Ujenzi wa Sekondari ya Kumbukumbu ya Profesa David Massamba Waanza Rasmi - Musoma Vijijini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

UJENZI WA SEKONDARI YA KUMBUKUMBU YA PROFESA DAVID MASSAMBA WAANZA RASMI

Leo, Jumatatu. tarehe 23.10.2023, ujenzi wa David Massamba Memorial Secondary School umeanza rasmi Kijijini Kurwaki, Kata ya Mugango, Musoma Vijijini.

Uamuzi wa kuenzi kazi na mafanikio makubwa ya utaalamu na ubingwa mkubwa wa Lugha ya Kiswahili wa Hayati Prof David Massamba ulifanywa na waombolezaji wote tarehe 30.8.2023, siku ambayo tulimpumzisha nyumbani kwake penye utulivu na amani ya milele!

Matayarisho ya kuanza ujenzi yamekamilika:
*Kiwanja cha uhakika na kikubwa kimepatikana kwenye Kitongoji cha Kati, Kijijini Kurwaki

*Michoro ya majengo imetolewa na Halmashauri yetu (Musoma DC). Eneo la ujenzi (kiwanja) limekidhi vigezo vyote hitajika.

Harambee ya kwanza ya tarehe 2.10.2023 iliyofanyika Kijijini Kurwaki imefanikisha upatikanaji wa:

Saruji Mifuko 481
(ikiwemo Mifuko 250 ya Mbunge wa Jimbo, na Mifuko 50 kutoka kwa Wajukuu wa Hayati Mzee Korogo wa Kijijini Kurwaki)

Mchanga: Lori 45
Mawe: Lori 31

Fedha taslimu: Tsh 615,000
(zikiwemo Tsh 500,000 kutoka kwa Familia ya Hayati Prof David Massamba)

Akaunti ya Benki ya kuweka mchango wako ni hii hapa:
*Serikali ya Kijiji cha Kurwaki
Benki: NMB
Akaunti Namba: 30302301539

TUNAKUKARIBISHA SANA UUNGANE NASI KUMUENZI ALIYEKUWA BINGWA MKUU WA LUGHA YA KISWAHILI HAYATI PROF DAVID MASSAMBA

Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO kutoka Kijijini Kurwaki - imeambatanishwa hapa.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatatu, 23.10.2023
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-10-23 at 00.01.23.mp4
    25 MB
Back
Top Bottom