Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,410
Anakufa mtu unayemjua tangu akiwa mzima wa afya hadi alipougua na kufariki. Kabla hujajua amekufa kwa maradhi gani, unaanza kupita ukinong'ona kwamba, amekufa kwa Ukimwi.
Inawezekana ni kweli amekufa kwa ukimwi, lakini hata kama ni hivyo, ni lazima upite ukitangaza kila mahali?
Je itakupa ahueni gani?
Lakini, hivi ikitokea na wewe unafiwa, halafu anatokea mtu au watu wanapita wakitangaza kuwa huyo mtu wako amekufa kwa Ukimwi utajisikiaje? Bila shaka utajisikia vibaya, utaumia na kukereka..... Ni ujinga eh! Ndio ni ujinga kwa sababu umesahau kuwa jana na juzi ulitenda hivyo kwa mwingine.......