Kwani CHADEMA inahitaji back up ya waislam ili kwenda ikulu?watuachie uislam wetu wafanye siasa zao

Status
Not open for further replies.
hawez kuwa imam huyo jamaa huku vipindi vya swala vinampita yeye yuko majukwaani anahubiri siasa

Ndio kwa maana tunasema chadema na wanasiasa wengine wajifunze kuheshimu iman za watu

Mkuu Hii thread unaiweka kisiasa zaidi sasa usifanye nami nikakujibu kisiasa.
Unataka kusema chadema kimchagua Said ni kuvuruga Uislam?

Funguka mkuu haya mambo ya kufanya vitu kwa mazoea acha, yakupasa ujielimishe kila siku ili uweze kuendana na Hii kasi ya mabadiliko ya dunia. Inamaana mtu ukiwa kiongozi wa dini huruhusiwi kushiriki siasa?
 
Nakujib kwa ufupi sana,

Imamu maana yake ni kiongoz wa waumin katika swala

Sisi waislam tunaswali swala tano kwa siku huku tunaongozwa na imamu sisi tukiwa nyuma yake

Sasa jiulize huyu makamu mwenyekiti wa chadema zanzibar ambae anajiita imam muda wa swala huwa unampita yeye yuko majukwaani anainadi chadema kwa backup ya uislam
Masuala ya chama anashughulika nayo 24/7?
JE,kule waumin wake wanaongozwa na nani??
Hakuna maimam wengine?
JE,kuwaacha waumin wake na kukimbilia kuinadi chadema majukwaani ni bora zaid kuliko uimamu wake kwa Allah s,w??
Wewe unadhani siasa haina umuhimu kwa watu?
Halafu mbona unaongea kama vile yeye ni imam pekee Zanzibar yote??
Hapana,Bali huyu Said Mohmed anayatamani sanaa maisha ya dunia ili hali akhera ni kitu kikubwa na chenye thaman kwake,
Anayatamani au wewe unadhani hivyo?
Anyaway sisi hatumkatazi,ila tunamchompinga ni kutumia uislam wake kwa manufaa binafsi ya kidunia
Kuutumia Uislam maana yake nini?
Anautumiaje Uislam?
Hawez imam vipind vya swala vinampita yeye amekomaa kuinadi siasa kisha mimi nisimuite muhuni
Ulivyoandika haya utadhani haufikirii kabisa

Si uwe mkweli tu useme yaliyoko moyoni mwako?

Inaonekana wewe huyu mtu kuwa Chadema au kuwa muislam kinakukera sana
Hayo si masuala yake na muumba wake?
Hilo haliwezekan
Haliwezekani kwa nani?
Wewe umegeuka Mungu wa kumhukumu huyo ndugu?
Hebu acha mambo ya ajabu!!
 
Mkuu Eiyer katika maswali ya Tuko najua hawezi jibu, ebu angalia Tittle ya thread alafu fuatilizia mtiririko wa hoja zake, inamaana yeye target yake haikuwa Uislam ila yeye target yake ni "SAID MOHAMED" na ndio maana kaenda mbali zaidi kufikia kumuita muhuni.

Mtoa hoja kwa wenye uelewa wameelewa nini hasa unataka kuwasilisha, achana na mambo ya Uislam na Ukristo , hiyo kitu haijengi nchi ila inabomoa zaidi. Kama hutaki nikuelewe kwamba unapalilia udini na unaonyesha chuki za dhahiri kwa bwana SAIDI MOHAMEDI, Basi vuka mipaka badilisha tittle ya thread then ongelea suala hilo kwa vyama vyote, Usiattack characters, unapomhusisha Nyerere, JK na Saidi Mohamed katika masuala haya inaonyesha moja kwa moja hujiamini na hautaki kuwaelimisha waislam wenzio.

Huyu jamaa nilimuambia mapema kabisa kuwa hii thread itamshinda
Sasa anajionea mwenyewe!!!!!!!
 
Miongoni mwa kosa kubwa ambalo wanasiasa ama kwa kutoliona au kwa kukusudia kabisa ni hili la wanasiasa la kudhani kwamba kwa kutumia sympathy ya waumin wa dini fulani basi itawasaidia kuwavusha katika changamoto zao za kisiasa na kufanikisha malengo yao ya kuingia ikulu.

Mimi nataka kuchukua kama case study kwa dini yangu,mimi muislam na namna ambavyo wanasiasa wamekuwa wanachukua nafasi zao kwa nyakati mbali mbali kujiingiza katika uislam na waislam kwa ujumla kuwafanya kama hao watu wa jamii hiyo ni mazuzu,wasiojitambau na kuingiza malengo yao kwao kwa matumain ya kupata backup yao na uungwaji mkono.

Hili limetokea mfano kipindi ambacho JK alikuwa anajiandaa kuingia ikulu kwa awamu ya pili ya utawala wake kwa wazi wazi kabisa,kwan CCM ilisimama kidete kuwarubun baadhi ya viongoz wa kiislam hususan wa bakwata na kuwaambia kwamba wawashawish waumin na kuwaambia kwamba endapo CCM itachukua dola basi itahakikisha inawasaidia kuanzisha mahakama ya kadhi na mambo kama hayo,kama hiyo haitoshi ilijinasibu kwa kuweka vipaombele vya waislam kama group linalojitegemea kipekee katika jamii ya watanzania.

Mimi kama Muislam haikunishangaza hata kidogo kwa CCM kutumia janja kama ile,ila niliumia kwa kuona ni kwa namna gani wanasiasa wanajaribu kucheza na hisia zetu katika mambo ya msingi yahusuyo iman zetu kwa maslahi yao kwa dunia yao.

Hili lilianzia tokea enzi ya Julius Kambarage Nyerere,yeye ndie kinara wa haya tunayoyaona kwa sasa na wanachokifanya wengine ni muendelezo tuh wa legacy yake,

Wote mtakuwa mnakumbuka kwamba kwa kias kikubwa sana waislam wameshiriki katika pilika pilika za kudai uhuru wa nchi hii kama group moja linaloojitegemea mingoni mwa magroup mengine yaiyokawepo katika zama hizo,
Na waislam walifanya hivyo sio kwa sababu ya kwamba wallikuwa wanataka kuismamisha dola ya kiislam la hasha,
Walifanya hivyo kwa kuwa wanajua fika kwa mujibu wa mafundisho ya iman yao utumwa,unyanyasi na ukoloni ni dhambi na dhulma kubwa kwa mwanadamu,na kwa mujibu wa mafunzo ya iman yetu tunaambiwa tuipinge dhulma kwa njia zote,thats why unaweza kuona kwamba waislam walisimama kidete kupigania uhuru kwa maslahi ya kujiweka huru na kuliweka huru taifa zima kwa ujumla.

Nyerere kwa kuona juhudi zile,aliingia na taharuki ya kibinadamu kwa kuona nguv ambayo waislam walikuwa nayo enz hizo na kwa kuona kwamba wanaweza kuibuka kuwa group hatari kwa baadae kitu ambacho wala hakikuwa na uhalisia,kwa mamlaka yake AKAAMUA KUWAUNDIA WAISLAM CHOMBO CHA BAKWATA ili kiweze kuwaratibu na kuwaregulate mambo yao on behalf of his goverment,pale ndipo palipokuwa kiini cha haya yanayotokea kwa sasa.

Waislam wakawa wanaratibiwa na kupangiwa kila aina ya propaganda na shutuma pasi na sababu za msingi kana kwamba wao sio watanzania au wao sio wananchi huru,hili lishasemwa sana mimi nafanya kama kukumbusha tuh,na sio nia yangu kuleta malalamiko au shutuma,au kuhubiri utengano katika jamii yangu,naipenda jamii yangu kwa utaifa wangu na uzalendo wa hali ya juu,japo siwez kuikanan iman yangu.

CCM, kwa jambo lile walilolifanya kipindi cha awamu ya pili ya JK waislam waliliona na wamejifunza,lakin niweke wazi kwamba ni group dogo sana la waislam ambao waliingia kwenye mtego ule.nalo ni lile lililofanikiwa kurubuniwa na BAKWATA ambacho ni chombo kilichoasisiwa na NYERERE.

CHADEMA,
Inafuata mkondo ule ule,
Kwa mara nyingi sana na kwa muda mrefu chadema imekuwa kwenye shutuma za malumbano na wanasiasa wenzao wa CCM ya kwamba kwenye chama hiko kuna kasumba za udini na kubaguliwa watu wenye iman ya kiislam kwa wazi wazi bila sababu za msingi,
Inawezekana jambo hilo likawa na uhalisia au lisiwe na uhalisia,ila hoja yangu kuu hapa ni kwamba CHADEMA kama chama,kitafute namna ya kupambana na wapinzani wao kwa utaratibu wao huo huo wa kisiasa,

Wasitake kutafuta sympathy kwa kuchukua baadh ya watu wahun wahun na kuwavisha uislam,kuwavisha madaraka ya uislam kama huyo SAID MOHAMED,makamu mwenyekiti wa chadema zanzibar ili kufikia malengo yao ya kisiaisa kwa kutafuta backup ya waislam.

Tunapinga jambo hilo,mimi sio msemaji wa waislam,.ila mimi ni miongon mwa waislam nilioudhika kwa kitendo hiko kama nilivoudhika kwa vitendo alivyofanya NYERERE kwa waislam,na kama vitendo walivyofanya CCM kwa waislam.

Tunajua uislam unapigwa vita na dunia yote kwa sasa,na tunajua wakati mgumu tunaoupitia,ila sio kwamba hatufaham namna ya kuzikabili changamoto kama hizo,

Tunawaambia chadema kama sample ya wanasiasa wengine waachane na waislam na uislam kama wanataka kuwa salama katika harakati zao,
Sisi hatuwez tumiwa na wanasiasa hata kdgo eti kwa maslahi yao ya dunia,sisi hatuwez kuwa subset ya wanasiasa na siasa zao,

Uislam kama uislam ni mfumo uliokamilika na kujitosheleza kwa kias kikubwa sana,lengo letu ni kuish maisha yanayompendeza mola wetu hapa ulimwenguni na kesho tuweze pata stahiki yetu akhera.

Kama chadema inaamua kutumia proportions ya vingoz wa dini ya kikristo waliopo ndan ya chama chao na kutaka kupandikiza viongoz fake wa kiislam ili kufanikisha kujikwamua kwenye vita vyao dhidi ya CCM,sisi tunawaasa kwamba hilo halitawafikisha mbali,kwani sisi tuna maisha yetu mahususi ambayo hatuhitaji kuingiliwa wala kutumiwa kwa maslahi ya watu fulani.

Ndug zangu waislam,hili suala na mengine kama haya yanapotokea tusiposimama kidete kuyakemea wanasiasa kama hawa wa chadema na wengneo wanaweza dhan sisi ni watu rahis rahis kama wanavyodhania kwa watu wengine.

Naomba Kuwakilisha.
Big Up mkuu, umenena vyema
 
Sasa kwani kiongozi wa kanisa akiuliwa au kufanyiwa uhalifu wowote basi ni suala la waislam kuchinguzwa/kudhaniwa kuhusu hayo matukio? Jenga hoja kutoka kwenye mawazo chanya na si hisia za chuki
 
Huyu jamaa nilimuambia mapema kabisa kuwa hii thread itamshinda
Sasa anajionea mwenyewe!!!!!!!

Halafu angalia anaoshirikiana nao ni wale wale ambao kila kukicha wanapata ban ajili ya kuhubiri udini. Kakosea sana sahivi unaona anajibu kisiasa zaidi badala ya kudefend hoja zake.

Huyu kunakoelekea atatafutia watu ban kutokana na majibu yake mepesi mepesi.
 
Huyu jamaa nilimuambia mapema kabisa kuwa hii thread itamshinda
Sasa anajionea mwenyewe!!!!!!!

May be kama ulikuja kwenye mashindano,lakini kama ni hoja ziko wazi na zinajisimamia zenyewe

Ni hiyari yako kuzikubali ama kuzikataaa,lakin tutaendelea kusimamia kile tunachokiamin
 
Halafu angalia anaoshirikiana nao ni wale wale ambao kila kukicha wanapata ban ajili ya kuhubiri udini. Kakosea sana sahivi unaona anajibu kisiasa zaidi badala ya kudefend hoja zake.

Huyu kunakoelekea atatafutia watu ban kutokana na majibu yake mepesi mepesi.

Kwanin unakuwa na hasira mkuu??

kuwaambia ukweli wanasiasa na kusimamia haki yetu wewe kipi unaumia??

Huna haja ya kujitafutia ban,kama unaona mjadala hauna tija kwako ruksa kuondoka

Tuachie tujadili
 
Masuala ya chama anashughulika nayo 24/7?

Hakuna maimam wengine?

Wewe unadhani siasa haina umuhimu kwa watu?
Halafu mbona unaongea kama vile yeye ni imam pekee Zanzibar yote??

Anayatamani au wewe unadhani hivyo?

Kuutumia Uislam maana yake nini?
Anautumiaje Uislam?

Ulivyoandika haya utadhani haufikirii kabisa

Si uwe mkweli tu useme yaliyoko moyoni mwako?

Inaonekana wewe huyu mtu kuwa Chadema au kuwa muislam kinakukera sana
Hayo si masuala yake na muumba wake?

Haliwezekani kwa nani?
Wewe umegeuka Mungu wa kumhukumu huyo ndugu?
Hebu acha mambo ya ajabu!!

Kama lile jibu langu nililokujibu kwa ufupi hujalielewa na kuliafiki basi nadhan sina cha kukusaidia zaid

Pole kama nitakuwa nimeuimiza hisia zako
 
Halafu angalia anaoshirikiana nao ni wale wale ambao kila kukicha wanapata ban ajili ya kuhubiri udini. Kakosea sana sahivi unaona anajibu kisiasa zaidi badala ya kudefend hoja zake.

Huyu kunakoelekea atatafutia watu ban kutokana na majibu yake mepesi mepesi.

Mkuu kuwa makini sana kukerwa na mtu ambae anaonekana kabisa anaongozwa na hisia kujibu hoja

Akikusababishia BAN mtu wa aina hiyo mwenye matatizo utaonekana ni wewe

Mwenye busara hamkimbizi mwendawazimu aliyechukua nguo zake akiwa anaoga
Bali
hutafuta namna ya kujisitiri kisha ndipo huchukua hatua.......!!!!
 
Kama lile jibu langu nililokujibu kwa ufupi hujalielewa na kuliafiki basi nadhan sina cha kukusaidia zaid

Pole kama nitakuwa nimeuimiza hisia zako

Sema tu huna majibu kwa maswali unayoulizwa

Ukikubali hilo utaonekana ni muungwana kabisa!!
 
Kwanin unakuwa na hasira mkuu??

kuwaambia ukweli wanasiasa na kusimamia haki yetu wewe kipi unaumia??

Huna haja ya kujitafutia ban,kama unaona mjadala hauna tija kwako ruksa kuondoka

Tuachie tujadili

Always watu wa design yako hayo uliyojibu ndo defending mechanism.

Kaka acha udini fanya kazi, this is too low to you.
 
Kwanin unakuwa na hasira mkuu??

kuwaambia ukweli wanasiasa na kusimamia haki yetu wewe kipi unaumia??

Huna haja ya kujitafutia ban,kama unaona mjadala hauna tija kwako ruksa kuondoka

Tuachie tujadili

Kama kweli unakijua unachokizungumza niambie Ukweli ni kitu gani ....!!!!!!!!!!
 
My friend, kwa upeo wako ni mzuri sana japo si kila mmoja ana hisia kama zako. labda ni kweli au si kweli. Ila ukiangalia sana unaweza kuta kinachokutafuna kimekukaa nguoni mwako.
Malumbano ya Kidini si mazuri na kama tukishindanisha maneno sana Amani haijengeki sana
 
Mkuu kuwa makini sana kukerwa na mtu ambae anaonekana kabisa anaongozwa na hisia kujibu hoja

Akikusababishia BAN mtu wa aina hiyo mwenye matatizo utaonekana ni wewe

Mwenye busara hamkimbizi mwendawazimu aliyechukua nguo zake akiwa anaoga
Bali
hutafuta namna ya kujisitiri kisha ndipo huchukua hatua.......!!!!

Mwambie hana haja ya kujitafutia BAN

Its very simple,kama anaona huu ni uchafu niliouandika a-logg - off tuh

Sio lazima kwake kukaa kwenye mjadaka unaomkwaza hisia zake
 
My friend, kwa upeo wako ni mzuri sana japo si kila mmoja ana hisia kama zako. labda ni kweli au si kweli. Ila ukiangalia sana unaweza kuta kinachokutafuna kimekukaa nguoni mwako.
Malumbano ya Kidini si mazuri na kama tukishindanisha maneno sana Amani haijengeki sana

Ni kweli,

Kuna watu wana mihemko mikali,ukweli ukisemwa hawataki kuukubali au kuupinga kwa hoja zenye mashiko,

hilo ni tatizo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom