The thing is mmekaa kwamuda huo bila kufunga ndoa na nakuomba tu ufanye uchunguzi kwani haya mahusiano yapo sana,lakini baada tu ya kufunga ndoa mambo yanakuwa mengine
Kwanini?
Hilo ndilo swali la msingi!
Inategemea ni kwa nini muda wote huo hawakufunga ndoa,Kama tatizo lilikuwa ni la nje(mfano wazazi walikuwa hawataki baadae wakawaruhusu)inawezekana hiyo ndoa kudumu.
Pia kama taratibu za kuunganisha mahusiaon zilifanyika mahari ilitolewa wazazi wakabariki mkaishi bila ndoa ya karatasi hata mtakapoamua kuwa na karatasi mtadumu.
lakini kama tatizo ni kukosekana kwa utayari wa kufunga ndoa kati ya wapenzi hao wawili,pamoja na kuishi miaka mingi na kuzaa watoto hiyo ndoa ikifungwa kuna uwezekano mkubwa ikafa.kabla ya ndoa yule asiyekuwa na utayari wa ndoa anafikiri muda wowote anaweza akaondoka kwenye hayo mahusiano,anaweza akamfanyia chochote mwenzie bila kujali maumivu yake, na mwenye utayari ni rahisi kuvumilia hasa kama wamesha zaa. baada ya ndoa yule aliyekuwa na utayari wa ndoa atakuwa na matumaini ya kuwa mwenza wake atam-treat vizuri kwakuwa ameji-commite kwenye ndoa inapokuwa tofauti ni ngumu kuvumilia tena.Na wengine wapo kulipa visasi.
Kuna binti alipobeba mimba boyfriend alimnanga sana kuwa amemtega na hawezi kuwa na mke kama yule,baada ya ushauri wa marafiki na ndugu boyfriend akaamua kuishi na binti wakazaa na mtoto wa pili wakaishi maiaka4,mume akaokoka akaamua afunge ndoa na mkewe,ndoa imefungwa tu usiku mke akamkumbusha mume alivyomnanga na akamwambia alikaa nae ili alipe kisasi, toka siku hiyo amani ikatoweka mke hana muda na mume,akatafuta uhamisho kazini kwenda mkoa mwingine ili awe mbali na mumewe huu mwaka wa pili,mke hajishughulishi na chochote cha mumewe,mume aliwahi kumfuata kuona watoto akaambiwa akitaka kuongea na watoto zaidi ya siku moja akakae hotelini asubuhi anawachukua jioni anawarudisha.
Pia ukifuatilia sana hayo mahusiano ya miaka 8 bila ndoa bila
sababu ya maana na watoto mnazaa hamna furaha/amani ya kweli, kuna mmoja anaumia na kuvumilia sana.