini huu wa makondakta na daladala zao.

Unaamka asubuhi ukiwa upo smart ila unawaza ukifika kwenye daladala hadi ushuke hali itakuwaje! Viti ni vichafu, sare za makondakta ni chafu, dereva ni mchafu na sare yake ni chafu. Ukitaka uone mashindano ya CHAFYA duniani basi ingia kwa Daladala utafurahi kama sio huzuni. Kwanini?

Pia soma: Makondakta wameiga kutoka wapi uchafu?
 
Ndo mana hua sishangai mtu akichukua mkopo akanunua gari kabla ya kuanzisha biashara na kujenga nyumba pale anapopata kazi.

Anyway nmemkumbuka Makonda, amewahi kuwaadabisha kidogo wakawa smart kipindi cha mkutano wa SADC.

Asubuhi njema.
 
Kipindi nipo advance nilipanda daladala asubuh mwenyew msafi kama kawaida yangu

Niliambulia kukalia mavi kweny siti, sijui nan alifany uozo ule

Ilikuwa siku ya Ijumaa nilienda shule nanuka 😑
 
Kazi yao ngumu sana, wanaamka saa kumi, wanalala saa sita....
Kama kijana Hana mkee anayemjali lazma ageuke mchafu
Hivi wasimamizi wa sheria za usalama barabarani hakuna kosa linalohusiana na uchafu? Kama halipo na wao wanatuambia wapo kwa ajili ya usalama wetu je isingekuwa sawa uchafu kuwa ni sababu mojawapo inayohatarisha usalama wetu! Angalieni mutuokoe kama itaafaa
 
Uchafu na Usafi ni tabia ya mtu, ni ngumu sana kumshurutisha mtu mchafu awe msafi au mtu msafi awe mchafu.
 
Tanzania na hasa Dar es Salaam, kuna uchafu wa kutisha ambao hautajiki kabisa sijajua kwa nini, ni mazoea au hauonekani, sio rahisi kusikia utajwe na watu serikalini, binafsi, mashirika, wala viongozi wa umma.

Nakumbuka usafi wa Jumamosi ulivyozingatiwa lakini huu wa makondakta na daladala zao.

Unaamka asubuhi ukiwa upo smart ila unawaza ukifika kwenye daladala hadi ushuke hali itakuwaje! Viti ni vichafu, sare za makondakta ni chafu, dereva ni mchafu na sare yake ni chafu. Ukitaka uone mashindano ya CHAFYA duniani basi ingia kwa Daladala utafurahi kama sio huzuni. Kwanini?

Pia soma: Makondakta wameiga kutoka wapi uchafu?
Muda tu wa kulala na kupumzika wanaupata kwa shida, sasa Muda wa kufanya usafi watautoa wapi ??

Daladala linaendeshwa mpaka saa 5 au 6 usiku, then kuanzia saa 8 au saa 10 usiku liko barabarani.

Sehemu kama Buguruni, Ubungo Daladala zinakesha.

Hesabu za boss, Tsh 70,000, 80,000 mpaka Tsh 120,000 inategemeana.

Hapo hamjapigwa bao na traffic na wenyewe usipowalipa ndani wimi pesa i a Riba.

Hapo hujahesabu namna ilivyo stress kwa Daladala, madereva na makonda kutwa nzima kugombana na abiria.

Tena unapaswa ushukuru Mungi kabisa hao madereva wanajitahidi kutoleta ajali, akisinzia kwenye usukani kumwagana nje nje
 
Pole sana, kuna daladala za Kariako - Mabibo, halafu zile za Kawe - Temeke aise huwezi amini utahisi ni za mifugo.
Jana nilipanda ya Temeke Gomz nilitamani kuvulia nguo nje niziache huko huko. Issue ya kujikuna kawaida Sana yaani ni Bora uwe na kagari kakuoshea kwenye sinki lakini sio uchafu WA kwenye baadhi ya daladala.
 
Sema rangi ya sare zao hafifu zikichakaaa ndo balaa hazitamaniki
 
Back
Top Bottom