Hebu tukae hapo kabla ya ndoa .......^^
Kuna tofauti ya maisha kabla ya ndoa, ndani, na baada ya ndoa. Kabla ya ndoa ni kukubaliana ili usipoteze penzi, ndani ya ndoa ni sheria, na baada ya ndoa ni kanuni ya majuto na lawama.
^^
Habari za jioni?
Ntumai mpo poa .....
Kama kawaida huwa siji na hoja hapa bila kuifanyia utafiti angalau kidogo na kupata mwanga,niliwahi kusikia na kusoma sana kwenye majarida na magazeti na zaidi nimeshuhudia watu wakiniambi jambo hili kuwa,kama kuna watu waliishi kwenye mahusiano kwa muda mrefu na kupendana na kuishi kwa amani kama mke na mume lakini hakukuwa na ndoa yaani yale makaratasi na ikaja wakaoana hupita muda mfupi na wanaachana
Nimekutana ma mahusiano ya aina hii ma 5 yaani watu walikuwa hawajaoana na waliishi maisha ya furaha kabisa lakini baada tu ya kuoana walitengana
Nilijaribu kuwauliza sababu hakuna aliyenipa sababu ya kushikika lakini kila mtu alikuwa anamtupia lawama mwenzake kuwa ndiuo alisababisha ndoa kufa,ukiwauliza kama ni mwenzake ni kitu gani kiliwafanya wasiachane wakati ule hawajafunga ndoa kunakuwa hakuna jibu
Hadi sasa sijapata jibu lakini kitu ambacho nina uhakika nacho kuna idadi kubwa sana ya mahusiano ambayo yamechukua muda mrefu nayalipokuja kubadilika na kuwa ndoa watu hawa ambao waliishi kwa amani muda mrefu sana wanaachana
Inawezekana kuna mtu ambae anaweza kuwa ana jibu ya hili naomba anijibu .....!!
Una uhakika na unachoongea au unarahisisha tu?
kwani Mungu aliposema Msizini alikua na mana gani?
Hapo jibu ni moja tu mnapokua katika uchumba na kuzini mmnakua rafiki wa shetan sasa mnapofunga ndoa mnakua adui yake mana mshaingia ktk hatua bora lazima aingize mkono wake.
Hiyo 100% umeipima na nini?
So ushauri ni kuoana na mtu ambaye hamjawahi kukaa kwenye mahusiano ya muda mrefu kabla ya ndoa au?
Hebu tukae hapo kabla ya ndoa .......
Haya mambo unayavumilia kwa miaka 8 halafu yanakuja kukushinda kumaliza hata mwaka baada ya ndoa?
The devil at work. Kabla ya ndoa you are already his; siku ya ndoa mnamfukuza. Then anatafuta weak point (hasira, tamaa,chuki, wivu, uchoyo, ulafi, ulevi) then anajiattach na kuwaattack. Ndoa kaputi, back to uzinzi.
^^
Miaka 8 upo kwenye uchumba? Unasubiri nini kitokee ambacho dunia haijui?.. Hayo ni mahusiano ya wizi, na aghalabu huishia kuvunja ndoa maana wezi wawili hawakai kichaka kimoja
^^
Unajua maana ya kuwa na hakika kwa 100%?
kabla ya ndoa wengi wanaficha makucha baada ya ndoa wanajionyea uhalisia wao
Mkuu sidhani ...
Kwenye mahusiano ndio mahali ambapo unamuangalia mwenzako kama anakufaa,sasa mnapoingia kwenye ndoa hapo ni kufa na kuzikana na hapo ndipo ambapo uvumilivu unahitajika
Inakuwaje mmeishi kwa miaka mi 5 halafu mkisha funga ndoa tu hata mwaka hauishi mnakuwa mmeachana?
Wewe umesha oa/olewa???