Abeid L Msanganzila
Senior Member
- Dec 30, 2018
- 121
- 209
Habari za mchana huu wadau wote wa jf?
Poleni na mihangaiko ya kutafta pesa. Mtaani kugumu kweli, kila kitu bei juuu😆
Niende kwenye point!
Wilaya ya Nkasi ni moja ya wilaya za mkoa wa Rukwa. Hii wilaya ina uhaba mkubwa sana wa maji. Mito ni mingi ila asilimia 90 ni mito ya msimu mmoja, yaani msimu wa mvua nyingi! Sasa serikali kupitia wizara yake ya maji ilishaanzisha mradi wa maji ambao huu mradi ulishakamilika ila cha ajabu maji hayatoki.
Kwanini maji hayatoki? Ipo hivi kuna watu walivyoona changamoto ya maji wilayani Nkasi hususani tarafa ya Namanyere waliigeuza fursa kwa kuchimba visima virefu ili kuuza maji kwa wananchi!
Sasa baada ya mradi wa maji kukamilika hawa watu nasikia wanatembeza cheji Halimashauri ili maji ya mradi toka mto mfili yasitoke na ndivyo inavyofanyika hadi sasa! Maji yananunuliwa shilingi 500 kwa ndoo moja ya lita 20!
Watu wanahangaika na maji sanaaa hadi maji yanayonywewa si salama kabisa kwa afya za watu!
Juzi kati walivyosikia kuna ziara ya makamu wa raisi wakayafungulia maji yakaanza kutoka na watu wengi wameyavuta majumbani mwao. Sasa ziara ilivyoyeyuka tayari wamerudi mtindo wao wa zamani wamefunga maji hakuna kutoka.
Wizara ya maji sijui huwa haina utaratibu wa kutembelea miradi yao ili kujiridhisha kama ripoti wanazopokea ofsini ni sahihi ama si sahihi! Wwnachi tunateseka na ugumu wa maisha tunateseka tena na uhaba wa maji/ bei juu za maji. Yani imefika hatua watu tumeanza kupanga ratiba ya kuoga mara mbili kwa wiki.
Najua humu kuna watu walio ndani ya hii wizara, plz tusaidieni wananchi wenu zidi ya wenye nazo jamani! Kisa mtu ana hela basi anataka tununue maji kwake kwa bei juu na tuachane na maji ya mradi wa wizara kwa bei chini.
Nchi ngumu hiii! Aweso amka kijana watu wanalia hukuuuu!