Kwangu Mimi Makabi Lilepo ni bora maradufu ya Louis Miquissone aliyechoka na asiye na jipya tena

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,852
109,552
Nimesikitika sana kusikia kuwa ni kweli aliyewahi kuwa Mchezaji wetu Louis Miquissone anarejea Simba SC.

Mwaka jana Novemba na mwaka huu March kuna Kiongozi Mwandamizi wa Simba SC alienda Kumfuatilia na majibu yake GENTAMYCINE niliyasikia yakisema.

"Hakuna Mchezaji tena pale na kama Tajiri anataka Kutengeneza Kikosi chetu aachane nae haraka na atizame Wachezaji mahiri Wengine"

GENTAMYCINE nami kwa Jicho langu Kali na la Kiufundi nikalazimika kuomba Mikanda kadhaa ya Timu zake alizocheza na Kujiridhisha tena kwa 100% kuwa hana Uwezo wake alioondoka nao alipokuwa nasi Simba SC.

Kwanini hii Fedha mnayomsajilia msingemsajili Complete Package Player Makabi GENTAMYCINE Lolepo na siyo Mchovu Louis adriz Miquissone?

Sikubaliani na Usajili wake japo nawaheshimu Viongozi kwa kuamua Kumrejesha kwani huenda wakawa Wameona zaidi yangu hasa Kiufundi na hata Kibiashara ( Kimasoko ) kwa sasa na baadae.

Hakuna Mchezaji ambaye ananiuma kwa Kutosajiliwa na Simba SC yangu kama Makabi Lilepo ambaye ndiyo inasemekana ( kwa mujibu wa chanzo changu ninachokiamini kwa 50% tu ) kuwa ndiyo Namba Sita iliyoimbwa na Yanga SC kwa Mwezi sasa ( nikimaanisha ndiye atakayetambulishwa leo ) Usiku wa Saa 6 Kamili na Kesho Kutembezwa Jijini Dar es Salaam na kupelekwa zilipo Ofisi za CRDB Makao Makuu.
 
Wewe nani hasa kwenye SIMBA?
Mimi ni GENTAMYCINE Media and Communication Expert, Chief Propagandist, a blessed Tanzania Football Pundit, Senior Simba SC Fan, Education, Social and Sports Advisor, Genius from Mara and Mtwara Regions and a JamiiForums Keyboard Warrior.

Be free to ask more questions please.

Cc: adriz, Bila bila and Bujibuji Simba Nyamaume
 
Mimi ni GENTAMYCINE Media and Communication Expert, Chief Propagandist, a blessed Tanzania Football Pundit, Senior Simba SC Fan, Education, Social and Sports Advisor, Genius from Mara and Mtwara Regions and a JamiiForums Keyboard Warrior.

Be free to ask more questions please.

Cc: adriz, Bila bila and Bujibuji Simba Nyamaume
Duh hii CV siyo ya kawaida. Au ndo mafundi wanaita CV joint?
 
Hii biashara ya kuuza na kununua bidhaa ileile sio
Tumuombe a-perform japo upepo aliokuwa nao unaweza kuwa tofauti na atakaorudi nao
 
Back
Top Bottom