Kwani ni Ushirikiano upi Magufuli anautaka?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
21,320
50,538
Mheshimiwa Rais nimewahi kumsikia akisema kuwa kazi ya kupambana na mafisadi waliotuibia mabilioni ni kubwa hivyo anahitaji ushirikiano na sote kwa pamoja tumpe support.

Ila mimi binafsi nimefeli kuelewa ni ushirikiano gani huo nitoe ili basi washughulikiwe haraka kabla hatujaskia ushahidi wa kuwabana haujitoshelezi.

Naombeni nielimishwe vizuri dhana ya mimi mwananchi wa kawaida kutoa ushirikiano.

Halafu kingine imezuka tabia ya watu wanaohoji mambo ya uendeshwaji wa serikali kuonekana ni nyumbu.

Mtindo huu umeanza kipind hichi mfano sote ni wa Tanzania lakini nikisema nitoe dukuduku langu niulize kwanini sisikii mafisadi hata mmoja wakipigwa mkwara au hata tuhuma zile tunazozijua zikianza kuibuliwa naambiwa eti niache rais afanye kazi yake mimi nimpe tu ushirikiano, sasa ni ushirikiano UPI HUO mnahitaji.

Kwa mfano hasa ukizingatia nina haki ya uhuru wa kujielezea,
Naipenda nchi yangu.
 
Last edited by a moderator:
Ushirikiano wa kuwataja hao wanaoficha madolari kwenye ndoo juu wanaweka nyanya;
 
Ni pamoja na kutoa tarifa za uhalifu/ubadhirifu katika vyombo husika.
 
kwakweli hata mimi sielewi.. labda anawatu anawakusudia pale mawaziri wake na wabunge. i dont know..
 
Ushirikiano wa kubomolewa nyumba, yaani tingatinga likija uwe mvumilivu tu as if hao Watu wa ardhi ndio wameajiriwa leo!
 
Ushirikiano wa kubomolewa nyumba, yaani tingatinga likija uwe mvumilivu tu as if hao Watu wa ardhi ndio wameajiriwa leo!
Hahahaha sio mambo hayo elli
Mimi nimejikita kwenye ufisad
 
Back
Top Bottom