Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,549
Hebu tuambizane ukweli, kudai katiba mpya kuna dhambi gani katika taifa hili mpaka kufikia hatua ya kufungulia na kesi za ugaidi? Kwani mjadala tu wa kuidai katiba mpya una tatizo gani hadi kufikia kukamata viongozi wote wa chama kimoja kilichotajwa kufanya mjadala huo?
Hivi ni kweli CCM hamchukui mifano kutoka mataifa mengine mkajifunza kua movement ya katiba ni suala gumu na kulizuia hamuwezi? Dunia imejua kua katiba ya Tanzania ina kasoro kubwa na ndiyo chanzo kikubwa cha ukandamizaji wa haki za binadamu.Hili suala limeamshwa kulizima ni ngumu maana si la CHADEMA pekee, mnakoelekea sasa mtakamata wanaharakati watakaoendesha mijadala hii na si wanasiasa pekee.
Mnamfungulia mashtaka ya Ugaidi kiongozi ambaye tangu kuanza kwake siasa akiwa kijana mdogo wa miaka 20 hajawahi hata kutuhumiwa kutishia kumpiga mtu achana na kuua, hiki mnachokifafanya kilianza kupata shinikizo la kimataifa tutakua salama?
Jeshi letu linatoa maelezo ya kujichanganya kua halijamkamata Mbowe kwa sababu ya mjadala wa katiba, sasa hao viongozi wengine wa CHADEMA wamekamatwa na kwenda kupekuliwa kwa sababu gani? Hii dhambi kubwa ya jeshi letu itatuvusha? Wanadhani hili jambo linaweza kuzimwa kwa wepesi kiasi hicho?
Hivi polisi wanaelewa maana na madhara ya kukamata kiongozi mkuu wa chama kikuu cha upinzani katika taifa lolote lile? Mbaya zaidi kumtuhumu kwa kesi ngumu kama ya ugaidi mtu ambaye hana historia ya matukio hayo maisha yake yote. Ngoja tupate mashinikizo ya jumuiya za kimataifa ndio tutajua,sisi tujawe na viburi vyetu lakini tutaelewa mbeleni.