Kwako mmiliki wa kampuni ya mabasi ya SuperFeo

Planett

JF-Expert Member
Mar 20, 2014
10,419
15,974
Popote pale ulipo kama unasoma uzi huu tafadhali sikiliza ombi langu lifuatalo.

Kwa heshma na taadhima najua kwamba wewe ni mzoefu wa masuala ya usafirishaji wa abiria na fitna zote kwenye sekta hii unazijua.

Kama ikikupendeza ulete mabasi barabara ya Dar es salaam kwenda Kilwa kivinje/masoko.

Sababu ya kukuomba uingie route hii ni kutokana na mtu mmoja ku-dominate route na kila anayekuja anaikimbia.

Namshukuru Ngombale kidooogo analeta ushindani lakini bado. Karibu sana ulete ushindani ili huduma ziwe bora na zenye viwango.

Kabla hujaja waulize wamiliki wa SWAHILI na TASHRIFU kwanini wamekimbia route na kumuachia mtu mmoja atawale ilihali kuna abiria wengi?

Naimani ombi langu utalifikiria.
Ndimi abiria/mwananchi wa Kilwa.
 
Kwenye njia ya Kigoma kina Adventure, Saratoga na Takbir walikuwa na magenge ya utekaji mabasi ya abiria kitu kilichopelekea wengine waikimbie hiyo njia.

Hatimaye magenge yamesambalatishwa na jeshi imara la polisi tanzania. Sijui huko wanatumia njia gani?
 
Hivi haya mambo kumbe yapo sehemu nyingi, sisi wenyewe kutoka mkoani kwenda kijijini kwetu ametawala mtu mmoja miaka nenda rudi akija mwingine anakimbia mbaya zaidi gari iko moja inaondoka alfajiri ukichelewa hiyo ndio imetoka unaanza kurudi nyumbani na mabegi yako
 
Wapi huko mkuu?
 
Kweli kuna mikoa bado ipo nyuma.

Nashukuru mungu kwetu kaskazini unapata usafiri wowote uutakao kwanzia hiace,coster,noah,bajaji,pikipiki,mabus,pickup,baiskeli...yani ni wew tu
Hivi haya mambo kumbe yapo sehemu nyingi, sisi wenyewe kutoka mkoani kwenda kijijini kwetu ametawala mtu mmoja miaka nenda rudi akija mwingine anakimbia mbaya zaidi gari iko moja inaondoka alfajiri ukichelewa hiyo ndio imetoka unaanza kurudi nyumbani na mabegi yako
 
Usicheze na watu wa kilwa mzee acha kabisa nliwai kuwa na project uko nkaona fursa ya kufungua sehemu ya chakula nlikatazwa na ndugu zangu
Wewe jiulize kwanini kuna hotel moja kunwa apo kilwa ambayo ni Nangurukuru hakuna hotel nyingine kilwa kwa mambo ya shirki ni hatari lazima watu wakimbie njia
 
Huko sio usafirishaji tuu hata shule ni balaa ! Piga mtoto wa mtu viboko uone utakula za uso balaa ! Kilwa wapo vizuri kwa ulozi
 
Back
Top Bottom