Mgibeon
JF-Expert Member
- Aug 7, 2011
- 11,141
- 20,787
Nilikua nafuatilia hotuba za muheshimiwa Rais alizokua akitoa huko Kigoma na Tabora wakati alipoenda kuzindua miradi mbalimbali ikiwemo barabara na miradi ya maji.
Katika kuongea kwake akasema kwamba Tanzania wakati inasisiwa na Baba wa Taifa ilikua na makabila 121, na katika jambo kubwa alilofanya na alilofanikiwa Hayati huyu ni kuwaunganisha watanzania wote pasikujali makabila yote.. Sasa katika kuongea akasema sasa Tanzania imekua na makabila 123 baada ya makabila mawili kuongezeka Wahutu na Watutsi..
Nimejiuliza sana, hawa ndugu zetu wameingia lini kwenye listi ya makabila yetu? Au kamaanisha kua wale waliohuku Tanzania wamepewa "ukabila" sawa tu na wale wanaopewa uraia"? Au muheshimiwa sana alikua anatania tu? Hebu ndugu zangu nifahamisheni kuhusu jambo hili zito, huenda mimi nilipitwa na habari za kurasimisha makabila haya ya jirani zetu.