Kwanini baadhi ya dini kama "Ismailia" hazihamasishi wala kushawishi waumini wapya kujiunga nao ?

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
14,631
2,000
Hello,
Imekuwa ni kawaida kuona baadhi ya dini zinatumia nguvu kubwa sana kushawishi watu kujiunga nao.
Tena kuna baadhi ya dini zinatumia mpaka vitisho na mapigano kuhakikisha wanapata waumini wapya.
Sasa inakuwaje baadhi ya dini kama hawa Ismalia hatuoni harakati zozote za kutafuta waumini wapya ?
 
Jul 30, 2019
69
125
Mbona Uislam ni dini ya waarabu lakini hadi watu wengine wanashisiki, vivyo hivyo kwa wakristo ni dini ya masharti ya kati.

Naomba nikurekebishe ndugu yangu u Kris to Siyo DINI, kama ujuavyo ww Bali UKRISTO ni LIFESTYLE NI MAISHA na Sio Dini watu wanakosea Sana Ndio maan watu wengi wanashindana na ukristu /ukristo wakifikiri ni Dini LA hasha ni maisha. Au lifestyle . unaweza ukanihoji DINI ni nini na ukristu ni nimi??
DINI ni mapokeo /wakati UKRISTO ni Maisha ya mtu wa KRISTO SI KILA mtu anayekwenda Kanisani ni mkristo LA hasha
 
FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
22,196
2,000
Mbona Uislam ni dini ya waarabu lakini hadi watu wengine wanashisiki, vivyo hivyo kwa wakristo ni dini ya masharti ya kati.
Waliwapa hizo dini zao ili wawatawale kiuchumi, kisiasa, kitamaduni na kijamii, yaani mmekwisha kabisa nyie mlioacha imani zenu na kufuata dini na tamaduni za wakandamizi wenu.
 
Mr Q

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,058
2,000
"Alikuja kwa walio wake nao wakamkataa." Pengine ndio maana mnajua habari njema ya wokovu kwa sababu ilibidi aliyekataliwa na walio wake4 aje huku kwingineko.
si nukuu rasimi hiyo

Sasa kwa upande wao nadhani alipokuja kwao hawakumkataa kwahiyo hakukuwa na haja ya kwenda kwa mataifa mengine
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
27,491
2,000
Dini zote za kikabila huwa hazitafuti waumini.Dini za kiasili za makabila huwa hazitafuti waumini.wa makabila Mengine.Ismailia na wahindu ni dini za kikabila.Mhindi hatafuti muumini asiye muhindi kujiunga na dini Yake.Ila dini zisizo za kikabila hutafuta waumini mfano Wakristo madhehebu yote Wana wamisionari ambao Toka miaka hiyo wawe katoliki au wamisionari Walokole kazi yao Ni kusaka waumini Kuanzia Roma Hadi Tanzania na ulimwenguni.kote uwe uanglikana,ulutheri nk
 
Flano

JF-Expert Member
Aug 7, 2019
549
1,000

Vipi kuhusu dini ya uyahudi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom