Kwanini baada ya kuoana tumeachana?

Kwanini baada ya kuoana tumeachana?

Sijaingia kwenye ndoa bado, so ntakujibu kile ambacho nakifikiria na ninachokishuhudia kwenye hizo ndoa....na ndo maana neno "labda" linahusika...

So nawaza labda kabla hawajaingia kwenye ndoa kila mtu alikuwa anajifikiria kama "yeye", Akitaka kufanya kitu "mimi" ndo ilikuwa inahusika zaidi yani ile Me, my self and I...
Lakini kumbuka ndoa inaleta muunganiko wa mambo yote, financial, social n.k
Baada ya ndoa hamna tena umimi bali ni "sisi"
Kama ulikuwa unatoa robo ya mshahara kupeleka kwenu sasa inabidi umshirikishe mwenzio, mapato na matumizi lazima yajulikane na yapitishwe....hapo ndo bifu zitaanza kwa sababu utahisi umeingiliwa uhuru wako...

Halafu sehemu nyingine watu wanayokosea ni ile tabia ya kuvumilia hata visivyovumlika kwa kujipa moyo kuwa baada ya ndoa mambo yatabadilika...
Watu tuna matumaini makubwa sana kabla ya ndoa, so mnapoingia kwenye ndoa na kuona mambo ni yale yale ndo hapo mnawaza kuachana.....!

Sidhani kama inawezekana kuishi pamoja miaka 8 halafu muwe mnaishi kwa aina ya mimi na sio sisi

Mtakuwa mmezaa na huduma zote zinafanyika kama wanandoa kinachokosekana hapo ni ile hati tu ambayo ndio kisheria inawafanya nyie kuwa wanandoa lakini kijamii nyie tayari ni wanandoa

Swali ni kuwa baada ya kudshirikiana yote hayo kwa muda wote huo,inakuwaje baada ya kuipata ile hati ambayo inatutambulisha kisheria kuwa ni wanandoa ndoa inatushinda?
 
Kwa watu wengi ndoa ni zaidi ya hati.
Nina rafiki yangu aliolewa, ila kama kawaida alishakutana kimwili na jamaa mara kibao, alikuwa anaenda kwa jamaa anakaa wanapika na kupakua...lakini cha ajabu akanambia kuwa siku ya harusi alikuwa anatetemeka, alikuwa anawaza wakifika room itakuaje, na akanambia siku ile alihisi tofauti wakati wanamake love...

So huo ni mfano tu wa matumaini walonayo watu kabla ya kufunga ndoa, tena wanayakuza matumaini haya kisaikolojia na wanataka yatokee katika nyanja zote....yani katika kupanga matumizi basi mtu anaona akishaoa tena basi ajue mshahara wa mkewe au mumewe wote unaishia wapi..
Kama mume mlevi basi mke anajipa moyo kuwa baada ya ndoa ataacha na atakuwa anawahi kurudi nyumbani...
Kama mchepukaji basi mtu atavumilia akiamini baada ya ndoa ataacha....!

Kwa watu wengi ndoa ni zaidi ya makaratasi!
 
Kukosea kuchagua, kufata vitu fulani vipendezavyo moyo, tamaa, kutoridhika na hali ya mwenzako, fitina, vyote hivi vinachangia ndoa kuvunjika mapema baada ya kufungwa
 
Mi naona watu wakishafunga ndoa wanaona wameshakula viapo kila mmoja anajiachia atakavyo, hamna anaeogopa tena kuachwa.Uvumilivu ukikosekana apo ndio kuachana kunafuata.Hii inakua tofauti na pale ambapo bado hamjapata vyeti vya kuhalalishwa kila mmoja anakua na uoga flani.
 
Kwa watu wengi ndoa ni zaidi ya hati.
Nina rafiki yangu aliolewa, ila kama kawaida alishakutana kimwili na jamaa mara kibao, alikuwa anaenda kwa jamaa anakaa wanapika na kupakua...lakini cha ajabu akanambia kuwa siku ya harusi alikuwa anatetemeka, alikuwa anawaza wakifika room itakuaje, na akanambia siku ile alihisi tofauti wakati wanamake love...

So huo ni mfano tu wa matumaini walonayo watu kabla ya kufunga ndoa, tena wanayakuza matumaini haya kisaikolojia na wanataka yatokee katika nyanja zote....yani katika kupanga matumizi basi mtu anaona akishaoa tena basi ajue mshahara wa mkewe au mumewe wote unaishia wapi..
Kama mume mlevi basi mke anajipa moyo kuwa baada ya ndoa ataacha na atakuwa anawahi kurudi nyumbani...
Kama mchepukaji basi mtu atavumilia akiamini baada ya ndoa ataacha....!

Kwa watu wengi ndoa ni zaidi ya makaratasi!

Kama mtu amekuwa mlevi kwa miaka 8 halafu utarajie mkifunga bdoa atabadilika ni tatizo kubwa sana

Inawezekana tatizo linaloonekana hapa ni la kisaikolojia zaidi

Mtu mlikuwa mnapakuana kila leo halafu siku ya ndoa unaogopa

Unaogopa nini sasa?

Ai ile kwamba "huu sasa ni mzigo wangu hadi kifo"?
 
Mi naona watu wakishafunga ndoa wanaona wameshakula viapo kila mmoja anajiachia atakavyo, hamna anaeogopa tena kuachwa.Uvumilivu ukikosekana apo ndio kuachana kunafuata.Hii inakua tofauti na pale ambapo bado hamjapata vyeti vya kuhalalishwa kila mmoja anakua na uoga flani.

Kwahiyo unajichunga kwa iaka 8 halafu baada ya ndoa tu unafungulia!?
 
Kama mtu amekuwa mlevi kwa miaka 8 halafu utarajie mkifunga bdoa atabadilika ni tatizo kubwa sana

Inawezekana tatizo linaloonekana hapa ni la kisaikolojia zaidi

Mtu mlikuwa mnapakuana kila leo halafu siku ya ndoa unaogopa

Unaogopa nini sasa?

Ai ile kwamba "huu sasa ni mzigo wangu hadi kifo"?

Nafikiri hilo ndo jibu, labda kabla ya ndoa mtu alikuwa anawaza kuwa wanaweza kuachana muda wowote, na ukishakuwa na mawazo hayo huwezi kuwa responsible asilimia zote kwa mwenzio kwa sababu unawaza anythig can happen, at any time...

Ila baada ya ndoa unawaza huyu tena ndo wangu, hadi kifo...unajifeel responsible kwake...sasa hapa hata yale mapungufu yake utayaona...chongo utaliona chongo wala si kengeza tena....!

Watu wengi na mimi nikiwemo tunaamini ndoa ni "nchi ya maziwa na asali"
 
Tatizo mi naona miaka ya hivi karibuni tumekosa hofu ya mungu..kukurupuka kwenye maamuzi unakuta mtu anaamua kuolewa ili alipe fadhila...mwingine amekurupuka tu kutokana umri umemfika kwahyo unakuta anataka aolewe faster mwisho wa siku wakiingia kwenye ndoa wanachoka kwa sababu hakuna true love iliyowaunganisha...! Sababu ingine uaminifu kwenye ndoa umekosekana sikuhizi hii michepuko inaleta hasira sana kwenye ndoa.inafikia kufanya ndoa nyingi kuvunjika
 
Aisee .....!!

Surely, kuna ndugu yangu aliishi na mwanaume miaka kama kumi bila ndoa.Walikua na migogoro ya kawaida tu.Baada ya kufunga ndoa migogoro ikawa mikubwa zaidi ingawa hawajaachana.Af kwenye ile thread yako nyingine( ya kusifiwa) mbona umekataa kunielewesha.
 
Nafikiri hilo ndo jibu, labda kabla ya ndoa mtu alikuwa anawaza kuwa wanaweza kuachana muda wowote, na ukishakuwa na mawazo hayo huwezi kuwa responsible asilimia zote kwa mwenzio kwa sababu unawaza anythig can happen, at any time...

Ila baada ya ndoa unawaza huyu tena ndo wangu, hadi kifo...unajifeel responsible kwake...sasa hapa hata yale mapungufu yake utayaona...chongo utaliona chongo wala si kengeza tena....!

Watu wengi na mimi nikiwemo tunaamini ndoa ni "nchi ya maziwa na asali"

Aisee ......

Unadhani matarajio ndio tatizo pekee kwenye jambo hili na hakuna kingine ambacho kibafanya watu ambao wameishi kwa amani na utulivu kwa miaka zaidi ya 7 na kuja kuachana muda mfupi tu baada ya kufunga ndoa?
 
Back
Top Bottom