Kwako JK (Shairi)

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,459
29,153
[h=5]Mpoto alituma salamu, ukavunga ujazisikia
Roma akashika kalamu, nyimbo akakuandikia
We una akili timamu, sema tu hutaki zitumia
au mpaka imwagike damu, ndiyo utajua tunaumia?

Izzo-B akamtuma rizi1, Kaka umetukaukia
Nami naenda Mtandaoni, Jibu nasubiria
Natoa Yangu Maoni, Maisha Kulalamikia
au mpaka imwagike damu, ndiyo utajua tunaumia?

Maisha Magumu Jamani, au kwako wayaonaje?
Ntaabika Maishani, Sijui kesho Ikoje,
Nataabika Mtaani, Ahadi zako nizingoje
au mpaka imwagike damu, ndiyo utajua tunaumia?

[/h]
 
JIBU KUTOKA IKULU
damu haimwagiki,na haki haitendeki
umekaa unataka HAKI?,utabaki kama MWALIMU na Chaki
mi ni maji we samaki,ila kihesabu ni buku na laki
mnachoongea siwasikii,niko bize naskiliza muziki (wa mipasho):biggrin:
 
Ari Mpya Kasi Mpya, Ahadi ulituletea
Vilevile Nguvu Mpya, Mbele Uliongezea
Ukweli Maisha Mapya, Kwako tulitegemea,
Chonde Chonde Mkuu, Mtaani ni Kugumu.

Mbona watutenga, nasi tulikuchagua,
Imani tulijenga, Daktari kutuagua,
Machozi yanilenga, Njaa yanikwangua,
Chondechonde mkuu, Mtaani Kugumu.
 
Ari Mpya Kasi Mpya, Ahadi ulituletea
Vilevile Nguvu Mpya, Mbele Uliongezea
Ukweli Maisha Mapya, Kwako tulitegemea,
Chonde Chonde Mkuu, Mtaani ni Kugumu.

Mbona watutenga, nasi tulikuchagua,
Imani tulijenga, Daktari kutuagua,
Machozi yanilenga, Njaa yanikwangua,
Chondechonde mkuu, Mtaani Kugumu.

Hapa siongei na Riziwani
naongea na baba yake
asitufanye maayawani watz si tuteseke
Ajiulize atajibu nini mbele ya Muumba wake
Kafisadi mpaka madini
Mwana-Apolo vipi atoke?
 
nilishasema hadi kuchoka nchi hii nimeichoka,
mambo yanavyoendeshwa si kama tulipotoka,
kila nikifikiria machozi yananitoka,
sijui lini mtanzania anaweza kuokoka.

tukijipanga kwa ufanisi nchi tutaikomboa,
wala rushwa na mafisadi hakika tutawaondoa,
majumba yao ya kifahari nakwambia tutayabomoa.
tuijenge tanzania mpya wafilisi kuwachomoa.
 
huyu raisi anajua hatukumchagua ndio maana hatujali,pia analipa kofia,kanga,fulana,wali maharagwe mliokula.
He was not chosen by us they just put him by fliping the results

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Mpoto alituma salamu, ukavunga ujazisikia
Roma akashika kalamu, nyimbo akakuandikia
We una akili timamu, sema tu hutaki zitumia
au mpaka imwagike damu, ndiyo utajua tunaumia?

Izzo-B akamtuma rizi1, Kaka umetukaukia
Nami naenda Mtandaoni, Jibu nasubiria
Natoa Yangu Maoni, Maisha Kulalamikia
au mpaka imwagike damu, ndiyo utajua tunaumia?

Maisha Magumu Jamani, au kwako wayaonaje?
Ntaabika Maishani, Sijui kesho Ikoje,
Nataabika Mtaani, Ahadi zako nizingoje
au mpaka imwagike damu, ndiyo utajua tunaumia?

attachment.php
 
nilishasema hadi kuchoka nchi hii nimeichoka,
mambo yanavyoendeshwa si kama tulipotoka,
kila nikifikiria machozi yananitoka,
sijui lini mtanzania anaweza kuokoka.

tukijipanga kwa ufanisi nchi tutaikomboa,
wala rushwa na mafisadi hakika tutawaondoa,
majumba yao ya kifahari nakwambia tutayabomoa.
tuijenge tanzania mpya wafilisi kuwachomoa.
hii tu ndio njia rahisi hamna nyingine
2015
attachment.php
 
Asiposikia muambieni ajaribu kufanya machache tu kati ya yale yaliyoimbwa na Jeremiah (Ningekuwa Rais)!!
 
mkuu the boss
kumbe hata huku huwa unapitia?

napenda mashairi
only ya siasa za kulalamika yananitia uvivu
nimewapa pole kwa kulia lia sana

mimi nilishaamua nitaishi as if nipo ugenini,mind my bussiness zaidi..
sitaki stress za siasa
 
napenda mashairi
only ya siasa za kulalamika yananitia uvivu
nimewapa pole kwa kulia lia sana

mimi nilishaamua nitaishi as if nipo ugenini,mind my bussiness zaidi..
sitaki stress za siasa

mkuu unakosea huwezi kuishi kama upo ugenini na hali upo nchini na nina uhakika yanayofanyika humu nchini yanakugusa. siasa si kwa ajili ya wanasiasa inamgusa kila mtu na kumuaffect kwa namna moja ama nyingine. na kwa uzalendo zaidi huwezi kusema unamind bussiness zako kwani unajidanganya mkuu. hizo business zako zinaafectiwa na namna nchi hii inavyopelekw kila mtu akimind business zake nani ataikomboa nchi.
naamini wewe ni mzalendo ila hujaamua ama umekata tamaa. kupiga kelele na kulalamika ni sehemu ya kuleta mabadikilo kwani inaprove that there is conflict in the society, and karl marx once said conflict leads to change in any society.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom