Kwanini awamu ya tano wanatudanganya SGR ni mwendo kasi wakati ni mwendo wa wastani?

Mkuu hata ingekuwa ya kasi unayoitaka wewe lazima ungetafuta kasoro ingine...hater is hater hana jina lingine litakalomfaa,la msingi hapa ni kuea hii reli tumeijenga wenyewe kwa fedha zetu za ndani na ndio reli ya kwanza kujenga wenyewe baada ya ile ya kati ya wakoloni..
 
SGRs zina speed tofauti na hilo kila mtu mfuatiliaji analijua. Haijawahi kusemwa kama Tanzania ni ya kwanza kuwa na SGR. Wengi tunajua Kenya ndio iliyoanzisha, Tanzania tukaduatia. Lakini uzuri, treni zetu itakuwa na kasi kuzidi za Kenya. SGR yetu ni pana kuliko ya Kenya, ina urefu mkubwa zaidi na ya Kenya na imetumia gharama ndogo kuliko ya Kenya.
What about quality? Na yenyewe ni bora kuliko ya wakenya?
 
Naamini uzi huu utasomwa na wahusika wa mradi huu kuanzia TRL yenyewe na wizara ya Miundombinu.... Nitumie fursa hii iliyotolewa na mtoa hoja kuhoji maandalizi ya ujenzi wa reli yetu mpya nikijikita zaidi kwenye uchafuzi wa mazingira.

Treni zinazotoa huduma kwenye reli ya kati hata zile za TAZARA zimetengenezwa kwa mtindo unaoruhusu wasafiri kujisaidia juu ya reli huko maporini treni ikiwa kwenye mwendo na kukataza kutumia vyoo vya treni pale inaposimama vituoni. Imekuwa hivyo miaka yote na naamini hadi leo hali ni hiyo.

Ujenzi wa reli hii mpya na miundombinu ya mabehewa na injini zitakazotumika, vitazingatia suala la usafi wa mazingira kwa kutumia vyoo kama vile vinavyotumika kwenye ndege au watu wataendelea kutupa vinyesi kwenye reli?. Ningependa sana kujua changamoto hii wataitatuaje.
 
Mkandarasi wa SGR yetu Yapi Merkezi mkataba wake ulitakiwa kumalizika mwanzoni mwa mwezi Novemba yaani mwezi ujao. Pia tulitangaziwa kuwa treni ya mwendo kasi itaanza kwenda Moro mwishoni mwa mwaka huu. Lakini ukiangalia mwenendo wa ujenzi sidhani kama hilo linawezekana
Hilo haliwezekani hata kwa dawa kwa ujenzi unavyoendelea labda itakamilika 2020 mwishoni
 
Mimi nasubiri hii treni ya mwendokasi itakayotumia saa moja unusu kufika morogoro inaanza lini kazi na tiketi zinapatikana wapi, haya maneno mengine naona kama ni blah blah tu..
 
Shida hakuna Hela jiwe analipuka tu
Mkandarasi wa SGR yetu Yapi Merkezi mkataba wake ulitakiwa kumalizika mwanzoni mwa mwezi Novemba yaani mwezi ujao. Pia tulitangaziwa kuwa treni ya mwendo kasi itaanza kwenda Moro mwishoni mwa mwaka huu. Lakini ukiangalia mwenendo wa ujenzi sidhani kama hilo linawezekana
 
Heshima kwenu wakuu,

Kwanini hawa jamaa wanatudanganya SGR ni mwendo kasi wa treni? Inamaana hawajui SGR ni mwendo wa kawaida?

Kwanini wanatudanganya sisi watanzania wanyonge?

Duniani ni treni ya Shanghai Maglev peke ndo ya mwendo kasi wa speed ya 267.8 mph. Na hii ya Morogoro tunayodai ni mwendokasi, inaenda Speed ya 75 mph. Kwanini twadanganya na ili iweje?

Kwanini wanatudanganya eti Afrika Mashariki, Tanzania ndo nchi ya kwanza kuwa na reli ya SGR?

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta leo jumatano alizindua rasmi awamu ya 2A ya reli ya kisasa (SGR) kutoka Nairobi hadi Naivasha.

Shughuli kuu ya uzinduzi ilifanyika katika kituo cha SGR cha katika eneo la Mai Mahiu.

Aidha huduma ya treni ya kubeba abiria itaanza rasmi kesho alhamisi huku ile ya uchukuzi wa mizigo ikianza baada ya miezi kadhaa ijayo wakati Tanzania bado inapambana na wapinzani wa kisiasa na kuwaweka korokoroni.

Watanzania wanazunguka nchi nzima kutangaza wanajenga SGR wakati Kenya wao wanazindua kimya kimya.

Ni wakati wa vitendo si maneno. Kenya wapo juu.

SGR ni Standard Gauge Railway. Sio High Speed Gauge Railway. Tuweni makini tunapoongea na wanyonge wa nchi hii.
SGR ya Kenya inatumia Mafuta only wakati SGR ya Tanzania itakuwa inatumia Umeme kwa kias kikubwa na mafuta kwa emergence tu
 
Back
Top Bottom