Kwanini Ali Kiba hataki bifu lake na Diamond liishe?

Jux juma

JF-Expert Member
Feb 27, 2017
871
691
Habarini wakuu
Nimetokea kushangaa sana kuona Alikiba baada ya Diamond kuonekana akizungumza kwamba hana tatizo na kiba naye kiba kaonesha katika mtandao wake wa Instagram kwamba hajaridhia kabisa ili bifu lije liishe.....

Ni kwann alikiba hataki liishe kwani annufika kwa kiasi gani na jee inamaanisha hawezi kusonga bila ya bifu!

Screenshot from 2017-03-15 07-59-13.png
 
Tatizo lake huwa hapendi kujishusha inapobidi ili apate zaidi, mwenzake anajua anapotaka kwenda, hivyo nyakati fulani anapohitajika kujishusha hufanya hivyo ili apate hatua zaidi, hapo ndo D anapomzidi mwenzake, anapenda kujifunza.

D haoni aibu kujipendekeza Kwa mtu ambaye anahisi amemzidi na anaona atapata kitu kutoka kwake, lakini mwenzake hapendi kujishusha anapenda kujiweka juu tu muda wote, hili linampotezea fursa nyingi, mfano angalia tu akaunti zao za IG itakupa picha ya ninachoongea, yeye anajiona ana umaarufu wa Beyonce.

Ally Alipaswa kuwa mbele ya D kwa sababu alianza gem na alitoka muda mrefu, lakini imekuwa tofauti kwa sababu ya kuridhika mapema na kutotaka kujipendekeza kwa walio mbele yake.

AJISHUSHAE ATAKWEZWA NA AJIKWEZAE ATASHUSHWA
 
Back
Top Bottom