Kwani kukosa mtoto ni dhambi?

Kwani kukosa mtoto ni dhambi?

Hivi umewahi kujiuliza mbona jamii iko negative na watu wazima wasiokuwa na watoto?

Unakuta mtu kachelewa kuoa/kuolewa hafu wananzengo wanamuona kama sio wa kawaida flani hivi . Wakati mwingine hata ndugu na wazazi hawaishi kuwashinikiza na kuwasema kwa vijembe!!.

Au inakuaje wanandoa ambao kwa sababu iwayo yote hawajabahatika kupata mtoto jamii haiishi kuwanyooshea mkono??

Ebu mnijuze je ni lazima kila mtu azae?

Hivi hizi negative perceptions tunazoziona kwenye jamii ni kweli zinatokana na kutamani watoto au ni figisu za maisha tu?

Mbona mitaa inawatoto wengi tu wa mitaani na jamii haionyeshi kuwatamani kiihivyo kama wanavyopenda kusumbua maisha ya wanajamii wasio na watoto??.


Wapi tunajikwaa?

Mapokeo au unafiki?



Sent using Jamii Forums mobile app
Sio dhambi ila unataka mtoto wa nani uje umtume mbeleni
 
Maoni yangu juu mada hii: Ni dhambi kama binti atashindwa kupata mtoto kwa sababu ya kuharibu kizazi chache kwa kutoa Mimba ujanani. Bila shaka wengi mnashuhudia wadada na aina hii ktk jamii zetu.
lakini kama ni swala la uumbaji toka kwa Mola, hio sio Dhambi KAMWE.

NAOMBA KUWASILISHA
 
Wengi wanakuwaga wachawi,usiruhusu hizo figisu zifike ndani ya nyumba yako...mke wako asipozaa nje,Mtalea toto la mganga!
 
Back
Top Bottom