Kwani kukosa mtoto ni dhambi?

doppla2

JF-Expert Member
Jun 16, 2014
1,324
1,373
Hivi umewahi kujiuliza mbona jamii iko negative na watu wazima wasiokuwa na watoto?

Unakuta mtu kachelewa kuoa/kuolewa hafu wananzengo wanamuona kama sio wa kawaida flani hivi . Wakati mwingine hata ndugu na wazazi hawaishi kuwashinikiza na kuwasema kwa vijembe!!.

Au inakuaje wanandoa ambao kwa sababu iwayo yote hawajabahatika kupata mtoto jamii haiishi kuwanyooshea mkono??

Ebu mnijuze je ni lazima kila mtu azae?

Hivi hizi negative perceptions tunazoziona kwenye jamii ni kweli zinatokana na kutamani watoto au ni figisu za maisha tu?

Mbona mitaa inawatoto wengi tu wa mitaani na jamii haionyeshi kuwatamani kiihivyo kama wanavyopenda kusumbua maisha ya wanajamii wasio na watoto??.


Wapi tunajikwaa?

Mapokeo au unafiki?Sent using Jamii Forums mobile app
 
ni ulimbukeni tuu, kwani mtu hata ukimpata watakuletea chakula, na huduma muhimu mpaka pale anakuwa mtu mzima? ni vile watu kijitia macho juujuu na yawengine tuu ila hakuna sababu ya msingi kumsema flani hajazaa maana mtoto wa mwenzako ni wako na si lazima wote wawe na watoto hilo husema kila siku ni mtu ajaliwe na awe tayari kumhudumia na kumpa yale yampasayo
 
Kuna wimbo unasema.'kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe'.ukitaka kujua umuhimu wa mtoto fika miaka 50+ na usiwe na mtoto,utaona chungu na tamu ya maisha. Tunakuwa na ujasiri kwa sasa kwa sababu tunatumia hisia za chini kujenga hoja.Mtoto wako ndio rafiki yako kabla ya Ashura,Juma n.k
Kwa hiyo inabid ambae hana mtoto mpaka kufika miaka 50+...awe ameshaaga duniaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wenye 50+ mbona wengi tu kitaa na pamoja kuwa na watoto bado wanaonekana wako frustrated

Nachokiona .. issue sio kuwa na watoto but how are you prepared for old age?
Kuna wimbo unasema.'kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe'.ukitaka kujua umuhimu wa mtoto fika miaka 50+ na usiwe na mtoto,utaona chungu na tamu ya maisha. Tunakuwa na ujasiri kwa sasa kwa sababu tunatumia hisia za chini kujenga hoja.Mtoto wako ndio rafiki yako kabla ya Ashura,Juma n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom