Haya ndo majibu ya Alikiba na Harmonize kwa Diamond Platinumz baada ya kupata mwaliko wake...

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Saa chache baada ya msanii, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz kuwaalika Harmonize na Ali Kiba katika tamasha la Wasafi, wawili hao wameibuka na kumjibu.

Wakati Ali Kiba akimtaka Diamond kutomfuatilia akitumia neno “unikome”, Harmonize amesema hataki kuongea kuhusu jambo hilo.

Leo mchana Jumatano Oktoba 30, 2019 Diamond wakati akizungumzia tamasha hilo litakalofanyika Novemba 9, 2019 jijini Dar es Salaam alisema ana imani Harmonize atashiriki na kwamba amepeleka mwaliko kwa uongozi wa Ali Kiba, ili msanii huyo naye ashiriki tamasha hilo.

"Wenzetu (wasanii) Nigeria ndio maana wanaendelea kwenye muziki kwani kunapokuwa na matamasha kama haya wanaweka tofauti zao pembeni, kumkuta jukwaa moja Wizkid na Davido ambao walikuwa na bifu kwao ni jambo la kawaida.”

“Kwa nini tung’ang’anie bifu hata sehemu ambayo ni ya kutengeneza pesa na kutuleta Watanzania pamoja,” amesema Diamond katika mkutano wake huo na waandishi wa habari.

Baada ya Diamond kueleza hayo, Mwananchi lilimtafuta Ali Kiba kujua kama ataweza kushiriki katika tamasha hilo na msanii huyo alisema hawezi kulizungumzia hili.

Baada ya muda Ali Kiba alimjibu Diamond kupitia ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Instagram, “usiniletee mambo ya darasa la pili unaniibia penseli halafu unanisaidia kutafuta unikome.”

“Mwanaume huwa anaongea mara moja tu sasa ukitaka nikuweke uchi watu wajue unayonifanyia hata kwenye hilo tamasha hatokuja mtu sasa tuishie hapo nakutakia tamasha njema.”

Wakati Ali Kiba akieleza hayo, Harmonize alipoulizwa na Mwananchi amesema, “achana na hayo mambo ya Diamond, tuongee mambo mengine.”

PIC%2BALIKIBA.jpeg
 
Kuna kitu kibaya Diamond "anaweza takuwa" amemfanyia Kiba ndio maana kila wakati anataka wayamalize, kama ni hivyo bora aombe msamaha yaishe maana kosa halina muda wa kuisha bila kuondoa tofauti, kama anaona muda umepita kosa limepita atakuwa anajidanganya.
 
Kuna muda inabidi mtu aache unafiki tu. Mondi huwa akiwa kwenye press huwa anajuwa kucheza na akili za watu kwa kujifanya innocent na asiyekuwa na tatizo na wenziwe.Ila yaliyoko moyoni kwake na kamati yake ya ufundi wanayoyafanya ni ushetani tu. Ila wote ni wasanii wetu tuwasapoti tu.
 
Ukiielewa hii sentensi "unaniibia pencil harafu unanisaidia kuitafuta" na
"ukitaka nikuweke uchi watu watu wajue unachonifanyia, basi hilo tamasha hatokuja hata mtu mmoja"

Ukizielewa hizi sentesi utagundua Ali ana kitu kikubwa alichofanyiwa na Mondi (mawazo yangu ni views za youtube n.k), na Ali hataki kusamehe.

Pia nia ya Mondi ni kuiangusha Clouds, hivyo anajifanya kumaliza bifu na Kiba ili awashinde clouds. Pia Mondi anajifanya hataki bifu mbele ya watu huku akifanya mambo ya ajabu nyuma ya pazia. Leo hii anamtaka Harmonize, wakati kwenye show ya Iringa alimtukana mbele ya watu na hata kwenye sherehe ya juzi kati hapo kamdiss sana harmo.

Mnafiki awakome Harmo na Kiba. Afanye mwenyewe kwani kuna kitu kimewahi kuharibika kwenye hizi festival ambazo Kiba na Harmo hawaja perform.
 
Mimi bado sijaamini Kama Ali amejibu hivyo.
Naimani kuwa wamehack na sio yeye alieandika.
Namuheshimu Sana kiba na Kama ikiwa Ni yeye kweli, nitaanza kumdharau
Hata ungekuwa wewe lazima ukasirike. Yaan mtu anakufanyia vitu vibaya chini ya pazia ila akija mbele za watu anajofanya yeye hana tatizo ila wewe ndiye mwenye tatizo. Ndiyo maana leo ameamua amtolee uvivu, kama alivyofanya kipindi kile cha kiti na malkia wa nguvu.
 
Hata ungekuwa wewe lazima ukasirike. Yaan mtu anakufanyia vitu vibaya chini ya pazia ila akija mbele za watu anajofanya yeye hana tatizo ila wewe ndiye mwenye tatizo. Ndiyo maana leo ameamua amtolee uvivu, kama alivyofanya kipindi kile cha kiti na malkia wa nguvu.
Exactly kiba sio muongeaji ila mpaka anaongea ujue the thing is real
 
Kuna kitu kibaya Diamond "anaweza takuwa" amemfanyia Kiba ndio maana kila wakati anataka wayamalize, kama ni hivyo bora aombe msamaha yaishe maana kosa halina muda wa kuisha bila kuondoa tofauti, kama anaona muda umepita kosa limepita atakuwa anajidanganya.
Diamond Ni boss mzuri Sana, unajua unapotafuta pesa personal issue unaweka pembeni una focus kwenye core subject. Diamond anaweza piga show bila wao na akafanikiwa lakini ameona Ni vyema akawashirikisha jamaa zake, lakini Kama hawataki sio lazima.
 
Back
Top Bottom