Umewahi kujiuliza kwa nini nchi za Ulaya zinaendelea kutajirika kila kukicha huku za kwetu zikiendelea Kumasikinika? Umewahi kujiuliza kwa nini wakati Life Expectancy kwao Ikiongezeka kwetu ndiyo inapungua zaidi? Umewahi kujiuliza kwa nini idadi ya watu kwao inapungua wakati kwetu ndo kwanza tunazaliana? Umewahi kujiuliza kwa nini 'vijiji' vyao vinakua kwa kasi wakati vya kwetu ndo Vinachakaa?
Kwa miaka mingi sana nimekuwa na fikra tofauti na wengine kuhusu umasikini na hali duni ya afya katika nchi zetu za bara la tatu. Japo hadi sasa bado ni mwanafunzi wa Human mind lakini maarifa ambayo nimejikusanyia hadi sasa yananitosha kuandika makala hii.
Mkuu mimi nekuosma na nitatofautiana na wewe sehemu kadhaa kwa sababu mimi natazama WAPI TULIPO na tutaweza vipi kusonga mbele kutoka hapa tulipo na sii kuwatazama ambao tayari wameisha fika wakutakako..It's very logic, kabisa kwamba nyenzo zetu ni tofauti kabisa..Kwa mtu aliyetumbukia ktk shimo au amekwamba ktk tope huwezi kumpa koleo ajiomboe kwa sababu ndio nyenzo inayozunngumziwa sana na Nchi tajiri..
Msemo wangu siku zote - WATU na MAZINGIRA waliyopo siku zote ndio huzaa creative thinking ktk maamuzi magumu na kuweka mikakati na maazimio. Leo hii Tanzania tuna furnish mahitaji yetu kimaendeleo zaidi ya kuondokana ktk umaskini maana tumeshaukubali kuwa ni sehemu ya maisha yetu... Look around you!
Tumeleta Umeme na hata huo mradi wa MCHUCHUMA kwa sababu wananchi hawana umeme, umeletewa Richmond kwa usanii kwa sababu ya upungufu wa umeme ktk jiji la Dar kwa kutazama mahitaji na Mtanzania na sio mahitaji ya uzalishaji. Tumejenga misingi yote ya kiuchumi kukidhi wahitaji yetu badala ya kukidhi masoko ya nje kuuza. Tupo sawa kabisa na mkulima kijijini anayelima mazao ya chakula kwa jili ya familia na sii kwa ajili ya biashara na miaka yote amekuwa akitumikia tumbo lake la umaskini maskini na akaridhika. We have gone nowhere!.. Huu ndio mtazama wa Watanzania kwa ujumla na hauwezi kufanisiwa kwa kufikiria ama kutazam matumbo yetu..
Hakuna linalotendeka nchini kuwa ni la bahati mbaya hakuna.. Reli ya kati imekufa kwa sababu hatutarajii kuongeza export na sii ajabu we export almost nothing kupitia reli so why bother. watu wanataka kuona ATC ikifa kwa sababu we don't think of export bali usafiri wa kwenda Mwanza, Kigoma na Mbeya! Tutaweza vipi kupata maendeleo ikiwa fikra zetu wenyewe ni kuboresha maisha ya wananchi - maneno ya rais wetu JK - MAISHA BORA KWA KILA MWANANCHI hayatanguliwi na kuboresha sera za uzalishaji kwa kutazam soko la nje kwa bidhaa zetu. Kila kiongozi anatazama uchumi wetu kisiasa zaidi ktk kuridhisha Watanzania badala ya kujenga sera bora za uzalishaji, kulinda na kujenga faida ambazo ndizo zitakazoboresha maisha ya wananchi wake. The more investment for export the more we create jobs.. while unalinda viwanda vya ndani kukidhi mahitaji ya ndani, ndio maana siku hizo small industries zinapata unamaarufu kwa sababu hawa wanatazama nyanja zote za mahitaji ya ndani na sio maswala makubwa ya exports..
China leo hii duniani ni mteja mkubwa wa oil and coal ktk imports zake.
China's hunger for resources is unsustainable yaani toka chakula steel hadi mchanga nikubwa sana. Haya sisi ndio kwanza tumekwenda wakabidhi Coal wao kwa kutaka watuletee umeme ambao hatujui watawauzia bei gani Tanesco. Kesho Tanesco wakisema umeme umepanda tunaanza kulalamika while we had a chance ya kuuza Coal China sisi wenyewe na tukatengeneza faida yetu wenyewe tukazalisha umeme na kadhalika.. lakini ndio kwanza tumeenda wakabidhi wao shamba na duka la kujiuzia mali yetu kwa ahadi ya Umeme kukidhi tu mahitaji yetu.Yaani tunakula toka dukani ile biashara ya Washihiri - Kumradhini mtanisamehe!
Hivyo, sio kweli kwamba we lack creative thinking bali hatujui tulipokwama, tulikwama vipi na tutaweza vipi kujikwamua na ndio maana wazungu na IMF wametutupia koleo la kuzidi kujichimbia tukiwa ndani shimoni. We have run out of ideas kwa sababu tumeridhika na kuwepo shimoni tukisaidia kutupiwa misaada ya chakula na maji while THEY figure out for us solutions ya kutuondoa ktk Umaskini..Hatuna sababu kabisa kwa nini reli ya kati na juu imekufa, kwanini bandari za Tanga na Mtwara zimekufa, kwa nini ATC imekufa, Shirikka la meli limekufa..yaani vitu vyote muhimu kwa boost export vinakufa na ndio kwanza tunasherekea kufa kwake..
Binafsi naamini kabisa tunaweza fanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi ikiwa tutaweka misingi bora ya kuzalisha uchumi wetu kwa kutazama soko nje. wengine mnaita Tiger economy lakini ukweli siku zote unabakia kwamba unapouza zaidi ya mahitaji yako ndipo unapoboresha faida na maisha yako kwa ujumla. Huwezi kutafuta mtaji ili ujenge nyumba bali nyumba ni matokeo na matunda ya kazi uloifanya. Hao Japan na nchi zote zilizoendelea kwa kila wanachokifanya leo ni kutazama watauza wapi mali zao..
Hii ndio asili ya Ubepari - freee market economy ni kuwezeshwa sisi kuzalisha mali na tukaziuza nje kulingana na soko lililopo nje na sii kutazama mahitaji yetu sisi kuwa kigezo cha maendeleo..Hizi ni fikra za Kikomunist, fikra za woga na kujilinda dhidi ya kukoloniwa wakati umekwama na kuwa mhitaji zaidi ulipokwama badala ya kufikiria mbinu za kujikwamua..
Huwezi kuzugumzia medical Aid na Insurance kwa watu maskini ambao pato lao kwa siku ni dollar 1. Na huwezi kuzungumzia kukuza Elimu kwa kutoza karo jamii ambayo asilimia 80 hawana uwezo. WE LACK CREATIVE THINKING kwa sababu, we copy and paste mambo mengi sana kutoka Ulaya na ndio maana tumefikia kuchukua lugha ya Kiingereza kama njia ya kufundishia Elimu... hatuna sababu yoyote ya msingi zaidi ya ku copy and paste.. Hivyo, vijana wetu hawaoni umuhimu wa elimu ikiwa swala ni kujifunza lugha ambayo wataijua huko mitaani na Madisco ndiko lugha inapojengwa kwa nini aende darasani?..
Sasa muulize Mtanzania wa kawaida maana ya CEO au hata tafsiri yake - Vijana wengi sana hawajui Kiswahili chake, lakini waulize maana na PEDEGEE watakambia ni President Director General... wow haya ndio cheo gani hicho? - aaah sii unamuona Papa Msovu - huyo ndio Pedegee bana. Kwa hiyo tunajifunza yasiyotakiwa kujifunza. Ya japan yaacheni Japan, tujitazame sisi tumekwama wapi na tunatakiwa kujikwamua vipi ktk mazingira haya.