Kwanini ajira hakuna?

Ajira ni zoezi endelevu,kwa sababu kuna watumishi wanastahafu kwa mujibu wa sheria kuna wanaofukuzwa,wapo wanaofariki kuna wanaohamua kuacha kazi wenyewe nk.
Kama hakuna ajira kwa visingizio vyoyote vile ni janga kwa taifa,kwa sababu wale wanaoondoka kwenye ajira hawapati watumishi wapya wakuelekeza kazi zinavyofanyika.
Lakini pia hospitalit zinakosa madaktari shule zinakosa walimu wataalamu wa kilimo mifugo nk hawajiriwi,matokeo yake wagonjwa na wanafunzi wanakosa huduma na kila kukicha pengo la ajira linazidi kuongezeka.
Tuliaminishwa kuwa baada ya uhakiki wa watumishi hewa ajira zitaanza lakini kumbe ilikuwa ni uongo.
 
na kwanza kuna haja gani ya mtu kusoma sheria kwa miaka 18 halafu leo hii aende akajiajiri shambani ambako hakuna uhusiano wowote na taaluma yake ya sheria?
Kama wewe nawe ni msomi na una mawazo ya kizembe kama haya basi taifa limepata hasara. Aliyekuambia MTU akisoma basi hapaswi kulima ni nani? Kwa akili yako hii utasugua masufuria kwa shemeji yako mpk uzeeke.
 
Kama wewe nawe ni msomi na una mawazo ya kizembe kama haya basi taifa limepata hasara. Aliyekuambia MTU akisoma basi hapaswi kulima ni nani? Kwa akili yako hii utasugua masufuria kwa shemeji yako mpk uzeeke.

Kubwa jinga wewe.. nimeuliza kuna uhusiano gani wowote wa lazima kati ya hicho kilimo unachokipigia debe na taaluma ya sheria kiasi cha kunitaka mimi niende shambani mara tu nimalizapo masomo?

Na kwanini serikali itumie rasilimali nyingi kunipa elimu halafu baadae inanitelekeza kwa kuniacha niende kutumia elimu yangu mahali isikohitajika hata kidogo?

Kwa unavyojibu watu humu wewe ndio unaonekana wazi unaishi kwa dada yako na umeridhika, hata hapo umevimbiwa ugali wa shemeji.. punguani wahed wewe
 
niende kutumia elimu yangu mahali isikohitajika hata kidogo?
Hivi wewe ulisoma ama umehudhuria darasami tu? Sheria haihitajiki kwenye kilimo? Historia, sayansi ya siasa, ustawi was jamii havihitajiki kwenye kilimo?

Elimu yoyote ile lengo lake ni kumjengea uwezo mwanadamu kuzikabili changamoto zinazomzunguka ktk mazingira take. Sasa kama wewe umesoma halafu unalilia ajira basi hujaelimika.
 
Kwani ukiwa na degree lazima upewe ajira? Acheni ujinga ninyi wasomi, ajira za kupewa hakuna duniani kote. Nendeni mashambani mkajiajiri kwa kulima.

Ni wajibu wa serikali kuhakikisha kila amaemaliza chuo anapata ajira.....kujiajiri ni utashi wa mtu....ndo maana unaona nchi zilizoendelea zinakua na statistics za employment!
 

mwambie atatatua migogoro ya mashamba as a lawyer..lol

Kwa nini usome law walati unaona kama unataka kujiajiri kuna sehemu tatu,biashara,kilimo na teknolojia...

nakubaliana na yeye though,elimu yetu haimuandai mtu kuexplore his environment for opportunities..
 
Ebo, flyover, barabara, shule, mavituo ya afya ukusanyaji bora wa mapato, wezi na majipu kutumbuliwa, uchumi kukuwa, viwanda kede kede halafu unalalamika hakuna ajira? Wewe sasa naona unataka kuhujumu maendeleo tunayoyapata.
My take: Innovate Innovate Innovate. Serikali sio muajiri hata kama ana waajiriwa.

Yale ya juu ni yale ambayo tunaamini kuwa yanaleta ajira. Ni vibarua.
 
Ni wajibu wa serikali kuhakikisha kila amaemaliza chuo anapata ajira.....kujiajiri ni utashi wa mtu....ndo maana unaona nchi zilizoendelea zinakua na statistics za employment!

Ni dhambi au dhihaki kumdanganya mwenzio. Sio wajibu wa Serikali. Serikali ina tengeneza sera kuwezesha watu kujiajiri na kuajiriwa kama na mie sijadanganya hapa basi, tuendelee...tunabanana na kupambana humu humu... statistics nini bana, kazi hamna basi ndio hivyo, hamna.
Hizo nchi zilioendelea, Serikali zimetengeneza kama insurance kwa wale amabao wanakosa ajira, na asilimia kubwa ni kwa vibarua tu


Tanzania yetu lazima hili liende kwa utashi, ni kweli na nakubaliana na yeyote anayeamini hivyo.
Hatuwezi kuwa na sera kama za hizo nchi kwani wao wana maendeleo tofauti katika jamii zao, wanatamaduni ambazo kwangu aidha ni duni kwetu, au ziko kinyume na za Kiafrika au hapa Tanzania
Historia ya dunia, inajirudia ama iko pale pale.
Akili ni mali
 
Pamoja na yotee uliyoyasema athari ya hayo haikuwa hivi kipindi cha Mkapa na Kikwete huyu alienda mbali zaidi kwa kutoa wafanyakazi hewa na wa vyeti feki na bado anawatupa wasomi wengi mtaani.
 
Kwani ukiwa na degree lazima upewe ajira? Acheni ujinga ninyi wasomi, ajira za kupewa hakuna duniani kote. Nendeni mashambani mkajiajiri kwa kulima.
Hivi unajua kuwa kilimo kinahitaji mtaji mkubwa sana.
Sio wote wenye mashamba ya kurithi kama wewe.
Inabidi wanunue,
Ili kilimo kiwe cha kibiashara ni lazima uwekeze vya kutosha.
Mitaji iko wapi?

Tatizo ni kukosa vipao mbele vya kitaifa kwa watanzania .
Kuwekeza kwenye kuwainua watoto wa maskini kwa kuwakopesha mikopo hailipi kwa watawala wanaosaka pesa za kujinufaisha kisasa.
Kuchukua bil. 700 ukanunua Magari ya kifahari ya serikali inalipa zaidi mana kuna 10% inayotolewa na kampuni unapowaunganishia dili kubwa kama hilo.
Tumesahau kuwa watawala ni binadam wasioridhika ,tukaamua kuwaachia kila kitu waamue wao matokeo yake ndio hayo watakimbilia mamiradi makubwa yenye kutoa tenda na usimamizi kwa ndugu na marafiki zao kwa mishahara mikubwa .

Kama Vijana wanaokaa JKT kwa mwaka mmoja wanaweza wakazalisha chakula kingi sana inakuaje hakuna ajira ya maana kwenye kilimo?
Kwa nini wasiwe wanaanzisha mashamba mapya kila mwaka na kuwaachia vijana hao wayaendeshe wenyewe kama mtaji wao huku wakitakiwa kurudisha mtaji wao na kodi kwa serikali ili wengine wapate?

Bila shaka hatuna vipao mbele vinavyowagusa watu wa chini zaidi ya vipao mbele vya kisiasa kwa malengo ya kisiasa na kupiga picha mbele ya kamera.
 
Je tulishawahi kuwekeza kwenye hilo eneo? Au mawazo yetu yote yako kwenye siasa?
 
Akili yako haiko sawa, sorry
 

Kwamba mtu asome sheria au utawala wa uma halafu akimaliza hapo aelekee moja kwa moja kulima viazi? hatumie taaluma ya utawala wa uma kukabiliana na changamoto za kilimo cha viazi?

Punguani kabisa wewe. tena usini quote tena
 
Kwamba mtu asome sheria au utawala wa uma halafu akimaliza hapo aelekee moja kwa moja kulima viazi? hatumie taaluma ya utawala wa uma kukabiliana na changamoto za kilimo cha viazi?

Punguani kabisa wewe. tena usini quote tena
Nitaendelea kuku-quote **** wewe. Maana yaelekea na wewe unajiita msomi wakati hujaelimika. Yaani unaona ajabu MTU kumaliza chuo na kwenda kujiajiri kwenye kilimo?!!! Utaendelea kula kwa shemeji yako mpk uzeeke
 
Aiseeeee
Kama wewe nawe ni msomi na una mawazo ya kizembe kama haya basi taifa limepata hasara. Aliyekuambia MTU akisoma basi hapaswi kulima ni nani? Kwa akili yako hii utasugua masufuria kwa shemeji yako mpk uzeeke.
 
Mkuu ebu ongea kwa ustaarabu..kilimo sio rahisi kama unavyosema..changamoto ni nyingi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…