Hayajamani
JF-Expert Member
- Jul 2, 2012
- 883
- 272
Aisee kuna watu wababe jamani..... nilikua napata kilaji mahala fulani hivi ...kuna jamaa kakaa na binti mzuri sana kama meza ya tatu kutoka tulipokaa...... unajua tena sehemu starabu watu huwa wanaongea kwa sauti za chini na mziki wa sauti ya mbali huku tunashusha vitu baridiii....
Ilikua ni mida ya saa nne au tano hivi usiku.....mara ghafla Jamaa aliyekua kakaa na yule mzuri binti akasimama na kwasauti nzito na ya ukali akamwambia yule dada...USIT*MBWE WEWE UNA NINI BWANA? akarudia tena kwa kumuuliza UNA NINI WEWE USIT*MBWE.
Alivyomaliza hiyo sentisi ya mwisho akamgeukia waiter huku anawasha sigara akawambia aisee tuletee bili tuondoke..
Huwezi amini jamaa kalipa kamshika dada mkono wakaondoka.....dada alikua anatia huruma kama anaenda kuuliwa vile...jamaa alikua kashiba hamna mtu aliyeingilia....
Aisee huyu jamaa kiboko.....
Mngeingilia tu jamaa angeanza na nyie ..... manake huwa wanatafuta sababu ya kumpata mtu wakum 071....