Kwanini 7/7 na si tarehe nyingine?

Tanzania Nchi Yetu Sote

JF-Expert Member
Mar 12, 2017
505
854

Kwa nini 7/7 na si tarehe nyingine?​

Tarehe iliyopendekezwa ya siku ya Kiswahili duniani ni tarehe 7 mwezi Julai kwa kuwa katika tarehe hiyo mwaka 1954 ni siku ambayo chama cha Tanganyika African National Union, TANU chini ya hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilipitisha Kiswahili kama lugha ya kuunganisha harakati za ukombozi.

Bila shaka, Rais wa zamani na pia Baba wa Taifa la Kenya, Hayati Mzee Jomo Kenyatta, pia alitumia lugha ya Kiswahili kupitia kauli yake maarufu, “Harambee” ya kuhamisha watu wakati wa harakati dhidi ya ukoloni.

Zaid hayo hapo tarehe 7 mwezi Julai mwaka 2000, jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC, ilianzishwa tena kurejesha ushirikiano na utangamano baina ya wananchi wa Kenya, Tanzania na Uganda ambako Kiswahili kinazungumzwa zaidi.

Rwanda, Burundi na Sudan Kusini zimejiunga baadaye na ni wanachama wa EAC.
 
Back
Top Bottom